Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Baada ya Mdau kueleza juu ya kero ya foleni kwenye Bandari ya Dar es Salaam hasa kwa abiria wanaotoka Zanzibar, Mamlaka ya Bandari umeeleza kuwa changamoto hiyo imemalizika baada ya kufungwa kwa mashine mbili kubwa za kukagua mizigo "scanner".
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amesema "Kwa siku tunahudumia abiria 6,000 hadi 7,000, mashine tulizofunga zina uwezo mzubwa na zinaweza kubeba mzigo hata wa Tani 3."
Ameongeza "Changamoto iliyopo ni Meli kutotofautiana muda wa kuwasili, zinapofika kunakuwa na watu wengi kwa wakati mmoja, nadhani tutazungumza na Mamlaka zinazoratibu safari kuhusu muda wa Meli kuwasili angalau wawaachanishe kidogo."