Playboy weds a good girl: inspired by true events

Mi-Ann

Member
Jun 9, 2020
81
150
1616934004341.png


Wiki iliyopita nlikua kwenye sherehe ya harusi. Well wanaooana wote nawafahamu. Bi harusi nilimfahamu kupitia bwana harusi. Bwana harusi nlimfahamu kupitia mzee wangu. I was very happy kwa bi harusi maana najua namna anavompenda mumewe. Ila namhurumia pia maana najua ubazazi wa bwana harusi. Yani haya mambo haya dah.

kabla ya kuendelea naomba niweke wazi, imebidi nichanganye kisa hiki na chai kidogo ili niendelee kuwa mtu nisiyejulikana.

I have known this guy for some time now. Haikua bahati mbaya kumfahamu, ni mdau mojawapo katika biashara za mshua. Sikuwahi kufikiria kabisa kuwa one day mi nayeye tunaweza kujikuta ktk mazingira yaliyosababisha niandike hapa. Siandiki kuomba ushauri, naandika tu ….. well sijui hata why nimeamua kuandika.

Mara nyingi hasa weekends ninapokua either bored home au nikijisikia tu, mm huamua kwenda kwenye moja ya ofisi za mzee. Ofisi hii huhitaji stationeries kila mara, hivyo tuna suppliers wanaotuletea hizo vitu atleast twice kwa mwezi. Moja wa suppliers ni ofisi ya Rajabu, au Raja kiufupi.

Raja sijui hata nimueleze vipi. Well, kwanza yeye na mzee wangu ni kama mtu na kaka yake. Maana kwanza ingawa mzee wangu ni mkubwa kwake, ila wamepishana miaka isiyozidi kumi. So kwangu ni mkubwa sana, yani kanizidi miaka kama kumi na tano hivi. Mtu mzima sana kwangu. Pili the guy ni mtu wa totoz. Yani kila akija kuleta mazaga pale ofisini anakua na toto, tena sio za umri wake, ni vibinti rika langu. Utajua tu ni toto zake kwa pozi zao. Tatu, Raja ni mtu wa pensi, kama lemutuz hahaha. Muda mwingi nikimuona ni katupia pensi na raba. Nne, the guy is financially good. Driving one of my favourite cars, Toyota Fortuner. Of course sio kwamba ndo gari expensive sana, bt ….. anyways, yuko njema kiasi chake.

Mi na yeye huwa ni Shikamoo…. Karibu ……. Sign hapa …. Etc. Na wala hakua na hiyana, shkamoo yangu huwa anaijibu fresh. Na mara zote huwa haachi kunitania. Utani ule wa kawaida tu, basi natabasamu pale, tunaagana. Ingawa ni mcheshi na mchangamfu, lakini pia yuko very systematic inapokuja kwenye kazi yake. Yani utofauti unauona kati ya yeye na suppliers wengine.

Raja pia yuko karibu na mzee. Sio ule u-best friend, hapana. Ila ni watu ambao wanafahamiana na mara chache naonaga kwenye picha za mzee akiwa kwenye function kadhaa wamepiga na Raja. Ktk moja ya picha za mzee alizopiga na Raja, nliona Raja yupo na mdada mwingine ambaye sijawahi muona akija naye pale ofisini. Uzuri niliona kwenye simu ya mama so nikamtania tu maza, “Dah huyu rafki yenu pendapenda sana, mi nikajua yule dada anakujaga nae ofisini ndo mtu wake”. Maza akanichekiiii, then akajibu kimkato tu, “huyu mkewe, Amina”. “Heeee, Ameoa kumbe?” nikajikuta nauliza swali kwa mshangao mkubwa. Maza hata hakujibu, “Hivi kazi zimeisha huko jikoni?” ndo jibu lake.

Tangu that day nimejua kaoa nikajikuta namkasirikia flani hivi. Yani hata akinikuta ofisini najikuta simuhudumii mimi. Hata akiniita sometimes nakausha, sometimes naitika. Najua hata yeye alihisi huyu binti ananichunia makusudi. Ila kiukweli sikupenda mtu aliyeoa alafu anakua anajionesha wazi na videm vyake namna ile. Sio heshima kwa mkewe hata kidogo.

