Ukishaamini hivyo ujue wewe una kasoro na yawezekana ukionja utabaka mpaka kuku au mtoto wako. Watu kabla ya hizi dini mila zetu zilikuwa zinafuata mfumo huu wa kulipa mahali kwa pombe na mifugo, kuzika kwa kunywa pombe na shughuli nyingine, mtoto akizaliwa ni pombe na sherehe. Dini haikuja kuvunja mila za watu na ndiyo maana ukiona dini inavunja mila zako hiyo ikimbie. Yesu basi si Yesu unayemwabudu maana angeanzisha amri zake. Amri kuu alitupa Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuongelea mambo ya pombe katu. Sigara na pombe kipi ni hatari kwa afya yako?