Kwanza kwenye amri kumi hakuna inayokataza pombe. Hawa ni watawa ambao kwenye nadhiri zao hakuna kifungu kinasema wasinywe pombe ila wamefunga nadhiri za useja, umaskini na wito. Wakatoliki tunaruhusiwa kunywa hata sherehe zetu zote au shughuli zetu zote dunia nzima hazikosi mvinyo. Yesu alitengeneza mvinyo kama muujiza wake wa kwanza pale Kaanani sasa wewe unatwambia nini?
Mimi naona usipeleke watoto wako huko kwenye shule za kikatoliki, wapeleke kwenye shule za kiislam maana hao ndo pombe ni haram. Tukae tufuatilie wote ni kipindi kipi baa huwa zinakosa wateja je ni kwaresima au Ramadhan?