JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Hali hii imekuwa ikitokea mara nyingi lakini nimeona niseme ili kama ujumbe huu utawafikia mamlaka basi wabadilishe mbinu na ikiwezekana wachukue hatua.
Mizigo ya abiria inakaguliwa wakati wa kutoka Unguja, ukifika Bandari ya Dar napo ukaguzi unachukua muda kwa kuwa unalazimika kupanga foleni ili mizigo ipote kwenye mashine, sijui kwa nini hawana utaratibu mzuri wa kurahisisha mambo, angalia hivyo video niliyoirekodi kwa ufupi juzi.
Najua watu hawakatai kukaguliwa mizigo, ila utaratibu ni mbovu.