Wadau wapi naweza kupata notice za sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kulingana na mtahala (syllabus) za wizara ya elimu Tanzania.
Wapi naweza kuzipakua (download) kwa ajili ya vijana wetu? Wengi wetu tunaweza kuwa na changamoto ya hili jambo maana unaweza ukawa na kijana akataka...
Mzazi ana watoto wawili aliowasomesha kwa tabu hadi chuo kikuu lakini wote wako nyumbani na hakuna mwenye ajira hata mmoja. Leo mzazi huyu kumpeleka mtoto sekondari tena anaona ni kumtania kabisaaa.
Hiyo ndo sababu ya uripoti duni wa wanafunzi wa kidato cha kwanza; 2023 ulikuwa mkubwa lakini...
Utekelezaji wa Mtaala mpya kuanza Januari 2024
Mnamo tarehe 02 Novemba 2023, Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa(Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alitoa taarifa rasmi juu ya kuidhinishwa kwa Sera ya Elimu na Mafunzo 2014, Toleo la 2023 na Mitaala ya Elimu Ngazi ya Elimu ya Awali...
Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Baraza la Mitihani la Tanzania zimekamilisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2024.
Uchaguzi ulihusisha wanafunzi 1,092,984 wakiwemo Wasichana 507,933 na Wavulana 585, 051...
Wadau, nimesikiliza na kufuatilia swala la kupotea binti Warda Mohamed mwanafunzi wa kidato cha kwanza huko kibaha, hakika inasikitisha jinsi Mamlaka husika yaani polisi na oficin ya mkuu wa wilaya Nick wa pili jinsi ambavyo wamelikalia kimya swala la huyu binti aliepotea tangu Mwezi wa nne...
Mwanza, Tanzania
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Elimu - wizara ya TAMISEMI Dr. Charles Enock Msonde na Dr. Lyabwene Mtahabwa - kamnishna wa elimu kutoka wizara ya elimu wahimiza waalimu wa darasa la kwanza na darasa la tatu shule ya msingi wawe mahiri ktk masomo yao huku vigezo vya lazima...
Wanafunzi 11,413 ambao ni asilimia 45 ya wanafunzi 25,362 waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule wa sekondari mkoani hapa hawajaripoti shuleni tangu shule hizo zilipofunguliwa Januari 9 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga amesema hayo Februari 2, 2023 wakati akitoa...
Habari!
Nimefuatilia habari za mikoa mbalimbali na wilaya zake, watoto wengi ambao wamepangiwa shule za sekondari kuanza kidato cha kwanza hawajaripoti shule mpaka leo. Yawezekana wapo wazazi ambao wanajichanga ili wawapeleke watoto wao shule na pia wazazi wengine hawana mpango wowote.
Yote...
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumapili Januari 15, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msingwa, wanafunzi 354,277 wakiwemo wenye ulemavu 697, ndiyo walioripoti hadi sasa kati ya wanafunzi 1,070,941 wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza sawa na asilimia 33 ya matarajio.
Aidha amesema...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa #TAMISEMI, Angellah Kairuki ameagiza Uongozi wa Mkoa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha Wanafunzi hao wanaripoti Shule mapema iwezekanavyo.
Idadi hiyo ambayo ni sawa na 55.2% ya Wanafunzi waliotakiwa kuwa Darasani mpaka sasa...
Wanafunzi 2,096 kati ya 2,194 waliofanya mtihani wa marudio wa darasa la saba, wamefaulu mtihani huo na kupangiwa shule za sekondari za serikali kuanza kidato cha kwanza.
Wanafunzi hao 2,194 wakiwemo wavulana 1,117 na wasichana 1,077 walifanya mitihani yao Desemba 21 na 22, 2022 kwa sababu ya...
Ikiwa wiki moja imepita tangu kuanza kwa msimu wa masomo mwaka 2023 Tanzania, wanafunzi wanne kati ya wanafunzi 88 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Izumachel iliyopo wilayani Geita mkoani hapo ndio walioripoti katika shule hiyo.
Shule hiyo iliyoanza mwaka 2022...
Zaidi ya wanafunzi 13,000 sawa na asilimia 63 wa kidato cha kwanza mkoani Songwe waliochaguliwa kuanza masomo Januari 9 mwaka huu, hawajaripoti shuleni hadi leo Ijumaa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda amesema hayo leo wakati akitoa salamu za mkoa katika kikao kazi cha...
Uchache wa Shule za Bweni nchini umesababisha Wanafunzi 46,251 kukosa nafasi ya kujiunga na Shule zenye huduma hiyo Nchini
Idadi ya Shule za Serikali zinazochukua Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza mwaka 2023 ni 4,307 ambapo Shule za Kutwa ni 4269 na Bweni ni 38 zenye uwezo wa kupokea Wanafunzi...
Rais Samia Suluhu anaendelea kuupiga mwingi sekta ya elimu alianzisha mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 8000 nchi nzima vyenye thamani ya Tsh Bilioni 160 sasa madarasa yamekamilika kwa asilimia 95 na kupelekea wanafunzi wote kuanza masomo kwa pamoja.
Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na...
Takriban wanafunzi milioni moja wanatarajia kujiunga kidato cha kwanza kwenye shule za Serikali mwakani huku changamoto ikiwa ni upungufu wa vyumba vya madarasa.
Takwimu za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Baraza ka Mitihani Tanzania (Necta) zinaonyesha shule...
Mimi labda sijaelewa.
Unakuta shule ya msingi A, ina wanafunzi 123 waliomaliza darasa la saba na wamafaulu wote kuingia kidato cha kwanza mwaka 2023.
Cha kushangaza wanafunzi wote wa hiyo shule ya msingi A wamepangiwa shule moja tu ya sekondari iliyopo kwenye hiyo kata kujiunga na kidato cha...
Wanafunzi 1, 073, 941 waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022 wakiwemo wavulana 514, 846 na wasichana 559, 095 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Desemba 14, 2022 na Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki imesema kuwa...
Kuna suala la wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza ambao hawatakuwa na uwezo wa kununua sare waendelee na zile za shule ya msingi , kauli hiyo ilitolewa na aliyekuwa waziri wa Tamisemi.
Kiukweli nimeona mtazamo wa wengi juu ya suala ,kuna wengine wanasema kwamba sio mbaya waendelee nazo tu...
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema Wanafunzi wote wa Darasa la Saba 907,802 waliofaulu Watafanikiwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2022 kutokana ongezeko la Madarasa. Amesema Serikali imewezesha ujenzi wa Madarasa mapya elfu 15 Nchi nzima kwa mkupuo huku...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.