A
Anonymous
Guest
Matukio hayo yalinishangaza sana, kwanza wahusika wa mabasi wenyewe wanaona kabisa basi limejaa lakini wanaendelea kuingiza abiria zaidi.
Pili abiria wenyewe wanaingia wanakuta hakuna siti iliyo wazi, kote kumejaa na bado hawalalamiki.
Yaani basi limejaza abiria kama vile mnaenda Daladala za Mbagala ama Gongo la Mboto kumbe ni safari ya masafa marefu, kilichonikera zaidi mtu anakuinamia kwenye siti yako, harufu ya jasho lake yaaani ni kero tupu,
Hakuna hata raha ya kupanda hili basi, hii sio mara ya kwanza, kwani nilijua ni ukitokea Moro tu lakini niliposiri tena kutoka Dar Kwenda Moro nikakutana na hali hiyohiyo.
Ukipanda Stendi Kuu kutoka Dar kila kitu kiko poa, subiri mfike kuanzia maeneo ya Kibamba ama Misugusugu kule Ubena Zomozi wanajaza abiria wa kusimama hasa nyakati za Alasiri kwenda jioni.
Huu utaratibu ni mbovu sana, nimeshaona pia katika mabasi ya kampuni kadhaa nyingine ambazo hazina umaarufu lakini kama Abood nao wameanza hii tabia, inamaanisha hatua zinatakiwa kuchukuliwa haraka, kwani mbali na kuwa kero pia sio salama kiafya na wanavunja utaratibu waliowekewa na mamlaka za usafirishaji.
Serikali inasisitiza mabasi yatumie Digitali katika kudhibiti mapato na kurahisisha mchakato wa ukataji tiketi, lakini hiki kinachofanyika inamaanisha kina baraka za wale Maafisa wanaosimamia vyombo vya moto barabarani kwa kuwa nina uhakika wanaona na hawachukui hatua kwasababu wanazozijua wao.
Kingine mrundikano wa Abiria unaweza kuchangia kuambukizana kwa magonjwa na hata ikitokea changamoto mfano hajali, wale walioongezeka hawatapata haki zao wanazostahili kwa kuwa hatakuwemo kwenye orodha.