Kampuni ya JEFAG Logistics: Kero ya foleni na ajali Kurasini

willpower

JF-Expert Member
Dec 3, 2019
404
2,271
Kampuni ya JEFAG Logistics iliyopo Kurasini Dar es Salaam imekuwa ikisababisha kero ya foleni kwa watumiaji wa barabara inayoelekea daraja la Mwalimu Nyerere (Daraja la Kigamboni) kutokana na mipangilio mibovu ya magari ya mizigo.

Muda wa asubuhi malori ya mizigo hujipanga barabarani karibu na daraja la treni huku malori mengine yakiziba njia inayoelekea zilipo ofisi za CCECC, Star oil na METL.

Kero hii inawalazimisha watumiaji wengine wa barabara kuegesha magari yao mahali pasipostahili kwa kuwa malori yanayoingia kwenye kampuni hii huwa yameziba njia yote; ya kwenda na kurudi.

Kwa akili ya kawaida nimegundua kuwa tatizo ni kuwa na malori mengi yanayokuja kushusha ama kupakia kontena wakati hakuna nafasi ya kutosha.

Mara kadhaa nimekuwa nikiona Polisi wakizunguka maeneo hayo lakini hakuna kinachofanyika.

Hofu yangu kubwa ni kuendelea kutokea kwa ajali hasa majira ya usiku kwa kuwa haya malori huwa yanaachwa barabarani huku madereva wakiwa wanaendelea na soga kwenye vijiwe vyao. Haya malori mengi hayana reflector na huwa yameegeshwa kwenye kona.

Wiki iliyopita kuna ajali ilitokea baada ya jamaa aliyekuwa anaendeesha BMW kuingia nyuma ya Lori lililokuwa limeegeshwa barabarani. Bahati nzuri hakuna aliyefariki ila BMW haifai tena na jamaa anauguza majeraha kwa sasa.

Kwa jinsi ilivyo Dereva anayekuja akikata kona tu anakutana na tela la lori limeegeshwa barabarani. Hii ni hatari sana. Hii barabara ndio inayoleta magari kutoka Uhasibu na Bandarini kwa wanaovuka kwenda Kigamboni.

Pembeni tu kuna kituo cha Polisi - Darajani Police Post; hawa nao hakuna wanachofanya zaidi ya kulala tu.

Wahusika wa kampuni ya JEFAG Logistics, Polisi na mamlaka nyingine, mnasubiri hadi basi zile Machinga Complex - Kigamboni iingie nyuma ya Lori na wafe watu 40 ndio mfanye jambo sahihi?

Watu wakifa hapo bado mtasema kuwa ‘’Kazi ya Mungu haina makosa?’’

Au hili nalo linahitaji Rais wa nchi Mama Samia kulishughulikia? Halafu tuseme mama anaupiga mwingi? Au apigiwe simu Makonda ili atoe agizo kwa jeshi la polisi? Au bango liwekwe kwenye maandamano ya CHADEMA?

Kwa nini Polisi wanaweza wa kwenda kufuata posho za mafuta kwenye njia hiyo hiyo lakini hawashughuliki na kero hii?

Kwanini tumekuwa na fikra mbovu za kutotaka kutimiza wajibu hata kwa kiwango cha chini kabisa?

Tumelogwa ama ni wajinga tu?

Timiza wajibu.
 
Leo asubuhi hali ilikuwa mbaya zaidi. Ni hatari kwa sisi watumiaji wa daraja la Kigamboni.
Traffic Police wapo bize kusumbuana na vijana wa bodaboda na bajani pale juu lakini haya malori kama hawayaoni hivi.

Kuna wakati nahisi labda kuna fungu wanapewa hivyo hizi kampuni ziendelee tu kuvunja sheria.

Ni abu kwa jeshi la polisi
 
Inasemekana lakini; wanaotakiwa kusimamia hili wanapewa mgao wao kila wiki ili mambo yaende hivyo yalivyo. Watu wanatembeza hela kwa wasimamizi wa sheria ili wafanye wanavyotaka.

Juzi basi la abiria ilibaki kidogo tu liingie nyuma ya Lori na kwa ile nyomi na mwendo kasi hapo wangekufa watu sio chini ya 30.

Wakishakufa mtasema ''AJALI HAINA KINGA''
 
Hawa madereva wa malori afadhali wangekuwa na akili kidogo,hawana akili kabisa. Unakuta wamepaki lane zote 2 wanasubiri kuingia depot ambapo hawajui wataingia muda gani! Sijui kwanini hawaegeshi lane moja. Kuna mtu aliniambia wale ni deiwaka tu madereva wanachukua lori mbele huko likishapakia mzigo.
 
Hawa madereva wa malori afadhali wangekuwa na akili kidogo,hawana akili kabisa. Unakuta wamepaki lane zote 2 wanasubiri kuingia depot ambapo hawajui wataingia muda gani! Sijui kwanini hawaegeshi lane moja. Kuna mtu aliniambia wale ni deiwaka tu madereva wanachukua lori mbele huko likishapakia mzigo.
Wanyonge tulieni matajiri tufanye yetu sasa,kipindi cha Mwendazake mlitutesa sana, sasa hivi hata mkilia mkatoa machozi ya samaki hakuna mamlaka itakayo wasikiliza,maana mamlaka zote tumeziweka mfukoni tunalamba nazo asali!!
 
Wanyonge tulieni matajiri tufanye yetu sasa,kipindi cha Mwendazake mlitutesa sana, sasa hivi hata mkilia mkatoa machozi ya samaki hakuna mamlaka itakayo wasikiliza,maana mamlaka zote tumeziweka mfukoni tunalamba nazo asali!!
Sawa tajiri lamba asali tu
 
Wakati wa Magufuli alitoa tamko mara moja tu lile eneo lote kutoka TRH mpaka Uhasibu lilikuwa jeupe bila kuwepo kwa malori yanayoegeshwa pembeni na barabarani.

Tangu amekufa wenye malori na madereva wao wanafanya wanavyotaka.
 
Back
Top Bottom