Mmoja wa totoz za Raja ni Cessie. Cessie ni mdada flani hivi sober. Kaenda hewani, black beauty, sio mnene ila mashavu yamenona. Zile sura za mviringo. Ngozi yake ni Zaidi ya laini. Kwa kumuangalia tu unaona huyu hatoki kwenye shida. Sio mtu wa kuzikutia raha ukubwani. Na hata akitembea, hana haraka, na wima. Sio mtu wa kuona haya, au kuwa uncomfortable sehemu hata kama ni mgeni. Maana wengi wetu tukifika mahali na mabwana zetu, kama wao wapo bize, sisi tutazuga hapo tunaangalia simu au tunakaa kwa kujikunyata kwenye siti. Sio Cessie, atasalimia kila mtu pale. Kama kuna picha kwenye kuta atazikagua zote na kuuliza kitu asipoelewa. Tena sio ile kimcharuko, ana sauti flani ya upole na sura iliyojaa adabu na heshima. Yani hadi nikawa nashangaa why pisi ya aina yake inaamua kutoka na a married man.

Katika wadada wote anaotoka nao Raja, huyu alikua mchangamfu Zaidi kwangu. Na hata kipindi namchunia Raja, bado Cessie alikua ananitafuta nilipo na kupiga stori na mm. Ilikua ni kama anataka sana tuwe close. Na hata haikuwa tabu mimi kuzoeana na Cessie. Akaanza kunichatisha, mara kunialika kumsindikiza mahali nk. Mara zote nilisisitiza kama tunaenda mahali basi bwana ake asiwepo, na hakua na shida, “siwezi kuwa nae nikakualika Ann” ndo huwa jibu lake.

Ingawa ni kweli tukiwa na Cessie Raja huwa hayupo, ila kiuhalisia ni kama huwa yupo na sisi. Maana Cessie haipiti dkk tano hajamzungumzia Raja. Hadi siku moja nikamuuliza, “Cessie why uko na Raja?”. Cessie aliniangalia kwa dkk kadhaa. Sio kiukali ila kiudadisi. Sio kuwa alikua anatafuta jibu, nadhani alikua anajaribu kutafuta sababu ya mm kuuliza vile. “is it because he is older?”, aliniuliza hatimaye huku akichezea mrija uliokua umezama kwenye juice aliyokua anakunywa. Kwa mara ya kwanza nikaona Cessie yupo uncomfortable. Hata hakuwa ananiangalia. “No bana. Usinifikirie hivyo. Mambo ya umri mi huwa sijali sana, as long as watu wamependana. Nimeuliza tu”. Ilibidi niongee kwa upole sana ili asijisikie vibaya.

Ulipita ukimya wa muda tena. Cessie akiendelea kuchezea juice yake. Anazungusha ule mrija as if anakoroga sukari kwenye hiyo glass. Nikajua nilichouliza kimemtatiza sana. Na nikahisi kabisa sio jambo la umri lililomchanganya. Ikabidi nibadili mada fasta. “Baada ya kugraduate, whats your plan. you planning for a masters degree Cessie?”,. Cha ajabu Cessie akatabasamu. Akiwa bado anaangalia juice yake lakini. Hakuweza kuniangalia akiwa anatabasamu. Then akaniangalia. Kwa kuwa namfahamu, nliona kabisa unyevu kwa mbaaaali kwenye macho yake. Bt she was still smiling. “You know he is married right?”. Hatimaye aliniuliza. Sura yake haikua inaonesha kuudhika. Sikua na haja ya kudanganya kuwa nlikua sijui. Nikaitikia kwa kichwa.

“Well hata sijui why nlijikuta nafall kwa Raja. I guess I was moved by his way of showing how he cared for me. Sio how he loved me, no, how he cared for me”. Alianza kunihadithia Cessie. Akiwa amerudia pozi lake la kuchezea juice. Ila now alikua anachezea vile vitone vya maji kwenye kuta za nje ya glass ya baridi. Tabasamu lake lilionesha kabisa alifurahia anachokisimulia.

Siku moja niko kwenye foleni natoka makumbusho napanda chuo. Kufika pale Mwenge kulikua na bonge la foleni. Nikaona nishuke ili niprint kazi ambayo kesho yake asubuhi ilitakiwa tukaiwasilishe kwa Chuhila. Kama unavyomjua yule dokta hanaga utani kwenye issue za shule, sikutaka nichelewe nikute stationery shops zimefungwa. So nikashuka Mwenge. Nikazama stationery mojawapo pale. Kijana aliekua ananihudumia akacopy fresh ile kazi, tukasaidiana kuiedit. Kabla hatuja print umeme si ukakatika. Nikaona kimbembe hiki. Nikapiga simu chuo kuuliza kama umeme pande hizo utakuepo, naambiwa hakuna mama pambana hukohuko.

