mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,039
Inawezekanaje watu wapange utaratibu ambao siyo rafiki kwa waajiriwa wapya? Iko hivi: Ukipangiwa ajira na sekretarieti ya ajira kwa maana ya kufaulu usaili, unapewa barua ya kuripoti kazini ndani ya siku 14 vinginevyo nafasi yako atapewa mwingine!
Hii inamfanya mwajiriwa atafute nauli hata kwa kukopa toka huko aliko na kusafiri hadi kituo alichopangwa. Akifika huko wanakagua vyeti vyake halisi, na kujaza taarifa zake binafsi kisha huambiwa RUDI NYUMBANI NA TUKIKAMILISHA TARATIBU ZA AJIRA TUTAKUITA KWA SIMU!!
Hapo wameshamaliza na unatoka ofisini bila hata senti moja! Hawajali utalala wapi na utakula wapi na usalama wako ni upi! na utasafiri vipi na utarudi tena vipi!!
Niliposikia kwa mara ya kwanza kwa mtu aliyekuwa amepangiwa halmashauri moja huko Tabora sikuamini kuwa huo ndio utaratibu!! Nilifikiri ni roho mbaya tu ya wahusika huko halmashauri ya Tabora!! Juzi juzi kuna dogo alipata nafasi katika moja ya manispaa za Dar.
Naye aliporipoti alipokelewa na kukaguluiwa vyeti vyake na kujaza fomu za personal particulars na kuambiwa arudi hadi atakapopigiwa simu! Ni wiki nimepita sasa na bado hajapigiwa simu na anajibanza tu kwa watu na hajui hadi lini!! Huu utaratibu una usumbufu sana!!
Ninachofahamu watu huitwa wakati serikali imeshafanya maandalizi tayari ya kuwapokea na kuwahudumia!! Yaani kijana amesota na interview kibao kwa gharama kubwa sana ya nauli, malazi na chakula, sasa ameitwa kwenye ajira bado anasoteshwa!
Niwaulize nyie mnaowafanyia hivyo wenzenu mnajua masaibu wanayopambana nayo wanaposubiria? Wengine wanalala kwenye vituo vya mabasi kwa kukosa pesa za gesti na nauli ya kurudi tena nyumbani hawana! Tafadhali angalau siku wanaporipoti wapeni zile posho za kujikimu zilizopo kisheria ili ziwalinde wanaposubiria!