Wakili msomi bwana Peter Kibatala leo katika 360 ya clouds TV amefunguka kisomi kuhusiana na katiba mpya.
"Katiba mpya ni hitajio la watanzania wengi. Wanaopinga, ni kwa sababu tu ya maslahi binafsi yatokanayo na katiba iliyopo." -- amesisitiza wakili huyo.
Zaidi sana anasema Kibatala:
1. Si kweli kuwa katiba mpya inatakiwa na wanasiasa tu.
2. Wanaopinga kuendelezwa kwa mchakato wa katiba mpya ni wale tu wa kunufaika kibinafsi na hii iliyopo.
3. Umuhimu wa kuzifanyia marekebisho ya kisheria tume za chaguzi ya Taifa na ile ya Zanzibar zitahusika kwenye kuivusha katiba hiyo mpya.
4. Kumalizia kiporo cha mchakato uliobakia kitampa Mama Legacy ya pekee na ya kudumu.
5. Vuguvugu la kudai katiba lililoanza Halizuiliki tena.
6. Kama ilivyo kwa mbegu, walioko madarakani inabidi waoze ili yapatikane mazao mengi
7.Kikwazo ni walioko madarakani kwani wana vingi vya kupoteza kwa ujio wa katiba mpya.
Hoja hupingwa kwa hoja. Barikiwa sana wakili msomi.