Kibatala: Wanaopinga Katiba Mpya wana Maslahi Binafsi

Chini pana clips 3 za mazungumzo yote ya wakili msomi Peter Kibatala kuhusu katiba mpya aliyofanya leo katika Power breakfast ya Clouds TV:

Anasema wakili huyu

1. Si kweli kuwa katiba mpya inatakiwa na wanasiasa tu.
2. Wanaopinga kuendelezwa kwa mchakato wa katiba mpya ni wale tu wa kunufaika kibinafsi na hii iliyopo.
3. Umuhimu wa kuzifanyia marekebisho ya kisheria tume za chaguzi ya Taifa na ile ya Zanzibar zitahusika kwenye kuipitisha katiba mpya
4. Kumalizia kiporo cha mchakato uliobakia kitampa Mama Legacy ya pekee na ya kudumu
5. Vuguvugu la kudai katiba lililoanza Halizuiliki tena
6. Kama ilivyo kwa mbegu walioko madarakani inabidi waoze ili yapatikane mazao mengi
7.Kikwazo ni walioko madarakani kwani wana vingi vya kupoteza kwa ujio wa katiba mpya.

-------
My take:

Tume za uchaguzi Taifa na Zanzibar kama asemavyo wakili msomi ni eneo muhimu la kukodolewa macho.

Barikiwa sana mtumishi. Endelea kututoa tongotongo machoni. Pamoja tutafika.
 
Chini pana clips 3 za mazungumzo yote ya wakili msomi Peter Kibatala kuhusu katiba mpya aliyoyafanya leo na Power breakfast ya Clouds TV:

Anasema wakili huyu:

1. Si kweli kuwa katiba mpya inatakiwa na wanasiasa tu.
2. Wanaopinga kuendelezwa kwa mchakato wa katiba mpya ni wale tu wa kunufaika kibinafsi na hii iliyopo.
3. Umuhimu wa kuzifanyia marekebisho ya kisheria tume za chaguzi ya Taifa na ile ya Zanzibar zitahusika kwenye kuipitisha katiba mpya
4. Kumalizia kiporo cha mchakato uliobakia kitampa Mama Legacy ya pekee na ya kudumu
5. Vuguvugu la kudai katiba lililoanza Halizuiliki tena
6. Kama ilivyo kwa mbegu walioko madarakani inabidi waoze ili yapatikane mazao mengi
7.Kikwazo ni walioko madarakani kwani wana vingi vya kupoteza kwa ujio wa katiba mpya.

-------
My take:

Tume za uchaguzi Taifa na Zanzibar kama asemavyo wakili msomi ni eneo muhimu la kukodolewa macho.

Barikiwa sana mtumishi. Endelea kututoa tongotongo machoni. Pamoja tutafika.
 
Kiswahili kimekuwa kigumu kiasi hiki?

Maslahi ya watu kwa sababu ya njaa za matumbo yao na familia zao. Vipi hayo yanaweza linganishwa na maslahi haya:

Mwananchi wa kawaida anayejielewa, anayekataa kuendelea kubambikiziwa kesi, kuendelea kudhulumiwa, kuendelea kubebeshwa mizigo ya kodi za wengine nk.

Au hata yule anayetaka mihimili ya utawala iliyo na uhuru kamili, anayetaka usawa, anayetaka uwajibikaji, anayetaka mawazo yake kusikilizwa nk.

Seriously, haikuingii akilini kuwa kwanini hapo pana tofauti?

Au ni ile mambo ya kujitia hamnazo?
Hayo yote unayodhani yatawezeshwa na Katiba Mpya yanaweza kubaki ndoto za alinacha. Kwa sababu moja kuu: tatizo sio sheria mpya, nzuri au kali bali tatizo kubwa si kwa watawala wetu bali Watanzania kwa ujumla ni katika kuheshimu sheria. Hebu tupia jicho hapo mtaani unapoishi, ni watu wangapi wanakiuka "sheria za ndoa"? Sasa kama watu hawaheshimu sheria "binafsi," miujiza gani itafanya sheria za kwenye Katiba mpya ziheshimiwe?
 
Upuuzi huu. Futa
 
Anachoongea Peter Kibatala leo na wanachoongea Chadema ni vitu viwili tofauti, Kibatala anaongelea kumalizia mchakato wa Katiba pendekezwa lakini Chadema hawaongelei kumalizia mchakato. Kwa wajibu wa Mheshimiwa Mbowe "tunamtaka Rais aunde tume ya Katiba..." tume ambayo kisheria ilishamaliza muda wake, kilichosalia ni huo mchakato wa kutangazwa gazeti ni na Tume ya Uchaguzi kusimamia mchakato wa kura ya maoni. Maana yake Katiba Mpya ipo katika mhutasari wa KATIBA PENDEKEZWA Kilichosalia ni mchakato wa kuipitisha au kuikataa.

Inawezekana ni kuteteleza ndimi tu mkuu.

Chadema wanataka kurejelewa kwa mchakato wa katiba uliolala tokea mwishoni mwa awamu ya 4.

Kibatala anachosema na Chadema ni kile kile. Kumbuka Kibatala ni wakili wa Chadema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom