Kibongo bongo: How to let ladies know you own a car?

Kibongo bongo: How to let ladies know you own a car?

hahahaaa sidhani kama walishindwa kukupa jibu! labda kama hukuuliza kwa style hii.
hahah haya bhana.bila shaka sasa swali limeeleweka.
08_lagos38__01__630x420.jpg
 
Hahahahahaha lol! unataka kuangalia ownership siyo!? Haya bana. Kwani kuwa na gari ndiyo kuwa na mapenzi ya kweli!? Anaweza kuwa na gari kisha "akakupotezea muda wako" vile vile ukabaki unalalama yule mkaka kanipotezea muda wangu tu mshenzi sana yule lol!

Bora mmetujuza sahv tutaomba kwanza kadi ha ha ha kama traffic vile
 
Wanawake njoni huku mseme mnaonaje mafunguo yaloninginia kwenye majinzi yetu. Hii kitu ya kuninginiza mafungui nimeiona hata moshi, lakini arusha haipo saaaaana.

Arushaaa hakunaaa kabisaaaa hyoo kituu
 
Hahahaha!! wacha bana wee, maboy wa Nai hawatumii Probox, hizi huwa zinaletwa mjini na Wakikuyu wa kutoka vijijini wakizitumia kupiga hela na ndio maana zimejaa na kutuzingua mjini.

Hapo pa kumfanya demu ajue una gari kwa kunig'iniza ufunguo ni tabia ya vijana ma-hustler wa campus. Vidume kama sisi hatuna haja, kwa jinsi unavyotamba, unavyojirusha na kuagiza watu wapewe vitu na simu uliyonayo demu mwenyewe anajijazia aina ya gari ulionayo. Hafai kuhangaika akili kama una gari au la. Yaani ikatokea kwamba huna gari, atakushangaa sana ama adhani uliibiwa.
kui

Sasa unategemea utamwambia nini baada ya fujo zote ulizomuonyesha? Off course umeibiwa tena Mercedes benz Pullman guard ya 2014.
 
Last edited by a moderator:
Hahaaaa!, ati adhani uliibiwa.....lol!
Hategemei kuwa huna gari, it's not even a question to say the least!, kuonesha onesha mafunguo ni backward thinking kusema kweli. Mimi najua there's MORE, to life than owning a car, ndo nasema Kidume kikijileta matawi mimi ntajifanya mti kabsaa!, ntamuuliza what kind of car you're drving cause am alergic to certain cars....lol!

You are killing this soul over here! Nimecheka sana!
 
  • Thanks
Reactions: kui
Hahahahahaha lol! unataka kuangalia ownership siyo!? Haya bana. Kwani kuwa na gari ndiyo kuwa na mapenzi ya kweli!? Anaweza kuwa na gari kisha "akakupotezea muda wako" vile vile ukabaki unalalama yule mkaka kanipotezea muda wangu tu mshenzi sana yule lol!

kuwa na mwenye gari sio kua ndo guarantee ya kupata mapenzi la hasha ila kupunguziwa adha ya kutembelea tz 11, jua, vumbi n.k
 
wenye vi Toyota ndio wanaongoza kutundika mafunguo kwenye suruali

hukuti funguo ya the ultimate German driving machine mtu katundika kwenye suruali

Gari ni gari tu. Thamani zinatofautiana maana hata hizo Toyota zipo za mamia ya mamilioni. Ulishawahi kwenda nchi za Afrika Magharibi ukaona mikweche iliyopo huko ni ya magari gani? Ni Mercedes Benz ndio zinachafua (baadhi ya) miji kwa sababu ni rahisi ku-import hizo kutokea huko zitokeako. mwenye Toyota huko naye anaonekana matawi ya juu.

Kwa hiyo whether ni Toyota, Toyo, Benz, Audi, Renault, Chevrolet, Ford, etc..mwenye nayo akiamua kuning'iniza ka-funguo ili kujidakia ka Evelyn Salt kamoja mi naona poa tu!
 
Last edited by a moderator:
Hupendi kutembea kwenye vumbi huku umeshikwa kiuno? Utaona aibu kushikwa kiuno hadharani? Niliwahi kuulizwa hili swali sikulipenda kusema kweli. Ndiyo date ya kwanza Dinner & Dance sehemu moja maarufu sana jijini. Namkumbushia tu mrembo kesho Jumamosi nitakuja kukuchukua saa mbili akaniambia sawa likafuata swali, "Una gari?" nikamwambia mimi nimekwambia saa mbili nikukute uko tayari. Huwa nikimuona namtania na hili swali lake "una gari?" tunaishia kucheka tu lol!

kuwa na mwenye gari sio kua ndo guarantee ya kupata mapenzi la hasha ila kupunguziwa adha ya kutembelea tz 11, jua, vumbi n.k
 
Kugombea daladala tabu jamani nyie acheni tu
ni kweli ila ni bahati mbaya sana,kwa wengine magari ya kutembelea huyatumia kama super glue ya kunasia wadada.wadada nao kwa kuelewa au kutokuelewa hunasa kweli.it's like when the hunter becomes the target of the hunted .:lol::lol::eyebrows:
 
Nakumbuka nilichangia hii mada mwaka jana ila sasa naifuta kauli!! Naifuta kauli kwa kuwa nimejua umuhimu wa kuninginiza funguo...ilitokea ivi siku ya kwanza nilikuwa natokea namanga na gari yangu mpya , nilipofika mbele kidogo custom officer akanisimamisha tukakague GARI, nikazima gari then ufunguo mkononi! Nikazunguka nyuma ya gari ili mizigo ikaguliwe! Ikawa ni kupakua mizigo yote! Kijana nikajichanganya nikaweka ufunguo juu ya box uku tukishusha mabox, upepo ukaja kasi na kubamiza boot ikajifunga- kifuatacho nilimtafuta Fundi kubomoa kuutoa na kulazimika kulala mpakani! Fundi kufika tu akasema kwa kejeli! Lete hela si mnatuonaga sisi kuninginiza funguo kwenye suruali ni ushamba!! Lete pesa APA!! Ikala kwangu!!


