Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu; Is it a prosecution or persecution?

Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu; Is it a prosecution or persecution?

Usichanganye kuelewa na kueleweka. Sina mashaka hoja yangu imeeleweka, changamoto ni ww kuelewa. Kwa kuwa kuelewa ni hatua, na hazilingani kwa wote! Itoshe nikupe muda, kwa wakati wako utanielewa.
Unajuwaje kuwa sikuelewa; na ni kipimo gani umekitumia kujuwa kuwa "hoja yako imeeleweka". Huoni kuwa unachezea maneno bila ya kuwa na maana yoyote?

Ni hivi, mkuu 'Daktari', wewe nilikuelewa mara tu baada ya kusoma ile mada yako ya kwanza kabisa hapa JF na nikaijibu mada hiyo. Huna lolote 'sophisticated' kiasi usiweze kueleweka kwa hizi mada nyepesinyepesi namna hii zenye lengo maalum. Wewe ni mchumia tumbo tu, huna la ziada.
 
Comrade, Rais hanihitaji mimi kumtetea, ana akina Mchengelwa kwaajiri ya kazi hiyo. Chapisho langu ni tahadhari tu tusije tukaingia kwenye matatizo kwa kumhusisha mtu na mambo ambayo tukiambiwa tulete ushahidi yatatughalimu. Mwita Waitara anadaiwa 6B, Cipriani Musiba naye aliamuliwa amlipe Member, yote haya yakiwa ni madhara ya kuwahusisha watu na tuhuma ambazo ukiambiwa uzithibitishe unaanza kutoa macho.
Yaleyale ya akina Kigwangala!
 
Comrade, Pole pole aliwahi kusema, CCM wahuni wapo na ndio wanaotuharibia chama. Kupambana na wahuni sio kazi rahisi au ya mara moja, ni mradi endelevu. Azimio la Arusha na Kujivua gamba ilikuwa ni jitihada za namna hiyo. Tukikimbia CCM kwasababu kuna wahuni wachache tutakuwa tumewapa ushindi. Tupambane nao tukiwa humuhumu mwisho watatuachia chama chetu.
Kijana, bado upo mbali sana.
Hivi huko vyuoni bado mnafundishwa 'Development studies' kama somo? Najuwa siku hizi hamfundishwi mambo kama hayo. Hilo lilikuwa ni compulsory hata huko unakojidai umepitia.
Hapa inaonyesha wazi huna 'clue' kabisa na unayo yazungumzia. Hilo Azimio la Arusha inawezekana unasikia tu kuliwahi kuwepo kitu kama hicho.
Naona una-'propensity' ya kuzungumzia mambo usiyoyajua, au unayajuwa kwa juu juu tu, sijui kwa sababu zipi hasa. Chukulia ule mfano wa Barua ya Martin Luther King. Hiyo 'quotation" ulivyo iweka kwenye mada yako haipo hivyo!
 
Umejuwaje kuwa sinao huo u-daktari, au hata zaidi?
Mada yako ni ya kinafiki, isiyokuwa na lengo wala uhalisia wa unachokiandika, ndiyo maana ukajibiwa ulivyo jibiwa

Unapokuwa mlaghai, fahamu tu kuwa watu watakuchukulia hivyo hivyo unavyojifanya mwenyewe.
Itoshe tu kusema dunia haijaacha kuzaa wendawazimu.
 
Itoshe tu kusema dunia haijaacha kuzaa wendawazimu.
EEEeenHEEeeee!

Na sasa utakuja na kusema hicho ki-MD ndicho kimekuwezesha kujuwa hali yangu ilivyo!
Wewe uliingia kwenye fani hiyo kimakosa kabisa. Wewe ulitakiwa kuwa kwenye fani ya sanaa, kama alivyo Samia Suluhu Hassan; ambaye sasa hivi unafanya kila liwezekanalo akutambue katika u-malkia wake mnaompigania hapa kuupata.

Hovyo Kabisa!
 
Tujiepushe na kutaja watu mahali ambapo hatuna ushahidi. Kwa jinsi UCHAWA ulivyokithiri, upo uwezekano mkubwa wanaoyatenda haya wakawa hawana baraka za Rais. Ushauri wangu, tuyakemee maovu kwa sura yake. CCM ina watu wema kadhalika na wabaya wachache hawawezi kukosa. Chama chenye wanachama milioni 13 si rahisi kutokuwepo wachache waliokengeuka. Hao tukiwajua na kama kuna ushahidi tunaweza kuwataja. Vinginevyo sio busara kufanya mobb justice. Tunawakosea wana CCM wema.
"Tujiepushe na kutaja watu mahali ambapo hatuna ushahidi. Kwa jinsi UCHAWA ulivyokithiri, upo uwezekano mkubwa wanaoyatenda haya wakawa hawana baraka za Rais."

Mkuu upo serious na hii kauli yako? Ni kwamba Rais haya yanayofanyika hajatoa ruhusa? Basi asingemsaka gwajima na kumzingua kila anayejitokeza na kupinga huu udhalimu.
 
Tujiepushe na kutaja watu mahali ambapo hatuna ushahidi. Kwa jinsi UCHAWA ulivyokithiri, upo uwezekano mkubwa wanaoyatenda haya wakawa hawana baraka za Rais. Ushauri wangu, tuyakemee maovu kwa sura yake. CCM ina watu wema kadhalika na wabaya wachache hawawezi kukosa. Chama chenye wanachama milioni 13 si rahisi kutokuwepo wachache waliokengeuka. Hao tukiwajua na kama kuna ushahidi tunaweza kuwataja. Vinginevyo sio busara kufanya mobb justice. Tunawakosea wana CCM wema.
Jinsi mfalme alivyo ndivyo na watu wake walivyo.
 
EEEeenHEEeeee!

Na sasa utakuja na kusema hicho ki-MD ndicho kimekuwezesha kujuwa hali yangu ilivyo!
Wewe uliingia kwenye fani hiyo kimakosa kabisa. Wewe ulitakiwa kuwa kwenye fani ya sanaa, kama alivyo Samia Suluhu Hassan; ambaye sasa hivi unafanya kila liwezekanalo akutambue katika u-malkia wake mnaompigania hapa kuupata.

Hovyo Kabisa!
Haya unayoendelea kuyachapisha yanakuvunjia heshma. Ukikakaa kimya utakuwa umejisitiri sana.
 
Haya unayoendelea kuyachapisha yanakuvunjia heshma. Ukikakaa kimya utakuwa umejisitiri sana.
Hapana. Niliona ni vizuri nikupe taarifa hizo; ukiwa na hekima kidogo utajifikiria na kuona sababu zinazofanya ujibiwe hivyo.
Siwezi "kujisitiri", kwa lolote ninaloliandika hapa, kwa sababu sina shaka na ninachokiandika. Maandishi yako ni 'provocative'; ukiyaweka kana kwamba unao ujuzi maalumu juu yake. Some of us can see through all that deception.

Tulia, andika kama ulivyo, siyo kwa unafiki unaotaka uonekane kuwa ndio ukweli uujuao.
 
Aidha kila mara, sio leo tu nimekuwa nikiandika kuhusu haki za kiraia, haki za binadamu na umuhimu wa demokrasia. Haya mambo wewe yanakukera nini?
Uandishi wako "unakera", usivyo kuwa 'sincere', unavyoonekana kujaa unafiki; unavyo jichanganya wenyewe. Hauna uhalisia wowote, bali ni wa hadaa tu, kama ilivyo kwa Samia na mambo yake mengi; kama zile $Rs, na maigizo mengi mengine.
 
Mchawi ndiye huwa wa kwanza kuja kukujulia hali asubuhi na mapema, huyu mleta mada anapima watu akili zao na kujaribu kuwasafisha CCM kwa uovu wao.

Labda aanze kwa kutaja mwana ccm mwema.
 
Tujiepushe na kutaja watu mahali ambapo hatuna ushahidi. Kwa jinsi UCHAWA ulivyokithiri, upo uwezekano mkubwa wanaoyatenda haya wakawa hawana baraka za Rais. Ushauri wangu, tuyakemee maovu kwa sura yake. CCM ina watu wema kadhalika na wabaya wachache hawawezi kukosa. Chama chenye wanachama milioni 13 si rahisi kutokuwepo wachache waliokengeuka. Hao tukiwajua na kama kuna ushahidi tunaweza kuwataja. Vinginevyo sio busara kufanya mobb justice. Tunawakosea wana CCM wema.
Unaanzaje kuwataja, wewe unadhani watu milini 60 wote hawawajui wanaotenda hayo maovu??
 
Sidhani kama kuna siku CCM ilikaa kuadhimia kuwa Tundu Lisu ashitakiwe. Haya ni mawazo ya watu wachache waliopewa dhamana. Wapo wana CCM wengi tu ambao hawakubaliani na haya mambo.
Hilo ni kweli lkn wasemee wapi, kila mtu kafungwa miguu na mikono.
 
Sidhani kama kuna siku CCM ilikaa kuadhimia kuwa Tundu Lisu ashitakiwe. Haya ni mawazo ya watu wachache waliopewa dhamana. Wapo wana CCM wengi tu ambao hawakubaliani na haya mambo.
Si wajiondoe ccm kama hawakubaliani na upuuzi huo?
 
Back
Top Bottom