Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,499
- 86,037
Mzee Kennedy Kaunda amefariki mchana wa leo wakati akipatiwa matibabu kwenye hospital ya Maina
=====
MAISHA YA AWALI
Kaunda ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanane. Alizaliwa katika hospitali ya Misheni ya Lubwa katika kitongoji cha Chinsali, katika Mkoa wa Magharibi mwa Northern Rhodesia, sasa hivi Zambia.
Baba yake alikuwa akiitwa David Kaunda, alikuwa kiongozi wa Kanisa la Kiskoti na mwalimu wa shule za wamisionari, ambaye alizaliwa nchini Malawi na kuhamia Chinsali kwa lengo la kufanya kazi katika Lubwa Mission.
Alianza masomo kadhaa katika Munali Training Centre ya mjini Lusaka (kunako Agosti 1941–1943).
Kaunda pia aliwahi kuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi na bweni ya Upper Primary School kuanzia mwaka wa 1943 hadi 1945. Alianza kazi ya ualimu huko Lubwa na kuelea zake mjini Lusaka kwa lengo la kuwa mwelekezi wa jeshi, lakini kwa kazi hiyo ilikwisha.
Kuna kipindi alikuwa akifanya kazi katika Migodi ya Salisbury na Bindura. Mnamo mwaka wa 1948, akawa mwalimu katika shule ya mjini Mufulira kwa ajili ya United Missions to the Copperbelt (UMCB). Pia aliwahi kuwa msaidizi katika Kituo cha Ustawi wa Jamii wa Afrika na Bodi ya Walimu wa Shule ya Mine School ya mjini Mufulira.
Kenneth David Kaunda alikuwa Rais wa kwanza wa nchi ya Zambia. Alitumikia taifa hilo kuanzia mwaka wa 1964 hadi 1991.
Rais wa zamani wa Zambia Kenneth Kaunda mwenye umri wa miaka 97 alikuwa anapewa matibabu ya ugonjwa ambao haukutajwa, kwenye hospitali ya kijeshi ya mjini Lusaka, ofisi yake ilisema Jumatatu 14 Juni, 2021.
Kaunda aliiongoza Zambia tangu mwaka 1964 wakati taifa hilo la kusini mwa Afrika lilipojipatia uhuru, hadi mwaka 1991. Ni miongoni mwa mashujaa wachache walioshiriki kuikomboa Afrika.
Ni Baba wa Taifa la Zambia.
Zaidi kuhusu Kaunda soma:
1). Mjue Hayati Kenneth Kaunda