Nikamuuliza ule dogo kama anajua mahali wana generator. Akanielekeza. Kufika pale, naulizwa ina peji ngapi. Kuwaambia peji nne, wakaniambia kama ntawapa elfu ishirini wawashe jenereta. Dah. Nikarudi kwa yule dogo. Now alikua kasimama na jamaa mwingine, sikumtilia sana maanani yule mwingine. Nilichofanya nikamuomba dogo umeme ukija aniprintie then nitaifuata asbh sana. Dogo akanambie kama ni asbh sana atakua hajafungua. So nitafute mahali pengine nikaprint. Yule jamaa mwingine ndo akauliza kinachoendelea. “Boss huyu dada kazi yake hatuja iprint maana umeme ulikatika”. Nikajua kumbe huyu jamaa ni boss wa huyu dogo. “inahitajika lini hiyo kazi yako binti?” yule jamaa akaniuliza. “Ni kesho asbh sana”. Basi akanipa pole pale, bt akasuggest kitu. “kama unaweza niachia hiyo flash, ntahakikisha nakuprintia kazi yako, ninapokaa kuna jenereta”.

Nikamuangalia yule dogo kama kujihakikishia usalama wa flash yangu. Dogo hata hakuonesha kukubaliana au kukataa. Bt nikawaza, cha thamani kwenye hii flash ni hiyo kazi tu. Kama huyu kaka ndo mwenye hii stationery, hawezi potea na kitu kama flash, yenye document zisizo na thamani yoyote. Basi nikaitoa kwenye pochi nikamkabidhi. Nikamtajia nilivyosave hiyo document. Nikampa namba yangu pale tukaagana.

Usiku ule sikupata usingizi vizuri. Nilikua nawaza itakuaje jamaa asipokumbuka, au asipojali umuhimu wa hiyo kazi kwangu. Ile asbh imefika bafuni hata sikukaa sana. Naogopa simu isije ikaita nikiwa mbali nisisikie. Kadri muda wa kipindi ulivyokua unasogea ndivyo hali yangu ilivyokua inazidi kuwa mbaya. There were so many things that could have gone wrong. Kwanza kosa la kwanza ni kuwa sikuwa na namba yake. Aliahidi atanipigia ikiwa tayari, so sikumwambia anibeep wakati nampa flash. Kingine ni kuwa umeme haukua umerudi. So hata chaji ya simu yangu ilikua ni tiamajitiamaji.

Ikafika muda nikawa nishakubali matokeo. Kuwa ntamwambia dokta umeme haukuepo. Ingawa kwa Chuhila that’s no excuse at all. Kazi tumepewa mwezi mzima uliopita nilitakiwa niwe nishaimaliza. Mpaka naelekea class sikua nimepata simu ya jamaa. Ile nimeshaingia class kabisa, dkk tano kabla ya kipindi ndo simu inaita. “Hello, nipo maeneo ya chuo hapa, uko wapi” very calmly as if hajachelewa. “Yombo”, nikamjibu. “yombo ipi?” akauliza, “Yombo 3”, kumbe anafahamu vizuri ramani ya hiki chuo. Nikatoka nje kkumsubiri. Enzi hizo alikua anaendesha prado flani zile za zamani. Nikaiona prado inakuja, bt hata sikutilia maanani. Hadi ilipopaki karibu yangu na kushusha kioo. Sikuweza hata kumshukuru fresh, maana alikua tayari anaongea na simu nyingine. Akaonesha tu ishara kuwa he will call later. Hakupiga.

Wiki kama mbili zikapita. Nikiwa tena kwenye daladala mitaa ya Mwenge, nikaona gari yake imepaki mahali. Nikajua atakuepo stationery kwake. Nikashuka. Nia ni kwenda kumlipa kwa kuniprintia kazi yangu that day. Nimefika hata sikumkuta. Basi nikamuachia hela kama elfu tano, nikamwambia hii ni kazi iliprintiwa siku umeme umekatika. Kasema poa.

Jioni sana, ndo akapiga simu. Tukaongea tu kiufupi. Kaniuliza program nisomayo nikamtajia. Nikamshukuru kwa ukarimu. Tukaagana. Three days later tukakutana mlimani city. Kama kawaida kapiga pensi hahahah. Pembeni na kadada flani hivi kamejitanda. Yeye ndo wa kwanza kuniona. Akanisalimia pale kwa uchangamfu balaa. “Cessie eeh?” nikamjibu ndiyo. “shopping?” akaendelea kuuliza, “yeah natafuta simu, nliyokua natumia imeharibika”. “ndo unanuaga simu hapa siku zote? Maana kuna maeneo mengi tu same quality na cheaper kidogo”. Raja akazidi niuliza. Mm nikawa naona kama ntakua nambore yule dada mwingine, ila kumcheki hakuonekana kukereka. “no nliona tu hapa ni karibu”. “okay tufanye hivi, sisi tumemaliza hapa mizunguko, twende wote nikupeleke a very good phone shop mahali”.

Nikajua tunaenda wote watatu hadi kwenye hilo duka la simu. Bt tulipofika maeneo ya ubungo, yule dada mwingine akashuka. Haoo mpaka Sinza. Na kweli nikapata a good phone. Na ingawa alikua nahela ila wala hakuoffer kunilipia hahaha. Baada ya hapo akaniomba nimsindikize sehem nyingine, tukaenda. Nakumbuka that day tulifika hadi ofisini kwenu pale ila hukuwepo.

Nilijikuta nazoena sana na Raja. All the time hakuwahi kunitaka kimapenzi. Tumezurura sana, sometimes akiwa na demu wake, muda wote sikujua ameoa. Bt nlimheshimu pia kama kaka yangu tu. Nimefahamiana nae nikiwa mwaka wa pili semester ya kwanza, tukaendelea kuwa marafiki hadi nikiwa mwaka wa tatu. Imagine, just friends for more than a year. Katika muda wote huo nilimfahamu vizuri Raja. alikua a very kind man. lakini pia alikua anapenda sana gils. So nlijua kabisa the man sometimes cheats on his girlfriend. Bt nikawa namtania tu kuwa watakuua hawa wasichana, basi tunacheka. Hakua ananihonga kama kunihonga, Bt alikua anaweza kuhisi nikiwa na uhitaji. So aliweka kama utaratibu, kila mwezi lazima aniwekee kwenye account pesa. Mwanzo nikawa nazitoa nazirudisha, hadi aliponiambia nisihisi vibaya. He respects me as a sister, kama sizihitaji kwa sasa niziache huko benki mpaka siku nikizihitaji. Na ikawa hivyo. Huo utaratibu mpaka sasa anao, na nyingi hata sijazitumia bado.

So the day he slept with me. Najua ndo ulikua unasubiri nielezee hicho. Cessie aliongea huku akizidisha tabasamu kuonesha kuwa hajutii. Raja alikua kagombana na dem wake ambaye nlikua namfaham. Sikua nakapenda kale kadada hata hivyo, na sikushangaa walivotemana. So nadhani ingawa sikua najua ila akili yangu ishanambia huyu sasa yuko free. Mimi kipindi hicho nlikua na boyfriend pia. Nakumbuka ilikua ni jumapili asbh. Raja alishazoea kuniagiza baadhi ya vitu vya ofisi zake akiwa kabanwa na kazi. So alinipigia simu kuniambia kama nikipata muda niende Makumbusho kuna vitu nichukue ofisi ya pale nipeleke ofisi ya Shekilango. Nilikubali, ingawa nlikua na ratiba ya kwenda home pia that day. So nikaamua niende home kwanza.

Kufika home nikawa kama nishasahau kazi nliyokubali kufanya. Kuja shtuka saa kumi na moja. Ndo kuanza kufanya halahala kuwahi. Nafika makumbusho jioni sana, nikaanza kuhangaika kuwahi Shekilango. Kufika giza lishatua. Jumapili wale jamaa wanawahi kufunga. Nikaulizia namba nikapewa. Kumpigia kasema yeye kanisubiri mno na hawezi rudi. Kumpigia Raja naona sooo. Baadaye yule kijana wa hii ofisi ya Shekilango akanitext. [Kwa taarifa yako boss kamind kinoma, huo mzigo ulitakiwa ufike leo, uzembe wako unaeza sababisha wote tukose kazi].

Nikaona huu sasa msala. Nikampigia Raja, hakupokea. Text nikatuma hazikujibiwa. Nikampigia tena yule kijana kuuliza Raja anakaa wapi, akaniambia anakaa Sinza ya Mugabe, mtaa flani nikifika niulize tu Raja ntaelekezwa kwake. Kwa kuwa sio mbali nikachukua bodaboda. Hapo ni saa tatu kasoro. Nikiwa kwenye bodaboda si mvua ikaanza nyesha bana. Dereva wa boda akapaki ili nisiloe, nikamwambia kaka nawahi we twende tu. Kufika nikauliza kwenye duka flani maeneo nliyoelekezwa nikaoneshwa geti.

Nikagonga. Haikuchukua muda, geti likafunguliwa. Basi tukaangaliana pale. “Im sorry Raja….. plz usiwe hivyo”. “Come in” ndo jibu lake. Kumbuka nimeloana na mvua. Yy anasemaga nlitia huruma sana that day hahahah. Basi akanikaribisha kwake. Nikiwa sebuleni akaniletea vitenge viwili na taulo safi, kisha akanielekeza room ya wageni kisha nikaelekea bafuni kuoga. Nlivyomaliza nikarudi sebuleni nikamkuta amechemsha chai, akaniwekea tukawa tunakunywa. Kwa kuwa hakuwa ameitikia msamaha wangu ikabidi nirudie kumuomba. Hakujibu tena. Ikabidi nimsogelee, kimsingi nlijisikia vibaya mno kumuudhi Raja. Sasa ile kumsogelea si nikaanza kulia anisamehe, nikiwa nimechuchumaa karibu yake. Imani ikamuingia, akaniinua. Nikawa nafuta machozi. Ikabidi asimame anifute mwenyewe sasa. Kilichofuata ni kunihug. Then sijui aliyemuanza mwenzie bt tulijikuta tuko room tushamaliza.

Asbh ndo ananiambia. “Cessie I never wanted to do this. You are a very good friend of mine, so sikutaka nikutumie”. Nikacheka eti. “ndo tushafanya sasa friend”. “So sio utani, Cessie, kuna kitu hufahamu. I am married”.

Alivotamka hayo maneno mwisho, nilisogea mbali nae ghafla. Kuna maneno alikua anayasema ila sikuwa hata nayasikia kwa wakati huo. Sikujua hasira nlizozipata ilikua ni kwasababu ya yeye kutoniambia mapema kuwa kaoa au kwangu mwenyewe kwa kutembea na mume wa mtu au kuhisi kumpenda mtu ambaye sitaweza kuja mmiliki. Nilichofanya nikavaa nguo zangu fasta nikasepa.

Niliazimia kutowasiliana nae tena. So nimekaa semester nzima sitaki kumuona. Alifanya kila analoweza kaka wa watu. Alileta maua, alitumia watu, alikuja mwenyewe na kuvumilia matusi yangu mbele za watu, ila hakuchoka. Yani ingawa nlikuaga na boyfriend, ila maumivu nliyoyasikia yalisababisha nimpige chini hadi yeye. hakuna kitu kinatibu kama muda. Siku moja natoka home namkuta kanisubiri kituoni. “We need to talk”, sasa kule ni maeneo ya home. Siwezi kuanzisha varangati maana taarifa zitafika hadi kwa wazee. So nikawa mpole, nikaingia kwenye fortuner yake.

Cha ajabu hata hakutumia nguvu nyingi tena kuomba msamaha. Na hata hakusema ‘sorry’ maana ashalisema sana. Alitamka tu, “I miss you in my life”. basi nikamuangaliaaaaa. Nikajikuta moyo wangu unamuamini. Kimsingi I missed him too. Nikampa tu masharti tusirudie tena kufanya. Akakubali. Akaniambia mkewe anafanya kazi shirika moja la kimataifa nje ya nchi. Sikutaka hata kufahamu kiundani. So taratibu hali ikaanza kurudi kama zamani. Sema na yeye alibadilika. Sikumuona tena na videm. Ingawa nlifahamu lazma atakua navyo bt ananiheshimu sasa.

