TAMISEMI: Katika kipindi cha 2015 hadi 2023 kuna ongezeko la jumla ya vituo vya huduma za afya ya msingi 1,867

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Ofisi ya Rais - TAMISEMI) ina jukumu la kusimamia Tawala za Mikoa; Tawala za Serikali za Mitaa; Uratibu wa Huduma za jamii Vijijini na Mijini kama vile Usafiri, Afya, Maji na Usafi wa Mazingira; Tume ya Utumishi wa Walimu; Utambuzi na Maendeleo ya Wajasiriamali na Wafanyabiashara Wadogo; Utambuzi na Maendeleo ya Vipaji; Tawala za ElimuMsingi na Sekondari; Uboreshaji wa utendaji na maendeleo ya rasilimali watu; na Idara za Serikali, Mashirika ya Umma, Wakala, Programu na Miradi iliyo chini ya Ofisi hii.

TAMISEMI imetoa Takwimu za Mafanikio na maendeleo ya huduma za afya ya msingi kwa mwaka 2020/2021 hadi 2022/2023

1. Katika kipindi cha 2015 hadi 2023 kuna ongezeko la jumla ya vituo vya huduma za afya ya msingi 1,867;

2. Zahanati zimeongezeka kutoka 4,127 mwaka 2015 hadi kufikia Zahanati 5,646 Septemba 2023;

3. Vituo vya afya vilivyosajiliwa na kuanza kutoa huduma vimeongezeka kutoka 535 mwaka 2015 hadi 788 mwaka 2023;

4. Vituo vinavyotoa huduma za Upasuaji vimeongezeka kutoka Vituo 115 mwaka 2015 kufikia vituo vya afya 537 Septemba 2023;

5. Katika Kipindi cha mwaka 2021/22 na 2022/23 pekee zimejengwa Zahanati 999

6. Hospitali za halmashauri zilizoanza kutoa huduma zimefikia 172 kutoka 77 mwaka 2015

7. Kuongezeka huduma za uchunguzi wa mionzi katika vituo 169
8. Kusimikwa mitambo 21 ya kuzalisha hewa tiba ya oxygen

9. Ujenzi wa majengo ya dharura 83 ambapo tayari hospitali 59 zimeanza kutoa huduma za dharura (Emergency medicine).

Chanzo: OFISI YA TAWALA ZA MIKOA NA RAIS SERIKALI ZA MITAA
 
Akija mwingine utasikia anatoa data tofauti na hizo. Ogopa sana serekali za wapika data.
 
Takwimu hizi Huwa hazina ukweli, ni Bora wawe wanaorodhesha majina ya vituo, mtaa, kata, wilaya na hata Mkoa vilipo Ili raia wajionee km ni kweli au la
 
Back
Top Bottom