Kesi ya Mbowe: Usalama wa Diary ya Msemwa unahakikiwa vipi?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,854
35,861
Shahidi Msemwa kwenye shauri ndani ya shauri la kesi hii, alikutikana na vitu vya chabo asivyopaswa kuwa navyo kizimbani.

Kwanini utetezi hawakwenda mbele zaidi kuhitaji kumkagua thoroughly kujiridhisha na kuvipata vyote?

Kwanini simu alirejeshewa bila kuwa imefanyiwa dodoso lolote?

Kwanini diary haikukaguliwa jana hiyo hiyo au hata kuchukuliwa snapshots zozote?

Usalama wa diary hii uko vipi mikononi mwa store ya mahakama iliyotoa detention register mapema kinyume cha utaratibu majuzi tu?

Nani anaamimika wapi kwenye kesi hii?

Hakujakabidhiwa fisi hapa, kutulindia bucha?
-----------

Msingi wa hoja:

Kesi ya Mbowe: Ushauri wa Bure kwa Mawakili Wasomi - Utetezi
 
Kilichotia fora ni shahidi kutoa hivyo vitu pindi alipomsikia Kibatala huku akibaki kusikitika kwa kuingizwa mkenge na mawakili wa jamhuri..

Nirudi kwenye mada, pale hamna usalama wowote. Ila hili jambo limetupa mwanga kwa hatua zingine za kesi inavyoendelea
 
Hii diary haina s/n kama ule wimbo wa A5340. Jumatatu inaweza kuwa diary nyingine au several pages missing.

Pana haja ya kutopuuzia jambo.
 
Kuna neno jana Kibatala alitamka, "UTU"
Alisema tungeweza kwenda mbali zaidi kwa kumkagua Shahidi kwani ana vitu vingine zaidi ya hivi, lkn kwa sababu ya utu basi tunamuacha.

Neno hilo binafsi lilinitatiza na linanitatiza sana. Hawa ndugu wana utu gani wao?

Wamemwonyesha nani utu hawa? Ni Mbowe, Adamoo, Bwire, Ling'wenya au Lijenje?

Ninakazia - hatupashwi kudharau au kupuuzia jambo kwenye kupambana na hawa watu..

Tusimwangalie nyani usoni. Hawa tusiyaangalie makunyanzi yao kama wasivyoangalia yetu.
 
Hawakumkagua vizuri shahidi ikiwemo kumpekea mifukoni kwa nia ya kumlindia utu wake, japo binafsi kwangu ningependa akaguliwe mpaka mifukoni kwasababu shahidi alishaonesha hakuwa na nia nzuri kwenye kesi yenyewe, na mahakama kama ofisi.

Usalama wa diary hiyo mikononi mwa mahakama ni mdogo au haupo kabisa kutokana na kitendo kilichofanyika siku chache zilizopita kuonesha kuna mawasiliano yasiyo halali kati ya jamhuri na mahakama, lakini binafsi hili halinitishi, kisaikolojia yule shahidi wa jana ameshaondolewa relini hata kama akiruhusiwa kuendelea na ushahidi wake.

Hii kesi la muhimu ni kusubiri mwisho wake tu uonekane, kuna mambo yanayokiuka taratibu za kutoa ushahidi na kanuni za mahakama yanayofumbiwa macho kwa lengo la kuwabeba jamhuri.

Ule uhuni alioonesha shahidi jana haukutakiwa kusubiri mpaka jumatatu ndio utafutiwe suluhisho, ni suala dogo la jaji kuangalia ni sheria na taratibu zipi zimekiukwa na shahidi na kuamua in favour of defence.
 
Nachojua hii kazi ni ya Jaji ina maana Jaji hawezi kuona watu wanaotumia dairy au simu kizimbani mpaka watetezi tena sijui Profesa Jay ndio anamstua Kibatala wana simu wale nilicheka sana...hii kesi ni vichekesho mtuhumiwa anaendelea kutoa ushahidi huku kala kiapo na anadanganya mahakama na mahakama ipo kimya...
 
Mnawapa mawakili wajibu mkubwa sana juu ya kazi zao za kawaida ambazo wanafanya.

Raia wote ndio walipaswa kuzifanya mahakama sehemu ya kuaminika. Dayari ilikuwa ibaki mahakamani au iende polisi tu, kuipiga picha pia ingeamuliwa kufanywa na mtu wa mahakama au polisi tu.

Hakuna namna hiyo dayari au kumbukumbu zake zingehifadhiwa nje ya hizo sehemu mbili.
 
Binafsi, nilikuwa ninafikiri, ni bora angeachiwa hiyo Diary yake kuliko ile simu. Kwani kwenye simu, ungeweza kupatikana ushahidi wa wazi, na kutoka kwa nani. Yaani pale, inawezekana, aliyokuwa anafundishwa kwa kutumiwa MSG ndiyo aliyokuwa anayahamishia kwenye Diary kwa ajili ya kuyakariri!
Fursa hiyo imeshapotea! Watakuwa makini zaidi!
 
Mnawapa mawakili wajibu mkubwa sana juu ya kazi zao za kawaida ambazo wanafanya.
Raia wote ndio walipaswa kuzifanya mahakama sehemu ya kuaminika. Dayari ilikuwa ibaki mahakamani au iende polisi tu, kuipiga picha pia ingeamuliwa kufanywa na mtu wa mahakama au polisi tu. Hakuna namna hiyo dayari au kumbukumbu zake zingehifadhiwa nje ya hizo sehemu mbili.
Unataka raia wafanye kitu gani kuzifanya mahakama ziaminike ikiwa hili ni jukumu la jaji kama kiongozi wa ofisi yake (mahakama), ulitaka raia waandamane? na wakiandamana si ndio wataambiwa wanataka kuingilia uhuru wa mahakama?

Kiuhalisia polisi na mahakama wote hawaaminiki kwenye hili suala, wameshaonesha wanashirikiana na jamhuri isivyo halali kuwalinda mashahidi wanaokiuka viapo vyao, na hili ni jukumu la jaji/ mahakama kutoa majibu sahihi kulingana na sheria kwasababu yako chini yake, bahati mbaya jaji nae ni timu inayovunja taratibu.
 
Binafsi awali hata Mimi Nilikuwa na wasiwasi huo. Lakini baada ya kujiridhIsha kuwa ukaguzi ulifanyika na kilichomo kikajulikana Kwa wote basi nikatulia. Kumbuka wakati wanaibua hoja hii Kibatala alisemà Mawakili wa pande zote 2 twende tumkague shahidi na katika kukagua Kwa pamoja waliona kilichomo. Hata wakibadili itaendelea kuivua nguo zaidi Mahakama inayouza ramani ya vita.
 
Hawa jamaa wanaaminika mkuu? Ni Jaji, mashahidi au ma WS?

Kesi ya Mbowe: Tujipange zaidi kwenye kuuweka Uongo Peupe
 
Sasa mawakili wachache wasiozidi 20 wafanye nini au wangefanya nini kuhakikisha dayari inakuwa salama?
Hawa mawakili wakati mwingine wanatwishwa mzigo mzito kana kwamba wao ndio wanapaswa kuwa wakombozi wa nchi hii.
Unataka raia wafanye kitu gani kuzifanya mahakama ziaminike ikiwa hili ni jukumu la jaji kama kiongozi wa ofisi yake (mahakama), ulitaka raia waandamane? na wakiandamana si ndio wataambiwa wanataka kuingilia uhuru wa mahakama?

Kiuhalisia polisi na mahakama wote hawaaminiki kwenye hili suala, wameshaonesha wanashirikiana na jamhuri isivyo halali kuwalinda mashahidi wanaokiuka viapo vyao, na hili ni jukumu la jaji/ mahakama kutoa majibu sahihi kulingana na sheria kwasababu yako chini yake, bahati mbaya jaji nae ni timu inayovunja taratibu.
 
Mnawapa mawakili wajibu mkubwa sana juu ya kazi zao za kawaida ambazo wanafanya.
Raia wote ndio walipaswa kuzifanya mahakama sehemu ya kuaminika. Dayari ilikuwa ibaki mahakamani au iende polisi tu, kuipiga picha pia ingeamuliwa kufanywa na mtu wa mahakama au polisi tu. Hakuna namna hiyo dayari au kumbukumbu zake zingehifadhiwa nje ya hizo sehemu mbili.

Si Jaji, mashahidi au ma WS wanaaminika kwenye kesi hii tena.

Kesi ya Mbowe: Tujipange zaidi kwenye kuuweka Uongo Peupe

Haipo haki yoyote tunayotegemea kupata katika mahakama hii.

Zaidi sana tungejipanga katika kuwaumbua kwenye ghiliba na hadaa zao.
 
Sio rahisi hivyo.
Utaratibu wa kuikagua hiyo simu ungeweza kuhitaji watu wengine zaidi na kuchukua hata zaidi ya wiki moja jambo ambalo ingekuwa ni kupoteza muda tu. Mawakili wamekuwa strategic kutotaka hili suala kuchukua muda adimu wa kesi yao.

Back
Top Bottom