BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
WANAFUNZI zaidi ya sh 10,000 kati ya 56,827 walichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika Shule za Sekondari za Serikali mkoani Morogoro hawajaripoti na kusajiliwa hadi kufikia Februari 23, mwaka huu (2024).
Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisa Elimu Taaluma mkoa huo, Hildegard Saganda wakati akiwa kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Morogoro, imeeleza kuwa hadi kufikia Februari 23 idadi ya wanafunzi walioripoti na kusajiliwa shuleni ilikuwa 46,775 sawa na asilimia 82 kati yao wavulana ni 22,203 na wasichana ni 24,572.
Ametaja halmashauri zenye wanafunzi wengi kuwa ni Kilosa ambao waliochanguliwa ni 11,156 wakati walioripoti hadi kipindi hicho walikuwa 8,990 sawa na asilimia 81 ikifuatiwa na Manispaa ya Morogoro waliochanguliwa ni 9,885 na walioripoti 7,502 sawa na asilimia 76.