Kazi iendelee na safari iendelee, tutafika tu. Ni wapi na kwa namna gani, tutakomaa tu!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Katika pita pita yangu humu JF nimekutana na huu mjadala kati ya ninaoamini ni watetezi wakubwa wa kazi iendelee na wana CCM kindaki ndaki.

A: Kazi iendelee, Shaka apewe Urais tu!
B: Bado hajakomaa vizuri...
C: Atakomaa huko huko!

Nakiri sikushangaa hata kidogo. Huwezi ukapanda mchicha ukavuna nyanya. CCM wamewekeza kweli kweli kwa Watanzania dizaini hii, wametamalaki!

Wako safarini lakini hawajui wanatoka wapi wanaelekea wapi na kwa kutumia usafiri upi. Watajua huko huko mbele ya safari, kazi iendelee na safari iendelee!

Kila baada ya miaka mitano wanamuongezea kiongozi wao mingine mitano. Na Ikitokea bahati mbaya asiwepo, hamna tabu, wanamrithisha msaidizi wake.

Wamejiaminisha kuwa hata miaka mia ipite ni wao tu watabaki usukani iwe kihalali au kiharamu. Ole wako ujenge kusudio la kuwapokonya usukani, utajuta!

Tanzania, Tanzania Nakupenda kwa moyo wote.

Nchi yangu Tanzania, Jina lako ni tamu sana.
Nilalapo nakuota wewe Niamkapo ni heri mama wee.

CCM imepewa muda mrefu na umetosha
 
Back
Top Bottom