Kenneth Kaunda afariki dunia akiwa na miaka 97

Kweli mashujaa wameisha
Walipigania haswa Africa na wananchi kwa ujumla
Tutawakumbuka daima
Pumzika KK
Hapo ndio umoja ulikuwa wa kweli
Na kulikuwa hakuna ubaguzi

IMG_1295.jpg

IMG_1294.jpg
 
Bila shaka ndio muasisi wa “Kaunda suits”
Kabisa na Mchonga alizifaidi hasa,iikichakaa tu kidogo anapiga
"ə bana kaunda suti hizi sio imara bana ishachanika"
Kaunda "imeisha hiyo nakuletea 2 mpya bure usimshtue Nkurumah km zilichanika "
Mchonga "Aah bro skuangushi hata kupiga ni sababu tu naenda kikao UNO"
Kaunda-poa

Mchonga huku-Yes 👊🕺suti 2kaunda buree
Story tu kijijini hizi inasemekana 👊
 
Aliyewahi kuwa Rais wa kwanza na baba wa taifa wa Zambia Dk. Keneth Kaunda amefariki usiku huu akiwa na umri wa miaka 97. Taarifa zaidi zaidi zitakujia badae.

R. I. P Daktari
 
Kwani mchana ulikuwa wapi ?
Mbona tuna taarifa hii tangu mchana uliopita!
 
Hata uwanja wa Mabingwa wa Kihistoria (TM) unaitwa Uwanja wa Kaunda kwa heshima yake.
 
Mzee Kennedy Kaunda amefariki mchana wa leo wakati akipatiwa matibabu kwenye hospital ya Maina
View attachment 1821814View attachment 1821815View attachment 1821816View attachment 1821817
=====

MAISHA YA AWALI

Kaunda ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanane. Alizaliwa katika hospitali ya Misheni ya Lubwa katika kitongoji cha Chinsali, katika Mkoa wa Magharibi mwa Northern Rhodesia, sasa hivi Zambia.

Baba yake alikuwa akiitwa David Kaunda, alikuwa kiongozi wa Kanisa la Kiskoti na mwalimu wa shule za wamisionari, ambaye alizaliwa nchini Malawi na kuhamia Chinsali kwa lengo la kufanya kazi katika Lubwa Mission.

Alianza masomo kadhaa katika Munali Training Centre ya mjini Lusaka (kunako Agosti 1941–1943).

Kaunda pia aliwahi kuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi na bweni ya Upper Primary School kuanzia mwaka wa 1943 hadi 1945. Alianza kazi ya ualimu huko Lubwa na kuelea zake mjini Lusaka kwa lengo la kuwa mwelekezi wa jeshi, lakini kwa kazi hiyo ilikwisha.

Kuna kipindi alikuwa akifanya kazi katika Migodi ya Salisbury na Bindura. Mnamo mwaka wa 1948, akawa mwalimu katika shule ya mjini Mufulira kwa ajili ya United Missions to the Copperbelt (UMCB). Pia aliwahi kuwa msaidizi katika Kituo cha Ustawi wa Jamii wa Afrika na Bodi ya Walimu wa Shule ya Mine School ya mjini Mufulira.

Kenneth David Kaunda alikuwa Rais wa kwanza wa nchi ya Zambia. Alitumikia taifa hilo kuanzia mwaka wa 1964 hadi 1991.

Rais wa zamani wa Zambia Kenneth Kaunda mwenye umri wa miaka 97 alikuwa anapewa matibabu ya ugonjwa ambao haukutajwa, kwenye hospitali ya kijeshi ya mjini Lusaka, ofisi yake ilisema Jumatatu 14 Juni, 2021.

Kaunda aliiongoza Zambia tangu mwaka 1964 wakati taifa hilo la kusini mwa Afrika lilipojipatia uhuru, hadi mwaka 1991. Ni miongoni mwa mashujaa wachache walioshiriki kuikomboa Afrika.

Ni Baba wa Taifa la Zambia
Umetupa wasifu wake wa kielimu na kazi za kitaaluma alizofanya lakini hujatuambia namna alivyopanda kisiasa hadi kuwa Rais,tupe wasifu wa harakati zake za kisiasa.R.I.P legandary
 
ameona wajukuu na vitukuu na vilembwe, mungu ni mwema sana.
Watu wenye mioyo safi waliompa Yesu maisha yao ndio wanaishi hivi.
 
Nimetamani kupaelewa hapa lakini nimeshindwa, Msaada tafadhali
Tafriri isiyo rasmi,kwamba wakati washindani wakiwa kwenye harakati za kumzuia kugombea awamu nyingine madarakani( to usher him away from the podium) baada ya kipindi chake cha uongozi kilichokuwa kimejaa migawanyiko( to ran over allotted time) aliangua vicheko kwa kejeli na kuwaambia wanajaribu kumdhibiti mzee aliyethubutu na kumudu kupambana na Boers/Africaners(Wazungu wa Afika Kusini ambao ni vitukuu au vizazi vya wahamiaji wakulima wa kilowezi kutoka Uholanzi-Dutch Settlers)
 
Mungu akubariki sana ndugu
 
Back
Top Bottom