Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu; Is it a prosecution or persecution?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
751
Reaction score
1,258
Baada ya kuisikiliza submission ya Mh. Tundu Lisu leo June 16, 2025, kwenye kesi yake ya uhaini nimeikumbuka barua maarufu kama "Letter from Birmingham Jail" ya 1963 Dr. Martin Luther King Jr.'s iliyosema "Injustice anywhere is a threat to justice everywhere,"

Ukiachilia mbali maelekezo ya sheria ya magereza na kanuni zake aliyoyaeleza Mh. Tundu Lisu katika submission yake, hata ibara ya 13(6)(b) ya Katiba ya Tanzania inasema "Ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo"

Nadhani kulikuwa na ukweli fulani kwenye maneno ya Mh Luhaga Mpina kuwa kama demokrasia ya vyama vingi imetushinda ni bora tukaachana nayo tu. Hatuwezi kuwa na wanasiasa ambao, akinusurika jaribio la mauaji lililomwachia ulemavu, tunawaweka kwenye death row, hata kabla hawajahukumiwa!

Mambo kama haya kwa mtu yeyote yule, acting outside ideological fanatism, hawezi kuyaunga mkono. Ninaamini tunaouwezo wa wakujenga nchi moja yenye umoja bila kujali tofauti zetu za kiitikadi. Tanzania ni yetu sote
 
Tujiepushe na kutaja watu mahali ambapo hatuna ushahidi. Kwa jinsi UCHAWA ulivyokithiri, upo uwezekano mkubwa wanaoyatenda haya wakawa hawana baraka za Rais. Ushauri wangu, tuyakemee maovu kwa sura yake. CCM ina watu wema kadhalika na wabaya wachache hawawezi kukosa. Chama chenye wanachama milioni 13 si rahisi kutokuwepo wachache waliokengeuka. Hao tukiwajua na kama kuna ushahidi tunaweza kuwataja. Vinginevyo sio busara kufanya mobb justice. Tunawakosea wana CCM wema.
 
Mpango wa Allah kumpeleka LISU UKONGA ni kuona mazingila ya jela yalivyo na kuona Sheria zinavyopindishwa ktk mageleza za hapa Tanzania.Allah hakukosea jambo hilo.ni wangapi wapo UKONGA wamenyimwa kufanya Ibada kama anavyosema LISU? Kuna namna Allah amelipitisha hili ili watu tufaham manyanyaso yaliyopo huko
 
Allah gani? Wabongo tupunguze upimbi, Mungu hawezi saidia wajinga wasio jisaidia, Lisu anapigania wajinga type yako.
 
Tujiepushe na kutaja watu mahali ambapo hatuna ushahidi. Kwa jinsi UCHAWA ulivyokithiri, upo uwezekano mkubwa wanaoyatenda haya wakawa hawana baraka za Rais. Ushauri wangu, tuyakemee maovu kwa sura yake. CCM ina watu wema kadhalika na wabaya wachache hawawezi kukosa. Chama chenye wanachama milioni 13 si rahisi kutokuwepo wachache waliokengeuka. Hao tukiwajua na kama kuna ushahidi tunaweza kuwataja. Vinginevyo sio busara kufanya mobb justice. Tunawakosea wana CCM wema.
Ni vigumu sana kwa mwana ccm kuwa mwema, mkweli na muungwana.
Ukiwa mwana ccm automatically unakuwa mwovu, mwongo na mla rushwa.
 
Mpango wa Allah kumpeleka LISU UKONGA ni kuona mazingila ya jela yalivyo na kuona Sheria zinavyopindishwa ktk mageleza za hapa Tanzania.Allah hakukosea jambo hilo.ni wangapi wapo UKONGA wamenyimwa kufanya Ibada kama anavyosema LISU? Kuna namna Allah amelipitisha hili ili watu tufaham manyanyaso yaliyopo huko
Uko sahihi kabisa, kisukuma tunasema ni blessings in disguise.
 
Tujiepushe na kutaja watu mahali ambapo hatuna ushahidi. Kwa jinsi UCHAWA ulivyokithiri, upo uwezekano mkubwa wanaoyatenda haya wakawa hawana baraka za Rais. Ushauri wangu, tuyakemee maovu kwa sura yake. CCM ina watu wema kadhalika na wabaya wachache hawawezi kukosa. Chama chenye wanachama milioni 13 si rahisi kutokuwepo wachache waliokengeuka. Hao tukiwajua na kama kuna ushahidi tunaweza kuwataja. Vinginevyo sio busara kufanya mobb justice. Tunawakosea wana CCM wema.
Mie naamini kule wema wachache mnoo na wabaya ndio wengi..
Kinachowapomza waonekane ni wabaya ni ile ratio.
Kinachowpaonza waha kuonekana ni wabishi ni ile ratio yao, wabishi ni wengi mnoo, haimaanishi hakuna wale wasiokuwa wabishi
Warangi usioe sijui malaya, ni ratio inawaponza, lakini haimaanishi hakuna watulivu.
Wavita bangi kuonekana ni wahuni, kinachoponza ni ratio, mihuni mimgi kuliko wastaarabu.
Wahaya halikadhalika
 
Baada ya kuisikiliza submission ya Mh. Tundu Lisu leo June 16, 2025, kwenye kesi yake ya uhaini nimeikumbuka barua maarufu kama "Letter from Birmingham Jail" ya 1963 Dr. Martin Luther King Jr.'s iliyosema "Injustice anywhere is a threat to justice everywhere,"

Ukiachilia mbali maelekezo ya sheria ya magereza na kanuni zake aliyoyaeleza Mh. Tundu Lisu katika submission yake, hata ibara ya 13(6)(b) ya Katiba ya Tanzania inasema "Ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo"

Nadhani kulikuwa na ukweli fulani kwenye maneno ya Mh Luhaga Mpina kuwa kama demokrasia ya vyama vingi imetushinda ni bora tukaachana nayo tu. Hatuwezi kuwa na wanasiasa ambao, akinusurika jaribio la mauaji lililomwachia ulemavu, tunawaweka kwenye death row, hata kabla hawajahukumiwa!

Mambo kama haya kwa mtu yeyote yule, acting outside ideological fanatism, hawezi kuyaunga mkono. Ninaamini tunaouwezo wa wakujenga nchi moja yenye umoja bila kujali tofauti zetu za kiitikadi. Tanzania ni yetu sote
View attachment 3371754
Lissu ameletwa na Mungu kwa lengo la kuiumbua serikali ya Tanzania
 
Ni vigumu sana kwa mwana ccm kuwa mwema, mkweli na muungwana.
Ukiwa mwana ccm automatically unakuwa mwovu, mwongo na mla rushwa.
Comrade hata Mwenyezi Mungu hatoi hukumu za jumla jumla. Lets call a spade a spade, mwovu aitwe mwovu kwa jina lake, mwongo aitwe mwongo kwa jina lake na mla rushwa aitwe mla rushwa kwa jina lake. CCM kama chama hakina mdomo wa kusemea uwongo, nafsi iliyohifadhi uovu wala mikono ya kupokelea rushwa. Wanaofanya haya ni watanzania wenzetu, pengine wenye dini kama zetu, lakini wanaweza kuwa wanajifichia kwenye koti la kijani kwasababu wanazozijua wao.
 
Tujiepushe na kutaja watu mahali ambapo hatuna ushahidi. Kwa jinsi UCHAWA ulivyokithiri, upo uwezekano mkubwa wanaoyatenda haya wakawa hawana baraka za Rais. Ushauri wangu, tuyakemee maovu kwa sura yake. CCM ina watu wema kadhalika na wabaya wachache hawawezi kukosa. Chama chenye wanachama milioni 13 si rahisi kutokuwepo wachache waliokengeuka. Hao tukiwajua na kama kuna ushahidi tunaweza kuwataja. Vinginevyo sio busara kufanya mobb justice. Tunawakosea wana CCM wema.
Ccm haina wanachama 13m, labda ukawadanganye waliolala. Hakuna chama chenye wanachama 5m+ nchi hii. Sema ccm wameuza na kugawa kadi 13m, na sio wanachama 13m.
 
Comrade hata Mwenyezi Mungu hatoi hukumu za jumla jumla. Lets call a spade a spade, mwovu aitwe mwovu kwa jina lake, mwongo aitwe mwongo kwa jina lake na mla rushwa aitwe mla rushwa kwa jina lake. CCM kama chama hakina mdomo wa kusemea uwongo, nafsi iliyohifadhi uovu wala mikono ya kupokelea rushwa. Wanaofanya haya ni watanzania wenzetu, pengine wenye dini kama zetu, lakini wanaweza kuwa wanajifichia kwenye koti la kijani kwasababu wanazozijua wao.
Ukitaka kujua ccm ni chama cha waovu, juzi Gwajima kaamua kuvunja utamaduni wa ccm kulinda uovu. Wanaccm wamemjia juu, hadi leo hafahamiki yuko wapi.
 
Ebu fikiria Prof. Juma alikuwa mwl pale UDSM baadae akapata bahati ya kuyasimamia yale aliyofundisha pamoja na aliowafundisha then anaona sheria inavyopindishwa huku anakenua meno tu pamoja na Ndugu yake Tulia.

Kule Kenya Jaji Msataafu Maraga anapeleka kesi mahakamani kushitaki maofisa wa polisi kwa kukeuka viapo vyao na kuhusika kwenye mauaji ya Ojwang'.

Wakati tupo shule na prof. Ole pale FOE UDSM alionekana kama mtu smart ila kwasasa ni msajili wa mahakama ila upuuzi mwingi sana inafanyika mbeye yake amebakia kupiga mdomo tu.

Kwa miaka mitano mingine ijayo ya Rais Samia naona dalili mbaya sana kwa nchi yetu.

Usalama umeingusha sana nchi hii
..muangamie popote pale mlipo.
Mpo hopeless kuliko mtumishi yeyote wa UMMA hapa Tanzania.
 
Mbona mm ni mwana CCM na nimechapisha humu Jamii Forum maoni yangu sio tu ya kupinga yale anayoyapinga Gwajima lakini pia kumuunga mkono kwenye hoja yake. Sio kila mwana CCM ni CHAWA, tupo wengi tunaoamini katika itikadi ya CCM ya KIJAMAA na HISTORIA yake.
 
Ebu fikiria Prof. Juma alikuwa mwl pale UDSM baadae akapata bahati ya kuyasimamia yale aliyofundisha pamoja na aliowafundisha then anaona sheria inavyopindishwa huku anakenua meno tu pamoja na Ndugu yake Tulia.

Kule Kenya Jaji Msataafu Maraga anapeleka kesi mahakamani kushitaki maofisa wa polisi kwa kukeuka viapo vyao na kuhusika kwenye mauaji ya Ojwang'.

Wakati tupo shule na prof. Ole pale FOE UDSM alionekana kama mtu smart ila kwasasa ni msajili wa mahakama ila upuuzi mwingi sana inafanyika mbeye yake amebakia kupiga mdomo tu.

Kwa miaka mitano mingine ijayo ya Rais Samia naona dalili mbaya sana kwa nchi yetu.

Usalama umeingusha sana nchi hii
..muangamie popote pale mlipo.
Mpo hopeless kuliko mtumishi yeyote wa UMMA hapa Tanzania.
Tatizo kubwa la nchi yetu kwa sasa ni UCHAWA, kila mahali pamejaa CHAWA, huyu anajiita CHAWA wa huyu, mwingine wa yule, ilimradi tafrani. Bad enough tumeseti precedence kuwa ukitaka CHEO kuwa CHAWA, sasa wengi amegeuka CHAWA kutafuta vyeo. Haya ndio matokeo yake.
 
Ccm haina wanachama 13m, labda ukawadanganye waliolala. Hakuna chama chenye wanachama 5m+ nchi hii. Sema ccm wameuza na kugawa kadi 13m, na sio wanachama 13m.
Nakazia ✍️
Kuna watu wanamiliki kadi za ccm kimkakati tu kuwarahisishia kupata fursa fulani kama ajira, tenda za biashara, vibali, mikopo, nk, lakini siyo maccm kabisaa
 
Mbona mm ni mwana CCM na nimechapisha humu Jamii Forum maoni yangu sio tu ya kupinga pia yale anayoyapinga Gwajima lakini pia kumuunga mkono kwenye hoja yake. Sio kila mwana CCM ni CHAWA, tupo wengi tunaoamini katika itikadi ya CCM ya KIJAMAA na HISTORIA yake.
Nani anakujua ww na hii fake id?
 
Nakazia ✍️
Kuna watu wanamiliki kadi za ccm kimkakati tu kuwarahisishia kupata fursa fulani kama ajira, tenda za biashara, mikopo, nk, lakini siyo maccm kabisaa
Kwa maoni yako, hawa tunaowaona wamefurika kwenye mikutano ya CCM wakiwa wamitinga kijani na njano ni akina nani sasa?
 
Hii sio ID fake, mm sio mhalifu, kwanini nifiche ID yangu? Unaweza search jina langu katika orodha ya madaktari kwenye link ya msajili wa madaktari Tanganyika (MCT) utalikuta hivi hivi na sura ipo pale.
Pitia maoni ya mwanaccm mwenzako hapa..

Back
Top Bottom