How to get a girl's attention via a mobile phone

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,453
20,736
Habari zenu wana MMU na poleni na sarakasi za utumbuaji majibu,mda mrefu sijaanzisha mada mtaa huu.

Mada yangu ya mwisho kwa mmu iliku ni mwezi march 2015. Hii hapa: www.jamiiforums.com/threads/kibongo-bongo-how-to-let-ladies-know-you-own-a-car.826790/

Mada ya leo inazungumzia ujanja ambao wakaka huutumia/wanaweza kuutumia kuteka hisia za mtoto wa kike haraka wanapozungumza katika simu.

Labda baadhi yenu mnaweza dhani nataka kuzungumzia zile text za mahaba au lugha laini ambazo wapenda nao hupagawishana kwenye simu,la hasha,hatuzungumzii hilo.

Nitazungumzia vitu vya kawaida sana ambavyo vinatokea katika mazingira yetu ya kitanzania au East AfriCa, hususani katika majiji makuu ya Dar, Mwanza, Arusha, Nairobi, Kampala nk.

Unaweza ukawa hukuwahi kuvifikiria lakini vinacheza part kubwa sana ktk mahusiano mapya yanayotarijia kuchipua.

TWENDE KWENYE MADA.
Upo katika mitikasi yako jijini dsm,ghafla unakutana na mdada mrembo sana, baada ya salam na maongezi ya hapa na pale, mnabadilishana namba za simu.

Baada ya siku moja au mbili mnaanza kuchat na kupigiana simu ili mfahamiane zaidi. Inafika wakati mtoto anaanza kukuuliza upo wapi and blablabla. Sasa hizi ndio aina ya activities na maeneo ambayo wakaka hutaja ili kujiongezea hadhi na hatimaye kuteka hisia za mtoto wa kike haraka.

1: Samahani dear,nipo barabarani na-drive.

Hakuna shaka kwamba watoto wa kike wengi huvutiwa na wakaka wanaomiliki magari. Mbinu hii hutumiwa na wakaka wengi mimi mwenyewe nikimwemo, haijalishi una drive gari la kwako, la kuazima, la kazini, bodaboda,bajaj au hau-drive kabisa. Pengine labda upo tu uswahilini kwenu umetulia.

Kitendo tu cha kumwambia upo barabarani una-drive, automatically atajua wewe unamiliki gari. Tayari hapo ushamteka.

2: Samahani dear nitakupgia baadae, namalizana na watu bandarini.

Hii nayo hutumiwa sana, yeye atadhani wewe ni mtu wa bandari na unahusika na issue kubwa kubwa za ku-clear makontena au magari bandarini, kumbe kapuku tu fulani. Hapa lazima utang'oa mzigo.

3: Samahani dear nitakupgia baadae,nipo kwenye mazungumzo na rafiki zangu hapa samaki samaki Mlimani City.

Kuna maeneo hapa dar ukiyataja kwenye simu, azima mtu wa upande wa pili unaye zungumza naye ashtuke. Kwa mtoto wa kike ambaye anapenda starehe, ukimwambia kwenye simu kwamba upo ktk maeneo hayo, atapagawa tu maana hakuna namna.

Samaki samaki Mlimani city ni eneo moja wapo lakini yapo maeneo mengi ya kula bata ambayo wakaka huyatumia kuwadanganyia watoto wa kike
kwenye simu kwa lengo kuteka hisia zao.

4: Samahani dear, nimepata safari ya ghafla naelekea Arusha.

Sote tunajua Arusha ni mji wa kitalii, lakini pia ni mji wa kula bata kama chenji unazo. Kuna mikoa hapa nchini, kuisafiri ni zaidi ya kwenda kikazi au kutembela ndugu na jamaa. Ni sehemu ya kufanya adventure.

Kwa wenzetu wa jinsia ya kike, ukishamwambia kwenye simu kwamba upo safarini kuelekea mikoa hiyo, wanakuwa so excited.

Wakaka hutumia sana mkoa wa Arusha na baadhi ya mikoa mengine nchini kuteka hisia za wadada.

5: Samahani dear nitakupgia baadae, nipo busy hapa TRA nashughulikia swala langu.

Naam, walipa kodi na wafanyabiashara mpo? Baadhi ya wadada wana imani kwamba wakaka wanaofanya kazi TRA au wale wanaoshinda/kufuatilia masuala yao ktk viunga vya jengo la TRA pale Samora avenue na lile jengo pale stesheni, wana pesa.

Hili niliwahi kulishuhudia kwa rafiki yangu wa karibu. Hakuwa mfanyakazi wa TRA na hakuwa na baishara yoyote ambayo ingeweza kumpeleka eneo lileM alitamka tu kwenye simu alipokuwa anazungumza na binti fulani aliyekutana naye siku kadhaa nyuma. Hatimaye akaja kula mzigo.

6:...Nipo Masaki, nikitoka nakucheki.

Ndio Masaki hutaki au? Kwa wakazi wa Dar; Masaki, Osterbay, Mikocheni na Mbezi beach ni baadhi tu ya maeneo ya kutaja na kujiongezea hadhi unapozungumza na mtoto wa kike kwenye simu ili kumteka kiakili. Tupo akina sie tunao ishi Mbagala, Kimara bonyokwa, Gongo la mboto, Manzese nk Tushataja sana maeneo hayo kwenye simu tunapo zungumza na wadada ilhali hatupo huko.

Kwa uchache huo ndio uchambuzi wangu kuhusu mada husika. Wewe kama mwana MMU unaweza ongezea pale nilipoishia.

MK254 tuweke kando upinzani kwetu wa jadi, najua pande za Nairobi mna maeneo yenu ya kutaja sambamba na aina ya shughuli mnazotumia kuteka hisia za wadada mnapozungumza nao kwenye simu. Nawe pia nakukaribisha.

Karibuni.
 
Kinyume chake, unanikumbusha Mlimbwende mmoja akitaka kwenda Viwanja vya starehe au misele yake alikuwa na kawaida ya kuja kuniazima Gari, ananiambia kuna wanaume wakimwona Demu amekuja peke ake sehemu za starehe na Gari, basi wanakuwa rahisi sana kuingia mkenge kwa kuwa wanajua demu Matawi.

Muwe makini jamani, kuna baadhi ya Wanawake hawafagilii Wanaume wenye mambo makubwa.

Na kingine ukumbuke njia ya mtu mwongo ni fupi, itafika siku ya siku uongo wako utastukiwa.

Ishi maisha yako achana na mambo ya kujikweza kwa ajili ya kuonekana babu kubwa kwa mwanamke
 
Haku mu-acknowledge mtunzi ambaye ni drake.
Nilimuelewa alipoweka " "

Vitu vidogo muhuni wangu wakati mwingine potezea.

Ujue Watu tunatofautiana kwenye kupokea suala, mtu mwingine anaweza kulipokea vibaya na kufikiria vingine, kumbe wewe ulikuwa na nia nyingine.

Sijui unanielewa ninachojaribu kukisema hapa Muhuni wangu?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Nilimuelewa alipoweka " "

Vitu vidogo muhuni wangu wakati mwingine potezea.

Ujue Watu tunatofautiana kwenye kupokea suala, mtu mwingine anaweza kulipokea vibaya na kufikiria vingine, kumbe wewe ulikuwa na nia nyingine.

Sijui unanielewa ninachojaribu kukisema hapa Muhuni wangu?
Nimekusoma kichaa wangu.haina noma baab.
 
nipo nakula mihogo hapa
Mihogo ya nazi na Samaki, hatari sana.

Na Seluni yangu hapa upepo murua wapita ati.

Au upate ile Mihogo ya kuchemsha ya kulainika, yajitokea unga, na Chai ya rangi ilowekwa Mchaichai.

Yaani ni raha ilioje
 
Back
Top Bottom