Kwani ilipita hata miezi miwili. Tukaanza tena kufanya. This time nikijua kabisa situation. Sometimes najilaumu sana. Bt Raja makes me happy. I don’t know how to let go of this happiness. I respect his wife. Bt ndo hivyo, I am deeply in love with this man.

“to answer your question, No. I don’t plan to go for masters”. Cessie akamalizia simulizi yake kwa kunijibu swali langu nlilomuuliza. Nlitambua jibu lake la mwisho ni kutokutaka maswali ya nyongeza kwenye majibu yake ya msingi. So tukaendelea kupiga stori kuhusu faida na hasara za kusoma sana kwenye jamii yetu. Ila kwenye akili yangu, nikimtazama Cessie kwa namna tofauti sana. She is a girl in love, and somehow confused. Ila confusion nipart ya maisha. Usipokua confused na mapenzi, utaconfusiwa kazini, au na wazazi, au na majirani, vyovyote vile, confusion is normal. So to sum it all up, Cessie is beautiful, in love and normal.

Mi na Cessie tukawa very close after that talk. Nikaanza na kumchangamikia tena Raja. So haikushangaza miezi kadhaa mbele Raja kunipa lift kurudi home. Kufika maeneo ya Ubungo darajani, foleni ikawa kubwa sana. Akashauri tupumzike pale MiCassa. Basi akaagiza msosi tukawa tunapata. Tumepiga stori sana. Nikawa namuona kwa namna Cessie anavyomuona. The guy is funny, kind and considerate. Tukiwa tunaangalia mwenendo wa foleni, akawa ameagiza wine. Basi tukaishare pale na stori nyingi.

Foleni ilipopungua kidogo, tukatoka. Saa nne tayari. Home maza alipopiga nlimwambia niko na anko Raja foleni kubwa bt atanifikisha home. Tukavuka mataa, katiza Mwenge hao tukanyoosha njia ya viwandani. Simu ya Raja ikaita. Ikabidi atafute mahali apaki. Akaongea na simu kwa muda kidogo. Alipomaliza akaomba radhi. Then akagundua sijafunga mkanda. Si akawa amesogea anauvuta mkanda anisaidie kuufunga. Videvu vikagusana.

Yani wanaokataa mambo ya masihara nawashangaa. Au maybe unconsciously I liked him. Ila kiukweli sikua hata na robo ya mawazo kuwa siku moja ntakua na kiss na Raja. Bt ndo hivyo. Akili iliniruka kwa muda. Kila kitu nlikua nakubali tu. Bahati mbaya kwangu na nzuri kwake nlikua nimevaa gauni, so kunitoa cha ndani ilikua sekunde tu. Nikastukia kiti kimelazwa, Raja anajiandaa. Akili imekuja stuliwa na mwanga mkali kwenye wind shield. Bahati nzuri kwangu alikua bado hajafanikiwa alichotaka. Sekunde chache mlango wa gari unagongwa kwa nguvu. “Polisi, fungua mlango”. Milango ilikua locked. La sivyo ningeaibika that day. Raja alikua fasta, akachukua nguo yangu ya ndani akaiweka mfukoni mwake, akafunga zip undo akafungua.

Hao polisi utadhani wameona madawa ya kulevya. Askari kama sita na difenda lao. Basi Raja akachezea vibao pale, tukakalishwa chini huku wakikagua gari. “yani mmeona barabara zetu ndo guest house”, muda wote huo mmoja akawa anatuchukua video.

“Twendeni kituoni”, basi tukaingia kwenye gari yetu na askari watatu. Kufika mitaa ya ITV pale wakasema tusimame. “mna sh ngapi, maana hii kesi kubwa”, Raja sjui alikua kapatwa na mshtuko gani. Hajibu hata vitu vya kueleweka. Nikaona hapa ntaadhirika. Nikaomba nimpigie mtu alete milioni chap. Wakasema aje na milioni mbili. Nikampigia Judy. Judy ni dada flani huwa anatoka na mzee wangu, ila ni muelewa sana. Kwanza nlipomwambia situation akakaa kimya dkk kama moja hivi. Then akaniuliza nilipo, akaomba aongee na hao askari, nikawapa simu. Wakanambia amesema wasubiri hapo, bt ikifika nusu saa hajaja itabidi watukabidhi kituoni.

