Kibatala: Wanaopinga Katiba Mpya wana Maslahi Binafsi

Hayo yote unayodhani yatawezeshwa na Katiba Mpya yanaweza kubaki ndoto za alinacha. Kwa sababu moja kuu: tatizo sio sheria mpya, nzuri au kali bali tatizo kubwa si kwa watawala wetu bali Watanzania kwa ujumla ni katika kuheshimu sheria. Hebu tupia jicho hapo mtaani unapoishi, ni watu wangapi wanakiuka "sheria za ndoa"? Sasa kama watu hawaheshimu sheria "binafsi," miujiza gani itafanya sheria za kwenye Katiba mpya ziheshimiwe?
Chahali:

Hili bandiko lako ni njia ya kutafuta suluhu na hao ccm wako waliokukimbiza nchini hivyo unataka kurejea nyumbani?

Hii mifano Yako mfu isiyoakisi sehemu kubwa ya mahitaji ya katiba mpya katika kuujenga uchumi imara siyo inatia kinyaa?

Hivi huko ulipo hakuna migogoro ya ndoa? Kama ipo haiamuliwi Kwa mujibu wa katiba Yao? Hebu kuwa serious kidogo basi unapojadili hoja zenye maslahi mapana Kwa ndugu zako uliowaacha kule kijijini!

\Nilidhani ungesaidia kuidai hiyo katiba mpya ili ikupe unafuu wa kuhoji bila kubughudhiwa na Kwa kuwa una exposure kubwa juu ya unaoishi nao juu ya katiba yao Kama Kuna mazuri ya kuiga kutoka kwao kumbe nawe ni walewale CCM mataga daissipora! Rudi TU hautafanywa lolote!
 
Kiswahili kimekuwa kigumu kiasi hiki?

Maslahi ya watu kwa sababu ya njaa za matumbo yao na familia zao. Vipi hayo yanaweza linganishwa na maslahi haya:

Mwananchi wa kawaida anayejielewa, anayekataa kuendelea kubambikiziwa kesi, kuendelea kudhulumiwa, kuendelea kubebeshwa mizigo ya kodi za wengine nk.

Au hata yule anayetaka mihimili ya utawala iliyo na uhuru kamili, anayetaka usawa, anayetaka uwajibikaji, anayetaka mawazo yake kusikilizwa nk.

Seriously, haikuingii akilini kuwa kwanini hapo pana tofauti?

Au ni ile mambo ya kujitia hamnazo?
Mkuu, umetumia muda wako kumpa jibu zuri kabisa, lakni kwa mtu kama huyo ni sawa na kazi bure uliyofanya. Kwa sababu hana uwezo wa kuelewa, na kama anao, maslahi anayoyapigania hayamruhusu kukiri ukweli huo.
 
Wanufaika wa moja kwa moja wa hali iliyopo wanafahamika kwa maandiko yao. Uzi huu uliwahusu wao:

Hayo yote unayodhani yatawezeshwa na Katiba Mpya yanaweza kubaki ndoto za alinacha. Kwa sababu moja kuu: tatizo sio sheria mpya, nzuri au kali bali tatizo kubwa si kwa watawala wetu bali Watanzania kwa ujumla ni katika kuheshimu sheria. Hebu tupia jicho hapo mtaani unapoishi, ni watu wangapi wanakiuka "sheria za ndoa"? Sasa kama watu hawaheshimu sheria "binafsi," miujiza gani itafanya sheria za kwenye Katiba mpya ziheshimiwe?
Mahakama ikiwa huru lazima Rais atafuata sheria
 
Ukiwa mjinga unaweza kusema hivyo. Lakini kama una akili japo kidogo, huwezi kusema hivyo, maana utakuwa ulisikia wananchi walisema nini kuhusiana na katiba yetu ya sasa na hitajio la katiba mpya, kupitia report ya Tume ya katiba ya Jaji Warioba.
Una akili nyingiiiiii mno🤣
 
Hayo yote unayodhani yatawezeshwa na Katiba Mpya yanaweza kubaki ndoto za alinacha. Kwa sababu moja kuu: tatizo sio sheria mpya, nzuri au kali bali tatizo kubwa si kwa watawala wetu bali Watanzania kwa ujumla ni katika kuheshimu sheria. Hebu tupia jicho hapo mtaani unapoishi, ni watu wangapi wanakiuka "sheria za ndoa"? Sasa kama watu hawaheshimu sheria "binafsi," miujiza gani itafanya sheria za kwenye Katiba mpya ziheshimiwe?

Kuwa na total separation of powers ni muhimu kwa utawala wa sheria kutamalaki.

1. SA leo Zuma yuko korokoroni kwa kuidharau mahakama.
2. Kenyatta kaufyata mahakamani na BBI yake iwe ya nia njema au fyongo.

Bado hudhani kuwa tutakapokuwa na total separation of powers tutakuwa tumejikomboa na:

1. Kumbambikizia kesi tukaozea jela bila mtu kuwajibika?
2. Tukidhulumiwa tutakuwa na mahali pa kukimbilia tukiwa na imani ya haki kutendeka?
3. Uwajibikaji utakuwa bora zaidi kuliko sasa?
4. Tutapiga hatua zaidi kuwa sawa mbele za haki?
5. Hatutasikitika kwa kuwa tume huru.
6. Nk

Nikuulize nawe sasa. Unasimama na upande upi kwenye kadhia hii?

Pana ambao wamejinasibu kuwa wao ni hao wenye kunyoa viduku hapo chini:

IMG_20210704_051559_619.jpg

Hao wenye viduku, yaliyomo kwenye red yanawahusu:

IMG_20210705_090501_586.jpg

"..... hata kama la kijinga." --- ninakazia.
 
Huyu ni miongoni mwa mawakili wachache sana walio goma hata kumsujudia jiwe enzi zake.

Ni miongoni mwa wasomi wachache wanaosimami wanachokiamini.

Bravo! Kibatala.
Alipomkwepa jiwe ni pale alipoamua kusimamia taaluma yake,na si kuijiingiza kwenye harakati kunuka kama za wengine.

Na ndicho kitu jiwe alikuwa anakiheshimu sana.

Ukisimamia taaluma yako unakuwa salama sana.
 
Ukiwa mjinga unaweza kusema hivyo. Lakini kama una akili japo kidogo, huwezi kusema hivyo, maana utakuwa ulisikia wananchi walisema nini kuhusiana na katiba yetu ya sasa na hitajio la katiba mpya, kupitia report ya Tume ya katiba ya Jaji Warioba.
Nchi huru hii kwa watu kutoa maoni.

Ujinga ni kujifunga na nira moja kama hitaji la wote.kwanini na wanaokataa wasiheshimiwe ila waitwe wajinga!

Hapa ndipo nguvu hutenganisha makundi haya mawili ya itikadi,wanaoamini wana akili hawawezi kujenga hoja zaidi ya kutukana na kudhalilisha,wanaodhalilishwa nao wanaona wacha maisha yaendelee wakila bata maana wako kwenye mneso.
 
Hayo yote unayodhani yatawezeshwa na Katiba Mpya yanaweza kubaki ndoto za alinacha. Kwa sababu moja kuu: tatizo sio sheria mpya, nzuri au kali bali tatizo kubwa si kwa watawala wetu bali Watanzania kwa ujumla ni katika kuheshimu sheria. Hebu tupia jicho hapo mtaani unapoishi, ni watu wangapi wanakiuka "sheria za ndoa"? Sasa kama watu hawaheshimu sheria "binafsi," miujiza gani itafanya sheria za kwenye Katiba mpya ziheshimiwe?
Mtanzania ndiye mtu pekee anayejua kudai haki na hapendi kutimiza wajibu.
 
sisi kama wananchi tunasema kwa sasa mambo ya katiba mpya hatutaki, labda hadi mwaka 2040.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wasio hitaji katiba mpya ni kwamba:

1. Hawajui kuna kubambikiziana makesi popote
2. Hawajui kutokea kwenye kubambikiziwa kesi wanaweza kushikiliwa kwa muda wowote, wakaja achiliwa bila mtu kuwajibika
3. Hawahitaji kuwa sawa na wengine mbele za sheria
4. Hawana taabu na utitiri wa viongozi wasio na ridhaa nao wala hawalali hata kama viongozi hao hawalipi kodi
5. Kwao mihimili ya utawala kuwa huru haina maana
6. Nk nk.

Kwa hakika watu hao hawajitambui au ni wanufaika wa moja kwa moja wa katiba iliyopo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Wanaolilia katiba mpya ndo wenye maslahi binafsi... wanadai katiba mpya ni takwa la wananchi ila kila cku utamsikia mbowe au vijana kadhaa wa bavicha, haohao kila cku!

yaani katika nchi yenye watu 60M+ kikundi cha watu laki moja wakipiga kelele ndo iwe wananchi wote?

tulio wengi wala hatuna mpango na hayo makatiba, sababu hayatusaidii sisi binafsi zaidi ya kuwanufaisha waliliaji

labda mtupe na mfano wa nchi yenye katiba nzuri ili tuangalie wao inawanufaisha vip watu wa vipato vya chin na wasio na status yeyote ktk jamii kama uongozi, nk
 
Wasio hitaji katiba mpya ni kwamba:

1. Hawajui kuna kubambikiziana makesi popote
2. Hawajui kutokea kwenye kubambikiziwa kesi wanaweza kushikiliwa kwa muda wowote, wakaja achiliwa bila mtu kuwajibika
3. Hawahitaji kuwa sawa na wengine mbele za sheria
4. Hawana taabu na utitiri wa viongozi wasio na ridhaa nao wala hawalali hata kama viongozi hao hawalipi kodi
5. Kwao mihimili ya utawala kuwa huru haina maana
6. Nk nk.

Kwa hakika watu hao hawajitambui au ni wanufaika wa moja kwa moja wa katiba iliyopo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
kwahiyo unadhani hiyo katiba mpya itayaondoa haya unayoyaota? tupe mfano wa nchi ambayo ina katiba nzuri ambayo haya mambo unayoyataja hayapo
 
kwahiyo unadhani hiyo katiba mpya itayaondoa haya unayoyaota? tupe mfano wa nchi ambayo ina katiba nzuri ambayo haya mambo unayoyataja hayapo

1. SA Zuma leo ni mtu wa korokoroni kwa kuidharau mahakama. Kwa katiba sahihi Zuma kutokuitika tu wito wa mahakama ni mhalifu kwa kuidharau mahakama sawa kama alivyo mu SA mwingine.

2. Kenyatta Kenya urais wake umepata kutenguliwa na mahakama akiwa ofisini kwa masharti na vigezo muhimu kutokuwa vimezingatiwa kwenye uchaguzi wao mkuu.

3. Kenya leo, Kenyatta na mwenziwe Odinga na BBI yao wameufyata, mahakama inapotamalaki katika maeneo yake.

Haiyumkiniki wewe ni huyo dogo aliye tupia kiduku hapa chini:

IMG_20210704_051559_619.jpg

Uyaone vipi wewe haya?

IMG_20210705_224945_255.jpg

Ukizingatia bila shaka hata hapa chini kwenye red napo pana kuhusu?

IMG_20210705_090501_586.jpg

"..... Kwa lolote hata kama ni la kijinga."

Hiiiiii bagosha!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom