Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu; Is it a prosecution or persecution?

Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu; Is it a prosecution or persecution?

Kwanza kuwa na maoni ni haki ya kiraia, haitokani na uanachama wa chama cha siasa. Ninao uhuru wa kuwa na maoni kwa CCM, CHADEMA, CHAUMA, ACT nk bila kuwa mwanachama wa vyama husika. Hakuna sheria inayopiga marufuku mtanzania kutoa maoni yake hapa jamii forum. Ningetaka kuyapeleka kwenye chama ningefanya hivyo, ila nimeyaleta hapa kwasababu nimeamua kuyaleta hapa full stop! By the way, umeyaelewa maudhui ya chapisho langu? Audience aliyekusudiwa ni nani? Kwa huo mtazamo wako, hakuna mtu angeanzisha mijadala hapa jamii forumu, wote tungetakiwa tukajadiliane kwenye vyama vyetu. I think unahitaji kukua kidogo, hoja zako ni nyepesi sana.
Nilitegemea utapanick. Uwe na mchana mwema boss.
 
Tundu Lisu akinyongwa ww utapata faida gani? Mawazo kama haya nilikuwa nayo nikiwa chipukizi. Sasa nimekuwa, naomba Mwenyezi Mungu anirehemu. Hivi vyama vyetu kuna siku vitakuwa vimekufa, ila utanzania wetu utakuwepo. Hatuna sababu ya kuutumia vyombo vya dola kukiuka haki za watu.
hapana hawezi kunyongwa ni part ya siasa tu, unatakiwa uwe umekomaa kwenye siasa kuelewa mambo yanayoendelea
 
Dr, labda Kwa kama utaruhudu matazamo kinzani ambao ni halisi vile vile.

Kwangu Mimi Rais hawezi kukwepa kutajwa hata Kwa Jina lake Samia Suluhu Hasaani pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na idara zake, Uhamiaji, Magereza na Polisi.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba yanayotokea yapo under their control na hayafanyiki Kwa Siri yapo Kwa uwazi na bayana kabisa.

Wakuu Hawa, mteule wao ni Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa hiso organs. Kama mambo yanafanyika na hawezi kuyakemea na isipokua anawakemea wanaoyakataa na wakati huo huo hamuwajibishi hata mmoja kati ya hao isipokua ni kuongeza uteuzi na mamlaka, ni vyema akatajwa yeye Moja kwa Moja.

Nachoweza kukwambia kwamba hii ni party coccus ya CCM Kwa sasa. Kuhakikisha kwamba vyombo vyote vya usalama vinafanya kazi Kwa maslahi ya chama kwanza kabla ya wananchi. Kwa sababu kutenda Haki kutasababisha chama kupoteza udhibiti na sio ushawishi na kukubalika Kwa sababu hayo yameshapotea.

Kama kwa mujibu wa katiba yetu serikali Ina wajibu wa kuhakikisha ustawi wa wananchi, na hapo serikali haitaku kuambiwa kwamba Kuna watu wanatekwa na kuuwawa na kwamba kunahitajika mifumo ya Haki na usawa badala yake inatengeneza makosa kama ya Lissu ya uhaini ni dhahiri mkuu na a hiyo serikali amebariki!
Linapokuja swala la uwajibikaji, maadam ulinzi wa raia ni sehemu ya majukumu yake, la kheri au la shali, atakuwa anawajibu nalo. Swali linabaki ni kwa vipi? Je, ni kwa yeye kutenda jambo ambalo hatuna ushahidi nalo? Au ni kwa kuwajibika kwa makosa ya wasaidizi wake kushindwa kuzuia matukia haya?
 
Sahihi upo hapo kwa mjadala basi pendekeza namna ya accountability ambayo ni relevant! Ila mpaka sasa hakuna accountability isipokua ni counter-accoutability inayosimaniwa na yeye mwenyewe na Kwa maneno yake Mwenyewe. Rejea kauli yake dhidi ya Gwajima katika Mkutano mkuu wa Ccm Dodoma.
 
Sahihi upo hapo kwa mjadala basi pendekeza namna ya accountability ambayo ni relevant! Ila mpaka sasa hakuna accountability isipokua ni counter-accoutability inayosimaniwa na yeye mwenyewe na Kwa maneno yake Mwenyewe. Rejea kauli yake dhidi ya Gwajima katika Mkutano mkuu wa Ccm Dodoma
Mbwa huzaliwa na u-mbwa wake. Hajifunzi kuwa mbwa. CCM njema ilikufa zamani ( kama hawaachiani glass ya maji mezani) huo wema upo wapi? CCM ilyopo ina mbegu ya uovu ndani yake hivyo kuuzaa uovu ni kawaida na ndio maana wajao kwa uwazi kukemea maovu (wana CCM) hupingwa na CCM yenyewe!
 
Mbona mm ni mwana CCM na nimechapisha humu Jamii Forum maoni yangu sio tu ya kupinga pia yale anayoyapinga Gwajima lakini pia kumuunga mkono kwenye hoja yake. Sio kila mwana CCM ni CHAWA, tupo wengi tunaoamini katika itikadi ya CCM ya KIJAMAA na HISTORIA yake.
Msimamo wa jumla wa CCM kuhusu haya mambo ya hovyo yanayoendelea nchini ni upi?

Bila shaka mnaunga mkono kila kinachoendelea. Uthibitisho ni viongozi wenu wakuu wa CCM, Mwenyekiti (Bi Samia), wasaidizi wake Wassira, Makala, wabunge wenu na hivyo serikali yote chini ya CCM.

Kwa upande wa pili, uko upande unaopigania justice bila shaka wakiongozwa na CHADEMA kupitia kauli mbiu ya NO Reforms No Election

Basically "reforms" zinazopiganiwa hapa ndio hizi zinazoweza kuondoa mfumo huu mbovu wa utawala ambao kiukweli msingi wake ni mfumo mbaya wa upatikanaji wa viongozi wa kutuongoza yaani "uchaguzi"

Huwezi kupingana na mfumo mbaya usioutaka ukiwa ndani mfumo huohuo ukila matunda ya mfumo huo

Kama wewe na Askofu Gwajima na wengine unaosema mko wengi huko CCM msiokubaliana na uovu huu unaoendelea, basi TOKENI HUKO NA MJITENGE NAO na dunia ijue kweli mmechukia na mnataka hali ibadilike

Otherwise, the birds of the same feathers fly together !
 
Sahihi upo hapo kwa mjadala basi pendekeza namna ya accountability ambayo ni relevant! Ila mpaka sasa hakuna accountability isipokua ni counter-accoutability inayosimaniwa na yeye mwenyewe na Kwa maneno yake Mwenyewe. Rejea kauli yake dhidi ya Gwajima katika Mkutano mkuu wa Ccm Dodoma.
Kwenye hizi nchi zetu za Africa dhana ya uwajibikaji imekuwa na changamoto kubwa katika utekelezaji wake. Chukulia mathalani report za mkaguzi wa hesabu za serikali, ninani huwa anawajibika? Africa kumwambia mtu awajibike nikutangaza uadui na muhusika. Inahitajika utashi wa kisiasa wa viongozi wetu kuondokana na utamaduni huu tuliojijengea.
 
Msimamo wa jumla wa CCM kuhusu haya mambo ya hovyo yanayoendelea nchini ni upi?

Bila shaka mnaunga mkono kila kinachoendelea. Uthibitisho ni viongozi wenu wakuu wa CCM, Mwenyekiti (Bi Samia), wasaidizi wake Wassira, Makala, wabunge wenu na hivyo serikali yote chini ya CCM.

Kwa upande wa pili, uko upande unaopigania justice bila shaka wakiongozwa na CHADEMA kupitia kauli mbiu ya NO Reforms No Election

Basically "reforms" zinazopiganiwa hapa ndio hizi zinazoweza kuondoa mfumo huu mbovu wa utawala ambao kiukweli msingi wake ni mfumo mbaya wa upatikanaji wa viongozi wa kutuongoza yaani "uchaguzi"

Huwezi kupingana na mfumo mbaya usioutaka ukiwa ndani mfumo huohuo ukila matunda ya mfumo huo

Kama wewe na Askofu Gwajima na wengine unaosema mko wengi huko CCM msiokubaliana na uovu huu unaoendelea, basi TOKENI HUKO NA MJITENGE NAO na dunia ijue kweli mmechukia na mnataka hali ibadilike

Otherwise, the birds of the same feathers fly together !
Mtoto akinyea mkono, hatukati mkono! Kujenga taasisi kama CCM sio lele mama. Kama nchi, gharama ya kuisahihisha CCM ni ndogo sana ikilinganishwa na gharama ya kuibomoa. Kazi zote za wanadamu zinayo mapungufu, CCM yapo hali kadhalika na katika vyama vya upinzani pia ikiwemo CHADEMA. Ninaamini kama kuna doria za mitandaoni basi wenye mamlaka wanayofursa ya kuyaona haya yanayolalamikiwa na wananchi. Ni imani yangu watachukua hatua kujisahihisha.
 
Mtoto akinyea mkono, hatukati mkono!
That's true
Kujenga taasisi kama CCM sio lele mama. Kama nchi, gharama ya kuisahihisha CCM ni ndogo sana ikilinganishwa na gharama ya kuibomoa.
CCM kilikuwa kiumbe hai. Kilizaliwa, kikakua, kikaishi, kimezeeka na sasa kilishakufa. Hapo mlipo mnaishi na mzoga/maiti lakini hamtaki kuuzika. Ndiyo sababu ya chaos hii yote
Kazi zote za wanadamu zinayo mapungufu, CCM yapo hali kadhalika na katika vyama vya upinzani pia ikiwemo CHADEMA.
Soma hapo juu. Mwisho wa kazi yoyote ya mwanadamu ni kufa na kufutika kwenye uso wa nchi, inabaki ni historia. Tuiweke CCM makumbusho, imekuwa historia
Ninaamini kama kuna doria za mitandaoni basi wenye mamlaka wanayofursa ya kuyaona haya yanayolalamikiwa na wananchi. Ni imani yangu watachukua hatua kujisahihisha
Wameshayaona ila wanaukataa ukweli

Na kwa kuwa wanaukataa ukweli, si rahisi kupata suluhu ya matatizo haya kwa njia za kawaida. Sometimes, Mungu hulazimika kutumia njia ngumu na za maumivu makali kurekebisha na kuwarudi (punish) wanae na watu wake. Hopefully, tunaipitia njia hii. Na hii ni kwa sbb tu ya ubinafsi (selfishness) na ugumu wa mioyo ya watawala wetu hawa wa leo!!

Laiti wenye mamlaka wakikubali RECONCILIATION, kisha tuka shortlist maeneo ya kuyafanyia REFORMS bila shaka tunaweza kwenda vyema sana kwenye mchakato wa REBUILDING ya taifa na nchi yetu
 
Baada ya kuisikiliza submission ya Mh. Tundu Lisu leo June 16, 2025, kwenye kesi yake ya uhaini nimeikumbuka barua maarufu kama "Letter from Birmingham Jail" ya 1963 Dr. Martin Luther King Jr.'s iliyosema "Injustice anywhere is a threat to justice everywhere,"

Ukiachilia mbali maelekezo ya sheria ya magereza na kanuni zake aliyoyaeleza Mh. Tundu Lisu katika submission yake, hata ibara ya 13(6)(b) ya Katiba ya Tanzania inasema "Ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo"

Nadhani kulikuwa na ukweli fulani kwenye maneno ya Mh Luhaga Mpina kuwa kama demokrasia ya vyama vingi imetushinda ni bora tukaachana nayo tu. Hatuwezi kuwa na wanasiasa ambao, akinusurika jaribio la mauaji lililomwachia ulemavu, tunawaweka kwenye death row, hata kabla hawajahukumiwa!

Mambo kama haya kwa mtu yeyote yule, acting outside ideological fanatism, hawezi kuyaunga mkono. Ninaamini tunaouwezo wa wakujenga nchi moja yenye umoja bila kujali tofauti zetu za kiitikadi. Tanzania ni yetu sote
View attachment 3371754
Kama kumbukumbu zangu ni sahihi;( bila ya kurudi nyuma kutafuta mada husika humu JF); mara yangu ya kwanza kukusoma wewe humu JF, ulijieleza kuwa ni mwanachama hai wa chama cha CCM.

Mada yako hii hapa ni nzuri sana; inaonyesha kujali zaidi uTanzania wetu sote, juu ya hivi vyama vya kisiasa, na hata hizi imani zetu binafsi zinazochangia mifarakanyo ndani ya utaifa wetu.
Hili la imani zetu, najuwa ni gumu kwa wengi wetu; lakini uamini wangu kwa kifupi ni kuwa, kama imani ya mTanzania ni halisi na kumwamini huyo anaye muamini kwenye imani husika; huyo anaye aminiwa hawezi kuwa haitakii mema Tanzania - na hii iwe ni katika imani zote zilizopo.

Lengo langu halikuwa kuzungumzia hizo imani; bali huu uchama katika vyama vya siasa.

Kama upo ndani ya CCM; na mengi yanayofanyika ndani ya chama hicho siyo ya ki-CCM; nawe umo humo humo, kimya huinui kidole wala kutikisa mdomo; huu ni u-CCM wa namna gani?

Hapana, mkuu 'Dr Adam Francis', hainipendezi wala kufurahia kukusuta wewe binafsi, kwa sababu sijui ni ngazi ipi uliyo nayo ndani ya chama; lakini wanachama wenzenu kama akina Lukuvi, Kabutu Mlamaganda; na hata akina Wasira, Nchimbi, Nchemba Madilu, na wengi wengine wa aina yao,... waTanzania wawaelewe vipi wakati kama huu nyote na CCM yenu?

Kweli bado mnaitakia mema Tanzania yetu hii; au mnajitakia mema nyinyi wenyewe?
 
Mtoto akinyea mkono, hatukati mkono! Kujenga taasisi kama CCM sio lele mama. Kama nchi, gharama ya kuisahihisha CCM ni ndogo sana ikilinganishwa na gharama ya kuibomoa. Kazi zote za wanadamu zinayo mapungufu, CCM yapo hali kadhalika na katika vyama vya upinzani pia ikiwemo CHADEMA. Ninaamini kama kuna doria za mitandaoni basi wenye mamlaka wanayofursa ya kuyaona haya yanayolalamikiwa na wananchi. Ni imani yangu watachukua hatua kujisahihisha.
Duh!
Naanzia hapa kuwa na ukinzani mkubwa na wewe!
You indulge yourself in academic semantics forgetting the real issues confronting people?
Hivi KANU, UNIP na wengineo wapo wapi siku hizi?
 
Hii sio ID fake, mm sio mhalifu, kwanini nifiche ID yangu? Unaweza search jina langu katika orodha ya madaktari kwenye link ya msajili wa madaktari Tanganyika (MCT) utalikuta hivi hivi na sura ipo pale.
AIIISEEEE!
Hiyo hadhi yau-daktari unaoutanguliza naomba uuweke pembeni. Huutendei haki hata kidogo!

Umeupata lini, hivi karibuni?

Kuwa na "ID Feki" humu ni kuficha uhalifu, kweli?
Ni wazi hizi makala zako na kujivisha hadhi hizo una lengo maalum; na siyo tofauti kabisa na hao akina Profesa Kabuti Kalamaganda na wengineo.

Lakini ngoja nikurudishe kwenye mwanzo wa mada yako hii.
Hivi bado unadhani kuwa unaendelea kuisimamia mada kama ulivyo ianzisha hapa?

Isije kuwa hata huu udaktari ukawa huutendei haki huko huko katika kutibu wagonjwa, kwa sababu tu akili yako inayo mizunguko mingi sana.

CCM limekuwa ni kama kokoro katika miaka yake yote hii. Sasa hili kokoro linazoa tu hata kila aina ya takataka.
 
Tujiepushe na kutaja watu mahali ambapo hatuna ushahidi. Kwa jinsi UCHAWA ulivyokithiri, upo uwezekano mkubwa wanaoyatenda haya wakawa hawana baraka za Rais. Ushauri wangu, tuyakemee maovu kwa sura yake. CCM ina watu wema kadhalika na wabaya wachache hawawezi kukosa. Chama chenye wanachama milioni 13 si rahisi kutokuwepo wachache waliokengeuka. Hao tukiwajua na kama kuna ushahidi tunaweza kuwataja. Vinginevyo sio busara kufanya mobb justice. Tunawakosea wana CCM wema.
Ajabu ni kuwa, bado nipo hapa; kwenye hii mada niliyo amua kuondoka baada ya hayo niliyoweka huko juu!

Tumekwisha shuhudia watu (waTanzania)wengi tu wa kila aina na fani za elimu za kila aina wakiingia CCM, mwanzo wakionekana kuwa na utulivu wa akili na matumaini yao makubwa kwa nchi yetu.
Lililo wazi na dhahiri kabisa kwa hii miaka ya karibuni, CCM imekuwa sumaku ya kuwavuta ndani ya chama hicho watu wasiokuwa na nia thabiti ya kulijenga taifa letu hili.

Mleta mada si mtu wa kwanza kuachana na taaluma yake na kutafuta maslahi binafsi kupitia njia zile zile walizopitia wengine; kama akina Kigwangwala.
Kwenda kusomea udaktari kutibu wagonjwa siyo wito tena kwao, bali ni njia tu ya kuwafikisha kwenye sega la asali.

Huyu, kwa uandishi wake tu, unaonyesha angefaa kuwa kwenye taaluma tofauti kabisa na hiyo aliyokwenda kupotezea muda wake.

Sasa soma alicho kiandika hapo juu katika maneno niliyo yanyanyua hapo juu, halafu uniambie kuwa huyu kweli ni daktari wa kutibu binaadam maradhi yao; wakati akili yake yote ipo kwenye kupiga propaganda za kumkingia kifua mhalifu mkubwa ndani ya nchi hii sasa hivi.
 
Ccm haina wanachama 13m, labda ukawadanganye waliolala. Hakuna chama chenye wanachama 5m+ nchi hii. Sema ccm wameuza na kugawa kadi 13m, na sio wanachama 13m.
Huyu anajiita Daktari; lakini sijui kama kweli ataelewa ulicho andika hapa!
Kwa kumsoma tokea aingie na mada zake hizi, sioni kuwa anao uwezo wa kutafakari jambo na kulielewa vizuri.

Nisimnyime kila kitu. Anajuwa kupangilia maneno vizuri katika uandishi wake; hata kama hauna mantiki sawasawa.
 
AIIISEEEE!
Hiyo hadhi yau-daktari unaoutanguliza naomba uuweke pembeni. Huutendei haki hata kidogo!

Umeupata lini, hivi karibuni?

Kuwa na "ID Feki" humu ni kuficha uhalifu, kweli?
Ni wazi hizi makala zako na kujivisha hadhi hizo una lengo maalum; na siyo tofauti kabisa na hao akina Profesa Kabuti Kalamaganda na wengineo.

Lakini ngoja nikurudishe kwenye mwanzo wa mada yako hii.
Hivi bado unadhani kuwa unaendelea kuisimamia mada kama ulivyo ianzisha hapa?

Isije kuwa hata huu udaktari ukawa huutendei haki huko huko katika kutibu wagonjwa, kwa sababu tu akili yako inayo mizunguko mingi sana.

CCM limekuwa ni kama kokoro katika miaka yake yote hii. Sasa hili kokoro linazoa tu hata kila aina ya takataka.
Kwanza huu udaktari ni wangu, ukiutaka kasome PCB, baada ya hapo miaka 5 ya medical school, halafu utaongeza mwingine mmoja kupata licence ya kutibu. Kwahiyo nitautanguliza sana, maana nimeusotea.
Pili, maada yangu ipo wazi, sio vizr kumtendea Tundu Lisu ambaye ni mtuhumiwa tu, kama mtu aliyekwisha hukumiwa kifo tayari.
Aidha kila mara, sio leo tu nimekuwa nikiandika kuhusu haki za kiraia, haki za binadamu na umuhimu wa demokrasia. Haya mambo wewe yanakukera nini?
 
Huyu anajiita Daktari; lakini sijui kama kweli ataelewa ulicho andika hapa!
Kwa kumsoma tokea aingie na mada zake hizi, sioni kuwa anao uwezo wa kutafakari jambo na kulielewa vizuri.

Nisimnyime kila kitu. Anajuwa kupangilia maneno vizuri katika uandishi wake; hata kama hauna mantiki sawasawa.
Usichanganye kuelewa na kueleweka. Sina mashaka hoja yangu imeeleweka, changamoto ni ww kuelewa. Kwa kuwa kuelewa ni hatua, na hazilingani kwa wote! Itoshe nikupe muda, kwa wakati wako utanielewa.
 
Ajabu ni kuwa, bado nipo hapa; kwenye hii mada niliyo amua kuondoka baada ya hayo niliyoweka huko juu!

Tumekwisha shuhudia watu (waTanzania)wengi tu wa kila aina na fani za elimu za kila aina wakiingia CCM, mwanzo wakionekana kuwa na utulivu wa akili na matumaini yao makubwa kwa nchi yetu.
Lililo wazi na dhahiri kabisa kwa hii miaka ya karibuni, CCM imekuwa sumaku ya kuwavuta ndani ya chama hicho watu wasiokuwa na nia thabiti ya kulijenga taifa letu hili.

Mleta mada si mtu wa kwanza kuachana na taaluma yake na kutafuta maslahi binafsi kupitia njia zile zile walizopitia wengine; kama akina Kigwangwala.
Kwenda kusomea udaktari kutibu wagonjwa siyo wito tena kwao, bali ni njia tu ya kuwafikisha kwenye sega la asali.

Huyu, kwa uandishi wake tu, unaonyesha angefaa kuwa kwenye taaluma tofauti kabisa na hiyo aliyokwenda kupotezea muda wake.

Sasa soma alicho kiandika hapo juu katika maneno niliyo yanyanyua hapo juu, halafu uniambie kuwa huyu kweli ni daktari wa kutibu binaadam maradhi yao; wakati akili yake yote ipo kwenye kupiga propaganda za kumkingia kifua mhalifu mkubwa ndani ya nchi hii sasa hivi.
Comrade, Rais hanihitaji mimi kumtetea, ana akina Mchengelwa kwaajiri ya kazi hiyo. Chapisho langu ni tahadhari tu tusije tukaingia kwenye matatizo kwa kumhusisha mtu na mambo ambayo tukiambiwa tulete ushahidi yatatughalimu. Mwita Waitara anadaiwa 6B, Cipriani Musiba naye aliamuliwa amlipe Membe, yote haya yakiwa ni madhara ya kuwahusisha watu na tuhuma ambazo ukiambiwa uzithibitishe unaanza kutoa macho.
 
Kama kumbukumbu zangu ni sahihi;( bila ya kurudi nyuma kutafuta mada husika humu JF); mara yangu ya kwanza kukusoma wewe humu JF, ulijieleza kuwa ni mwanachama hai wa chama cha CCM.

Mada yako hii hapa ni nzuri sana; inaonyesha kujali zaidi uTanzania wetu sote, juu ya hivi vyama vya kisiasa, na hata hizi imani zetu binafsi zinazochangia mifarakanyo ndani ya utaifa wetu.
Hili la imani zetu, najuwa ni gumu kwa wengi wetu; lakini uamini wangu kwa kifupi ni kuwa, kama imani ya mTanzania ni halisi na kumwamini huyo anaye muamini kwenye imani husika; huyo anaye aminiwa hawezi kuwa haitakii mema Tanzania - na hii iwe ni katika imani zote zilizopo.

Lengo langu halikuwa kuzungumzia hizo imani; bali huu uchama katika vyama vya siasa.

Kama upo ndani ya CCM; na mengi yanayofanyika ndani ya chama hicho siyo ya ki-CCM; nawe umo humo humo, kimya huinui kidole wala kutikisa mdomo; huu ni u-CCM wa namna gani?

Hapana, mkuu 'Dr Adam Francis', hainipendezi wala kufurahia kukusuta wewe binafsi, kwa sababu sijui ni ngazi ipi uliyo nayo ndani ya chama; lakini wanachama wenzenu kama akina Lukuvi, Kabutu Mlamaganda; na hata akina Wasira, Nchimbi, Nchemba Madilu, na wengi wengine wa aina yao,... waTanzania wawaelewe vipi wakati kama huu nyote na CCM yenu?

Kweli bado mnaitakia mema Tanzania yetu hii; au mnajitakia mema nyinyi wenyewe?
Comrade, Pole pole aliwahi kusema, CCM wahuni wapo na ndio wanaotuharibia chama. Kupambana na wahuni sio kazi rahisi au ya mara moja, ni mradi endelevu. Azimio la Arusha na Kujivua gamba ilikuwa ni jitihada za namna hiyo. Tukikimbia CCM kwasababu kuna wahuni wachache tutakuwa tumewapa ushindi. Tupambane nao tukiwa humuhumu mwisho watatuachia chama chetu.
 
Kwanza huu udaktari ni wangu, ukiutaka kasome PCB, baada ya hapo miaka 5 ya medical school, halafu utaongeza mwingine mmoja kupata licence ya kutibu. Kwahiyo nitautanguliza sana, maana nimeusotea.
Pili, maada yangu ipo wazi, sio vizr kumtendea Tundu Lisu ambaye ni mtuhumiwa tu, kama mtu aliyekwisha hukumiwa kifo tayari.
Aidha kila mara, sio leo tu nimekuwa nikiandika kuhusu haki za kiraia, haki za binadamu na umuhimu wa demokrasia. Haya mambo wewe yanakukera nini?
Umejuwaje kuwa sinao huo u-daktari, au hata zaidi?
Mada yako ni ya kinafiki, isiyokuwa na lengo wala uhalisia wa unachokiandika, ndiyo maana ukajibiwa ulivyo jibiwa

Unapokuwa mlaghai, fahamu tu kuwa watu watakuchukulia hivyo hivyo unavyojifanya mwenyewe.
 
Back
Top Bottom