UPDATE 5: Kesi ya Thadei Kweka
December 31, 2025
1. Upande wa Jamuhuri wamepeleka Maombi (Ex-parte) Mahakaman kwa hati ya dharula na yamesikilizwa Upande mmoja bila Thadey Sabinus Kweka kuwepo Mahakaman ukizingatia kuwa yupo mikononi mwao.
2. Maombi hayo yanahusu kumtaka Thadey Sabinus Kweka kutoa Nywila (password) za simu yake ili Polis wafanye upelelezi.
3. Mahakama imetoa Amri kuwa Thadey Sabinus Kweka anatakiwa kutoa Nywila (password) za Simu yake ili Polisi wafanye uchunguzi.
4. Thadei ameshindwa kutoa password kwa sababu haikumbuki baada ya kupitia unyanyasaji wa kisaikolojia tokea akamatwe. Zoezi la kutoa password limeshindikana hadi kesho Thadei akikumbuka password yake.
5. Polis bado wamemkatalia Thadei dhamana na kusaini consent forms kutoka ubalozi wa Marekani ili America iwe involved.
6. Thadei anashtakiwa kuchapisha taarifa za uongo kwenye groups za ”what sup”. What sup hatujui ni Application gani haya Thadei mwenyewe haelewi!
Tutaendelea kuwapa taarifa.
#FreeThadeiKweka
Asante
View attachment 3523512