Safari ikaendelea maisha takasonga!!

Kilichonifanya niunge mkono ujinga wa kuninginiza funguo ilikuwa mwezi wa January nilipoenda night club na kuweka kipochi cha funguo mfukoni pamoja na simu- wajanja wakavuta kipochi na cm! Muda wa kuondoka niliusaka ucunguo bila mafanikio-
Ikawa usiku ikawa asubuhi siku ya pili!
Kutafuta fundi niliambiwa funguo hauchongeki! Izi gari ukipoteza unaorder upya kwa manufacturer! Hapo ndio majonzi yalianza....sasa nikaingia kwenye website nikasubmit details ndio nikaletewa invoice ya USD 760 na order time 21 days!!
Nimepoteza 1,410,000/= eti kwa kuhofu kuninginiza funguo!!

Liwalo na liwe NIMEJIUNGA KWENYE CHAMA CHA WANINGINIZA FUNGUO!!

Gari mpya and u don't have a spare key or spare keys??!!
 
wadau wa MMU habari za toka mwaka jana.nakumbuka mara yangu ya mwisho kuanzisha mada hapa ilikuwa ni december 2014.nimekuja tena na mada nyepesi tu.bila shaka mtaipenda.

Kibongo Bongo: How to let ladies Know You Own a Car.
attachment.php


kuning'iniza funguo za gari kwenye suruali ndio habari ya mjini kwa sasa kwa wakaka wa mjini.haijalishi ni gari la kuazima au la kwake,ni ku-show off tu na kuning'iniza ''mafunguo'' kwa kwenda mbele ili kuopowa warembo.


rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia,moja ya vitu vinavyo "wapagawisha" sana wadada wa mijini,ni magari ya kutembelea.

gari ina mvuto sana ktk mapenzi na zimesababisha wadada wengi kujikuta wanatoa penzi bila hata wao kujitafakari kwa kina.


rafiki yangu huyo aliendelea kuniambia,kwa mkaka kuning'niza funguo za gari kwenye suruali,inamuongezea hadhi mbele ya mwanamke/wanawake,pia inasaidia kupeleka ujumbe wa kimya kimya kwamba "nimekuja na gari langu".


kwa sisi wakaka ambao tumeshindwa kumiliki hata vitz au toyota passo,tuwe wapole tu,mademu wenye viwango tutaishia kuwaota ndotoni,hatuna magari,tutaning'iniza nini?,labda funguo za bodaboda.:biggrin1:


they say if you've got it, flaunt it!.so ladies how do you provoke a brother if you want to notify him you own a car?.

Funguo zote ninazoziona hapo ni za Toyota tena za 2003 kushuka, over 10yrs old cars! Ningekuwa mimi hizo funguo ningeficha kabisa!
 
Funguo zote ninazoziona hapo ni za Toyota tena za 2003 kushuka, over 10yrs old cars! Ningekuwa mimi hizo funguo ningeficha kabisa!

mkuu yawezekana huo ndio umri wa gari ambazo vijana wengi wa kibongo wanazimudu kwa maana ya gharama.
kwa mfano,leo hii sidhani kama kuna chalii wa kipato cha kati anaweza kuagiza Toyota Rav4 ya mwaka 2014 japo Rav4 ni gari common sana bongo.labda kwa wale machali wauza sembe au watoto wa vigogo aka mafisadi.

Toyota Rav4 2014 2.5L 4WD GXR
2014_Toyota_Rav4_Front_2.jpg
 
Hupendi kutembea kwenye vumbi huku umeshikwa kiuno? Utaona aibu kushikwa kiuno hadharani? Niliwahi kuulizwa hili swali sikulipenda kusema kweli. Ndiyo date ya kwanza Dinner & Dance sehemu moja maarufu sana jijini. Namkumbushia tu mrembo kesho Jumamosi nitakuja kukuchukua saa mbili akaniambia sawa likafuata swali, "Una gari?" nikamwambia mimi nimekwambia saa mbili nikukute uko tayari. Huwa nikimuona namtania na hili swali lake "una gari?" tunaishia kucheka tu lol!

hehe!, kama alivosema Evelyn siku hizi tutauliza zaidi, kwanza kama unalo?, halafu ukifika unapigwa na, "Lisence and Registration Please?!,......lol!
 
Funguo zote ninazoziona hapo ni za Toyota tena za 2003 kushuka, over 10yrs old cars! Ningekuwa mimi hizo funguo ningeficha kabisa!

Asa lalee!, watu wana Zoom in!, chezea JF weyee!
 
lol! Khe khe kheeeeee! Sasa hapo ndipo mnapokusikia Kui. Mwingine anaweza kabisa kuwa na mapenzi ya kweli lakini swali kama hili linaweza kumfanya afikie hitimisho la kupoteza muda tu akishajichokea anasepa taratibu hivyo kumuacha mrembo akilalama "Yule mkaka alikuwa hana mapenzi ya kweli kanipotezea tu muda wangu" Mnapotanguliza maswali kama haya hata kabla ya penzi kuchanganya njemba hustuka na kufanya yao kwa kujua hapa hakuna penzi.

hehe!, kama alivosema Evelyn siku hizi tutauliza zaidi, kwanza kama unalo?, halafu ukifika unapigwa na, "Lisence and Registration Please?!,......lol!
 
hizi shobo za gari ziko vere siliasi eeee
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom