Kenya: Rais Samia afungua kongamano la wafanyabiashara nchini Kenya, Rostam Aziz atema madini ukumbi mzima wamshangilia

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
44,323
2,000
Rais Samia amefungua kongamanano la wafanyabiashara nchini Kenya ambalo limehusisha pia wafanyabiashara kutoka Tanzania.

Rostam Aziz ametaka uwepo wa uwiano mzuri wa kibiashara kati ya Kenya na Tanzania badala ya nchi moja kuwa msambazaji wa mali ghafi na mwingine akiwa muuzaji wa finished goods, mmoja atafaidika na ajira kwa watu wake na upande mwingine ajira zitakosekana.


Tukio liko mubashara runinga ya Star.

Kazi Iendelee!
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,668
2,000
Rais alisema anataka kurudisha pesa kwenye mzunguko, na watu muhimu kutimiza hilo ni wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa, Mungu amsaidie atimize lengo lake bila wapiga dili kujitokeza na kumuharibia nia yake nzuri kwa Mtanzania.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,382
2,000
Nina imani, nchi yetu ipo kwenye njia sahihi baada ya kupotezwa kwa miaka mitano.

Tukazanie kujenga mifumo itakayozuia Taifa kuangukia kwenye uongozi wa watu wasio na uwezo. Mifumo iwezeshe, akitokea kiongozi wa hovyo, kuwe na utaratibu rahisi wa kumwondoa.

Fikirieni miaka mitano tuliyokosa uongozi sahihi, hasara kubwa tuliyoipata kwa sekta mbalimbali. Na ikumbukwe kulikuwa na hatari ya nchi kuburutwa kwa miaka kumi, na pengine zaidi.
 

Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,514
2,000
Hapa Rostam nampinga kwa kiasi fulani, wajibu wa kutumia raw materials ni watanzania kuzalisha bidhaa bora ukiwa unalalamika unataka nani aje kuweka viwanda halafu kwa maneno ya Mama jana kuna wakenya wamewekeza zaidi ya kampuni 500 na kutengeneza ajira karibia alfu 56 wakati Tanzania wame invest kampuni 30 Kenya na kuzalisha ajira 2000 hivi sasa anahitaji usawa upi angekuwa specific. Kilimo tu ni ajira kubwa kwetu tukiweka nguvu za dhati katika kilimo hasa kilimo cha kisasa.
 

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,011
2,000
Sasa huyo 'Samjo Samjo' Rostam Aziz akitema hayo Madini kwa Kuongea hivyo hapo Ukumbini Nairobi 'Practically' ina Tija ipi ( gani ) kwa Maendeleo ya Tanzania yetu hii?

Usitake tu Kutulazimisha tuseme yake.
Unataka pindi akimaliza tu kuongea uone maendeleo siyo?

Halafu unalugha chafu ya ubaguzi, sio vema mkuu
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,332
2,000
Lakini alichokisema kina hoja au hakina hoja? Usiendekeze chuki binafsi bila kudadavua mantiki ya kile alichokisema.
Kaharibu mno Uchumi wa Tanzania hasa hasa ( 2005 hadi 2015 ) kwa 'Usamjo Usamjo' wake akibebwa na Kushirikiana waliokuwa 'Maswahiba' wazuri wa Msoga na Monduli.

Naomba niishie hapa tafadhali nisije kusema mengineyo yasiyo na Faida sasa Kwako ( Kwenu ) kuyajua.

Akhsanteni.
 

Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
2,077
2,000
Hapa Rostam nampinga kwa kiasi fulani, wajibu wa kutumia raw materials ni watanzania kuzalisha bidhaa bora ukiwa unalalamika unataka nani aje kuweka viwanda halafu kwa maneno ya Mama jana kuna wakenya wamewekeza zaidi ya kampuni 500 na kutengeneza ajira karibia alfu 56 wakati Tanzania wame invest kampuni 30 Kenya na kuzalisha ajira 2000 hivi sasa anahitaji usawa upi angekuwa specific. Kilimo tu ni ajira kubwa kwetu tukiweka nguvu za dhati katika kilimo hasa kilimo cha kisasa.
Haueleweki, Unaweza kuwa na hoja nzuri sana, ila unashindwa kuwakilisha hapa.
 

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,181
2,000
Meko si alikua anakimbiza investors hapo Tz.

Sasa hizo processing industries zingejengwa na nani?

Lile nyangumi bora halipo kabisa.

Bila ya kuvutia wawekezaji seriously tutaendelea kuuza raw materials tu.
Hayati alijenga mazingira wezeshi ya ukuzaji wa biashara. Kufufua reli iliyokufa zaidi ya miaka 25 ni ujenzi wa mazingira ya usafirishaji ambayo ni nyenzo muhimu kibiashara.

Ufufuaji wa shirika la ndege ni urahisishaji wa biashara kimataifa. Kama sio corona muda huu Air Tanzania ingekuwa kila wiki inakwenda China na kurudi kupeleka matikiti. Kama sio corona muda huu biashara ya maua ya Arusha ingeitumia sana Air Tanzania kuyapeleka Amsterdam na kwingineko.

Hayati hakutaka dharau kama zile za kipindi kile mamlaka ya anga ya Kenya kuzuia ndege zetu kisa corona halafu kukubali ziingie kwao ndege za US na UK ambako ugonjwa ulikuwa umepamba moto. Dharau ile ilijibiwa vizuri sana na TCAA kwa kuzuia ndege zao zisiingie nchini.

Tufanye biashara pamoja kwa kila hali lakini tuheshimiane, tusileteane dharau za kutaka kuburuzana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom