Kenya: Rais Samia afungua kongamano la wafanyabiashara nchini Kenya, Rostam Aziz atema madini ukumbi mzima wamshangilia

Tapeli hilo.

Biashara yake kuu ni MADAWA YA KULEVYA.

Huwezi kusikia amefanya uwekezaji wenye tija.

Akiwa ana biashara mahali ujue hicho ni kichaka cha UTAKATISHAJI WA FEDHA ZA MADAWA YA KULEVYA, UHUJUMU UCHUMI na KUONGOZA MAGENGE YA UHALIFU.
Ndio maana utaona wakenya wana zaidi ya makampuni 500 hapa Tanzania na sisi tumewekeza kwao kwa kampuni zisizozidi 30. Kwa akili hizi za kimaskini kuwa kila Mtanzania tajiri ni mpiga dili ndio tutaendelea kuwa maskini hivi hivi ila akija mgeni tunamyenyekea
 
Rais alisema anataka kurudisha pesa kwenye mzunguko, na watu muhimu kutimiza hilo ni wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa, Mungu amsaidie atimize lengo lake bila wapiga dili kujitokeza na kumuharibia nia yake nzuri kwa Mtanzania.
Ulikwenda.wapi Mkuu
 
Nina imani, nchi yetu ipo kwenye njia sahihi baada ya kupotezwa kwa miaka mitano.

Tukazanie kujenga mifumo itakayozuia Taifa kuangukia kwenye uongozi wa watu wasio na uwezo. Mifumo iwezeshe, akitokea kiongozi wa hovyo, kuwe na utaratibu rahisi wa kumwondoa.

Fikirieni miaka mitano tuliyokosa uongozi sahihi, hasara kubwa tuliyoipata kwa sekta mbalimbali. Na ikumbukwe kulikuwa na hatari ya nchi kuburutwa kwa miaka kumi, na pengine zaidi.
Jpm alitaka kututumbukiza shimoni mungu akamuwagi
 
Ndugu zangu,

Habari ndio hiyoView attachment 1774123
Ila pamoja na yote mama lazime aende taratibu na jilani zetu Kenya hao watu sio waminifu katika ujilani mwema wa kenya ni wabinafsi sana anapenda wafaidika katka uhusiano peke yao.
Wanatumia udhaifu wa watanzania katika masuala ya uchumi kuwapora na kuchukua ajira zao kiu janjaujanja, wakenya wako pamoja likija suala lakuibia Tz hamna cha Odiga au Kinyatta wote ni wale wale........So mama wetu be very conscious ukedeal nao tunaweza kuumia kama taifa.
 
Rais alisema anataka kurudisha pesa kwenye mzunguko, na watu muhimu kutimiza hilo ni wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa, Mungu amsaidie atimize lengo lake bila wapiga dili kujitokeza na kumuharibia nia yake nzuri kwa Mtanzania.
Kwaiyo mama ataku pocket pesa?

Unaamini mwanasiasa?
 
Nyie mataga wa lumumba akili zenu sawa na za popo.
Wakati jiwe anaharibu na kuyumbisha mahusiano na majirani zetu mlikuwa mnafurahia sana utadhani kinachofanyika ni jambo lenye manufaa kwa taifa.
Mkuu wewe hujui Historia. Toka kipindi cha Kikwete walikuwa wanatutenga. Mheshimiwa Kikwete ni Shahidi wa hili. Wanatusumbua sana. Magufuli alipoona Watanzania wananyanyaswa akawa anawawashia Moto. Wakizuia Maziwa ya Tanzania na yeye anazuia huku wakajua Tanzania tupo Serious na sisi. Makampuni 500 ya Kenya hayajaanza kipindi cha Magufuli yalikuwepo. Magufuli aliwashikisha Adabu, ndio maana unaona Mazungumzo yapo. Mkuu mimi nilikuwa kampuni fulani siitaji, jamaaa Wakenya Waligoma hata Contacts details ziwekwe za Tanzania wakati Kampuni ipo Tanzania. Wateja wetu walilalamika sana ila hatukuwa na namna tukanyamaza.

Kwahiyo mkuu Mmawia usilete Cheap Politics eti Magufuli aliharibu uhusiano. Uhusiano gani kama wao wanaruhusiwa kufanya biashara huku na wao wanatuzuia? Rostam Aziz katoboa Siri leo. Ndiyo wana Jamvi wengi walikuwa wanasema humu. Halafu tukumbuke Hapa Tunazungumzia Tanzania, tuwe wamoja katika hili. Mpaka wao wanafikisha Makampuni mia 500 sisi siju hata 30 hayajafika tulikuwa wapi? Tuache Unyonge watanzania. Tusimame Imara.
 
Ndugu zangu,

Habari ndio hiyoView attachment 1774123

huyu ni mafia sio wakumuani sana..
kwa nafasi alionayo, kusumbukia vibali sidhani na ukizingatia ni mtanzania mwny asili ya asia

kwa kauli yake hiyo na ya kenyatta, naona ametumika tu kama double agent ili kuwepo na stepping stone, ya namna ya kuiegeza Tanzania ifungue au iachie huru vibali kwa raia wa kenya..

ni watanzania wangapi wanaosotea vibali huko kenya, ukilinganisha na wakenya wanaohangaikia vibali Tanzania..

huyo katumika na upande ule kuibua mjadala, tusiingie force kingi. ni kama vile kenyata amemwambia mama nimekupa hili, wewe je unanipa nn kwa raia wangu kwny ishu hii?
 
Ungemsikiliza usingeandika ulichokiandika. Jifunze kupata habari kamili au kutoka kwa muhusika kabla ya kutoa maoni.
Nimemsikiliza vizuri tu kwenye ajira sisi tumenufaika kuliko wa Kenya ila kaongelea kuhusu ruhusa ya kuwekeza Kenya ni mizengwe mingi kwamba kuwa wao na makampuni 500 kwetu na sisi kuwa na 30 kwao ni ishara kwetu uwekezaji ni rahisi kuliko Kenya anaweza kuwa sawa kabisa ila kwenye ajira hapana wanafaika ni sisi. kwa upande wake yeye akiwekeza Kenya ni kinyume yeye atapata faida lakini ajira zitaenda kwa wa Kenya sio watanzania labda wachache. uwekezaji ukifanyika kwetu zaidi ni vizuri kwa Tanzania maneno aloyoongea yeye angelalamika Mkenya ningeelewa kuwa ajira zinaenda TZ.
 
Una akili ndogo sana wewe dogo,hivi "mabilionea" Mbowe na Sugu kwanini hawajaenda Kenya?
Nyie mataga wa lumumba akili zenu sawa na za popo.
Wakati jiwe anaharibu na kuyumbisha mahusiano na majirani zetu mlikuwa mnafurahia sana utadhani kinachofanyika ni jambo lenye manufaa kwa taifa.
 
Hapa Rostam nampinga kwa kiasi fulani, wajibu wa kutumia raw materials ni watanzania kuzalisha bidhaa bora ukiwa unalalamika unataka nani aje kuweka viwanda halafu kwa maneno ya Mama jana kuna wakenya wamewekeza zaidi ya kampuni 500 na kutengeneza ajira karibia alfu 56 wakati Tanzania wame invest kampuni 30 Kenya na kuzalisha ajira 2000 hivi sasa anahitaji usawa upi angekuwa specific. Kilimo tu ni ajira kubwa kwetu tukiweka nguvu za dhati katika kilimo hasa kilimo cha kisasa.
Kama tumeshindwa kuongeza thamani raw materials tulizonazo tuwaombe wakenya waje tujifunze kwao maana sisi tumejiweka dhaifu, hata mashamba ya maua kuna kipindi walikuja kulima Arusha yakawa na soko kweli wakati sisi tuliona maua nikwaajili ya nyuki tu, usagaji wa viungo na unga yaani ready to cook wameanza siku nyingi naona na sisi tumeanza kujikongoja kuiga, haya mafuta ya kupaka na kupikia pia hivyo hivyo ila hapo kwenye ubora bado hatujafikia vya kwao, pamba inatoka Tanzania inakwenda kenya kutengeneza nyuzi za sweta, carpet na mpaka shuka na blanket then tunaletewa kununua sasa wao wakenya wanakosa gani Kama wamewekeza kwenye kupata mashine za kuthaminisha raw materials hata za nje ya nchi Ili kuongeza ajira na sisi tumeng'ang'ana kujisifu na degree na kutumia miaka Mingi kukaa shule kusoma theory badala ya kukaa kwenye jamii na kutengeneza urahisi wa kupata mahitaji ya jamii Ili tupate vipato sasa tunawaonea wivu wakenya kwa nini?
 
Nina imani, nchi yetu ipo kwenye njia sahihi baada ya kupotezwa kwa miaka mitano.

Tukazanie kujenga mifumo itakayozuia Taifa kuangukia kwenye uongozi wa watu wasio na uwezo. Mifumo iwezeshe, akitokea kiongozi wa hovyo, kuwe na utaratibu rahisi wa kumwondoa.

Fikirieni miaka mitano tuliyokosa uongozi sahihi, hasara kubwa tuliyoipata kwa sekta mbalimbali. Na ikumbukwe kulikuwa na hatari ya nchi kuburutwa kwa miaka kumi, na pengine zaidi.
Sema ulipata hasara wewe. Mtu makini hawezi kuanguka kwa utawala wa aina yoyote
 
Ungemsikiliza usingeandika ulichokiandika. Jifunze kupata habari kamili au kutoka kwa muhusika kabla ya kutoa maoni.
Sisi kama nchi tunanufaika zaidi makampuni yakija kwetu kuwekeza sio makampuni yetu kwenda kuwekeza Kenya ila kuwekeza kama kutanua biashara ni vizuri kwa nchi yetu, mafanya biashara na kwa wa kenya. lakini sitaona ufahari nikiona mfano kampuni A inatoka Tanzania inaenda kuwekeza Kenya napenda kuona sio kampuni 500 waje hata 2000 ni nzuri kwa nchi japo haitakuwa nzuri kwa watu kama Rostam sababu ushindani unakuwa mkubwa. Point nakubali wapate nafasi kuwekeza kule kwa urahisi ila ajira sisi tumenufaika.
 
Sema wakenya kwenye biashara na management huwa wako smart sana.
Nimekaa huko kenya nilijifunza hao watu hawapendi kupoteza muda kabisa Kama tulivyo sisi, na silaha yao kubwa ni kutopoteza muda kabisa, hata kusali ni jumapili tu, zile ibada za Kati Kati ya wiki huko hakuna, shule form iv yupo vizuri na anakwenda chuo kikuu, kwenye kazi hakuna soga ni performance.
 
Kama tumeshindwa kuongeza thamani raw materials tulizonazo tuwaombe wakenya waje tujifunze kwao maana sisi tumejiweka dhaifu, hata mashamba ya maua kuna kipindi walikuja kulima Arusha yakawa na soko kweli wakati sisi tuliona maua nikwaajili ya nyuki tu, usagaji wa viungo na unga yaani ready to cook wameanza siku nyingi naona na sisi tumeanza kujikongoja kuiga, haya mafuta ya kupaka na kupikia pia hivyo hivyo ila hapo kwenye ubora bado hatujafikia vya kwao, pamba inatoka Tanzania inakwenda kenya kutengeneza nyuzi za sweta, carpet na mpaka shuka na blanket then tunaletewa kununua sasa wao wakenya wanakosa gani Kama wamewekeza kwenye kupata mashine za kuthaminisha raw materials hata za nje ya nchi Ili kuongeza ajira na sisi tumeng'ang'ana kujisifu na degree na kutumia miaka Mingi kukaa shule kusoma theory badala ya kukaa kwenye jamii na kutengeneza urahisi wa kupata mahitaji ya jamii Ili tupate vipato sasa tunawaonea wivu wakenya kwa nini?
Tatizo la wafanya biashara wa Tanzania hawataki ushindani wanataka kulindwa fursa ziko nyingi sana lakini hawawekezi na wakiwezeza wanafanana biashara waende kwenye mafuta, unga na juice wamemaliza sasa wajiulize hizi kampuni 500 zimekuja kufwata nini? sababu fursa nyingi kwetu tuna ardhi kubwa za kilimo tumeacha Ng'ombe tu kuwafugia. wengine kina Mo wamechukuwa mashamba makubwa kuendeleza zero wanachukulia mikopo tu. Mama afungue milango biashara waje tu ajira zitakuwa za ushindani na wakiwa wengi hata maslahi ya wafanyakazi yatapanda ifike kipindi kazi nyingi kuliko wafanyakazi.
 
Back
Top Bottom