Dkk 30, 40, 50 hadi saa. Mtu hajaja. Askari wakaona huyu anatuzingua wakawa wanataka sasa kutupeleka kituoni. Ndo Raja akili ikamrudia. “Twendeni benki niwatolee”. Ile tunaingia kwenye gari, tunashangaa difenda nyingine inapaki mbele yetu. Nliposhuka nakutana na wale askari waliotukamata wanapiga saluti tu kwa mmoja wa wale maafande. “Nini kinaendelea” aliuliza yule afande. “hamna kitu boss, tumewakamata hawa tunaelekea kituoni”. Yule afande akatuuliza vitambulisho vyetu, tukamuonesha. Then gari ya Judy nayo ikaingia. Nikaona wanasalimiana na yule afande. Then afande kaamrisha wale askari wawekwe chini ya ulinzi. Wakanyang’anywa simu zao zote, wakapakiwa kwenye difenda na pingu. Yule afande kamkabidhi simu zote Judy then akasema zake.

Akaniambia niingie kwenye gari yake. Akanipeleka hadi home. Njiani hata hatukuongea sana. Zaidi ya kumwambia tu asante, akajibu ya kawaida haya mdogo wangu. Tulivofika home, hata hakuingia ndani. Bt kabla sijashuka kwenye gari nikamgeukia, “Da Judy, naomba……..” “Usijali, no one will know”. “Hatujafanya chochote……” nikaona ni vema pia niweke hilo wazi asije dhani nimefanya. “Ann, hata ungekua umefanya, I don’t judge…. I know you naamini you can take a good care of yourself so usijisikie vibaya, na ulifanya jambo la maana kunipigia mimi.” “Thank you”. Nikawa nashuka, akaniita, akanikabidhi zile simu za wale askari. “nadhani zitakua safe Zaidi kwako” then akasepa.

Ndo hivo bana, Cessie ilibidi abadili dini. Now ni mke halali wa ndugu Rajab. i know she will be happy. ila kiukweli funzo moja nimelipata katika hii situation ni kuwa usizoeane wala kujenga urafiki na mume wa mtu. kuna muda akili zinavuka. unaona kama mimi ikabidi nimuachie nguo yangu ya ndani Raja, na sijui aliipeleka wapi hahahaha. au kama kwa rafiki yangu Cessie. kuja stuka keshazama mno hadi haezi toka. ikabidi aolewe mke wa pili jambo ambalo najua hakua amelipanga. Nasubiri watoke fungate aje tupige stori Zaidi. Kama kuna lolote interesting nitawajulisha. Mungu aniongoze hata siku yakitokea masihara tena, basi isiwe na mume wa mtu. Amen.

1616934004341.png
 

Algedo

Senior Member
Jul 24, 2020
103
250
I think kila kitu kinaitaji tu mda. Hata swala la mahusiano ni mda tu. Ingawa huwa tuna kurupuka most of tyme na ndio maan mahusiano mengi hayadumu na mpaka yadumu then needs more tyme to create frndship first
 

Mi-Ann

Member
Jun 9, 2020
81
150
Alifanya kila analoweza mkaka wa watu" hii kauli inaonyesha dhahiri huruma ndizo zinazotuponza wanawake tunaishia kukosa misimamo.Tutawalaumu sana wanaume but kiukweli tumekuwa mama huruma sana.
kwa kweli. alipotamka tu hayo maneno nikawaza exactly ulivyowaza. thanks
 

Mi-Ann

Member
Jun 9, 2020
81
150
Kumbe Judy hajaachana na baba yako mpaka leo?mama yako alishajua uhusiano wa Judy na baba yako?

Vipi ile biashara kati ya Judy na mama yako walifanikiwa kufungua?

Hata hivyo una kipaji cha kuandika na kusimulia.
thanks Harry. Judy na mzee bado sana. nadhani tungekua muslims wangeshaoana. Biashara aliyotaka mama, Da Judy aliona kabisa namna nlivyokua sijapenda. so alitafuta namna akajiweka pembeni mwenyewe bila kushurutishwa.
 

Mi-Ann

Member
Jun 9, 2020
81
150
I think kila kitu kinaitaji tu mda. Hata swala la mahusiano ni mda tu. Ingawa huwa tuna kurupuka most of tyme na ndio maan mahusiano mengi hayadumu na mpaka yadumu then needs more tyme to create frndship first
sure. "give it time".
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom