Kero gani umewahi kukutana nayo kutoka kwa abiria mwenzio wakati unasafiri?

Nilipanda na mdada mmoja akaagiza mayai ya kuchemsha akala, mahindi ya kuchoma yakapita akanunua akala, koni za bakhresa akala, korosho zikapita akaitisha akala...baadae akaanza kuharibu hali ya hewa. Ninashukuru mungu safari yake iliishia njiani baada ya kubanwa na tumbo la kuhara tukamshusha nzega.
 
Nilipanda na mdada mmoja akaagiza mayai ya kuchemsha akala, mahindi ya kuchoma yakapita akanunua akala, koni za bakhresa akala, korosho zikapita akaitisha akala...baadae akaanza kuharibu hali ya hewa. Ninashukuru mungu safari yake iliishia njiani baada ya kubanwa na tumbo la kuhara tukamshusha nzega.
Nimecheka kama fala
 
Ebana Kuna Jamaa hakupiga mswaki alafu story aziishi na maswali yasiyo eleweka.


Vipi wewe Mkuu?
Binti mmoja alitapika kuanzia Mpanda hadi Dar.
Nilichukia sana lkn baadaye nikamhurumia.

KUna wakati akaniomba radhi sana kwa hali hiyo..
Nikamtia moyo kuwa asijali kwani hakukusudia bali ubinadamu.

Mwisho nilijaribu kuvaa viatu vyake, nikajiuliza ingenitokea mimi ingekuwaje?

Kumbe kuchukuliana ni jambo muhimu sana
 
Njiani Kuna vituko sana

Miaka ya nyuma niliwahi kupangiwa siti na dada mmoja sister du kinoma sema alikua Pisi sana maringo mengi, kwenye kutafta siti namuona ndo kaka kiti Cha pembeni nikasema mambo si ndo haya, ebana ile nampa salamu dada kanikata jicho Wala hakuitika akatoa ipad yake(kipindi hicho 2nd generation) akaweka earphones Wala hakunisemesha, nikafadhaika nikasema poa tu


Njiani kufika ile sehem ya chakula nikavuta sambusa zangu na soda take away nikarudi zangu kwenye gari, sister du kaja na chips kavu nyama choma na kachumbari ya kutosha ( big big mistake) 😃😃


Sasa sijui ile kachumbari ilikua imelala au vipi, aisee baada ya muda safari kuendelea sister duh tumbo likavuruga, kama usiwahi pata tumbo la kuhara najua Kila mtu anaelewa mziki wake, sister du akaanza kuomba kujisaidia maporini, konda akawa anamkubalia anampa na maji ya kujisafisha Yale ya emergency kwenye madumu kwa ajili ya kupooza rejeta, anaingia porini anafanya yake anarudi, tumbo nalo halina adabu ukikaa tu ndo linachanganya zaidi😃😃


Akapiga trip kadhaa abiria wakaanza kua wakali gari linasimama Kila muda, mi hapo Sina habari na mi nikatupia earphones zangu... Kuja mwangalia huyu sister du aisee anataka kulia anajinyonga nyoga sio poa nikaingiwa na Imani nikamzingua konda pale na abiria kadhaa wakisimama akatoka tena, maji yashaisha anapewa zile hand tissues, aisee huyu sister du sijui nguvu zilimuishia au alikua ashavurugwa yaani akawa haendi porini tena, akishuka tu anavua nguo anaachia mzigo karibu na gari kabisa, watu wanafanya Kuona aibu kumtazama wanaangalia pembeni....


Kuna mama akamstiri kanga maana nguo ilishaanza kulowana kwa nyuma, tukafika Kijiji kimoja nikaongea na konda pale nikashuka nikaenda pharmacy Kuna dawa nikamchukulia na maji, Mungu saidia tumbo likatulia mpaka tunafika.... Alikuja kuniomba namba mwenyewe kwa aibu


Wahenga sio watu nilikuja kupita nae kimasahara na mpaka Leo tunawasiliana mara moja Moja ana maduka tu makubwa ya electronics kariakoo aliotea kuolewa na jamaa kibopa hatari
,
 
Nilipanda na mdada mmoja akaagiza mayai ya kuchemsha akala, mahindi ya kuchoma yakapita akanunua akala, koni za bakhresa akala, korosho zikapita akaitisha akala...baadae akaanza kuharibu hali ya hewa. Ninashukuru mungu safari yake iliishia njiani baada ya kubanwa na tumbo la kuhara tukamshusha nzega.
Kuna watu wanakula njian ni hatari
 
Umenikumbusha story iliyotrend ya miaka ya nyuma, kuna muingereza alikuwa anatoa mashuzi mpaka ikalazimu ndege kutua ghafla ili ashushwe maana abiria wengine walikuwa wanateseka kwa harufu
 
2017 Tukiwa kwenye Nyehunge ya Mwanza kwenda Mji kasoro Bahari.
Kuna Mzee mmoja kufika hapo Bahi akaomba kwenye kukata Gogo,akiwa nachupa yake ya maji.

Mimi nikiwa sehemu ya abiri tuliopiga kelele kuwa ametumia muda mwingi kukata Gogo😀😀😀Mungu Baba tusamehe

Mzee yule akarudi na ile chupa ikiwa ina maji kidogo.Na bahati alikaa na mdada.

Safari ikiwa inaendelea ile jioni,Mvua ikanyesha?Ac ya Basi ikawa inazingua.

Abiria tukaanza kuhisi harufu kali,kumbe mzee ile kuogopa kelele za abiria kuomba tena kukata gogo ni kama aliteleza kidogo ka uhalisho kakapita.

Ile safari ilikuwa ngumu mno,mvuq inanyesha,mkifungua madirisha maji yanaingia,licha ya mzee kushuka na kubadili nguo bado ile harufu ilibaki mle ndani.Aiseee tuliteseka ile siku sio kitoto.
Alikuja kushukia hapo Dakawa.

Toka ile siku nilijifunza kuchukuliana kwa Upendo.😀😀😀😀
 
Demu kujambajamba kila muda na kuniomba msamaha kwa sababu alikuwa anaharisha. Pia aliomba tubadilishane viti ili akae njiani ili basi likisimama awahi kukimbia kuchimba dawa maana alikuwa anaharisha
 
1. Kung'ang'ania siti ya dirishani ili hali hajakata
2. Abiria ana watoto kadha na amekata siti 1
3. Kutapika au kutetema mate
4. Yero kula ugoro na kufungua kioo ateme
5. Mchanganyobwa mafuta na pafyum kwenye gari
6. Abiria kusimama wakati basi limejaa na kuanza kugasi tuliokaa karibu na njia
 
Back
Top Bottom