Kati ya AZAM na STAR TIMES, ipi itakayowafaa wazee wangu kijijini?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Si mpenzi wa mpira wala vipindi vinavyofanania mpira, n.k., labda wajukuu wake, lakini siweki kwa ajili yao ila bibi yao.

Mlengwa anapendelea vipindi vya kwaya na mahubiri ya Kiswahili na "movies" zenye maudhui ya Kiafrika, hasa ya Kitanzania, lakini zinazozingatia maadili .

Nilishajaribu ZUKU lakini hawajakidhi vigezo. Ninataka nichukue mojawapo kati ya AZAM na STAR TIMES. Ni ipi kati ya hizo mbili ina vipindi vingi vinavyohitajiwa na mlengwa?

Kumbuka, kipaumbele ni GOSPEL SONGS, MAHUBIRI YA KISWAHILI na MOVIES za Kiafrika, lakini hasa hasa, za Kitanzania, kwa ajili ya urahisi wa kuzielewa (za lugha ya Kiswahili). King'amuzi ipi itakayomfaa?

Nashukuru🙏🙏🙏

••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
MREJESHO: Nilichukua AZAM. Ikiwa ni mwezi mmoja sasa tokea ianze kutumika, nimeridhika kuwa lilikuwa ni chaguo sahihi. Nawashukuruni wote kwa ushauri wenu🙏🙏🙏
 
Nikuambie tu ukweli Mkuu,

Wewe ni Mkristo bila shaka. Chukua StarTimes.

Azam imejaza Channel nyingi zenye maudhui ya Kiislamu. Hata movie nyingi zina lengo haswa la kueneza Uislamu.

Ambacho Azam wanakimudu vizuri ni mambo ya Soka la Bongo tu.

Startimes wana Channel za kila aina.
Wana Upendo TV, muda mwingi ni Injili na nyimbo za kuabudu na sifa. Channel za Kikristo zipo nyingi mno.

Kama mpira si sehemu ya wanachopenda wazee, opt for Startimes. Bei chee, mzigo mwingi.
 
Nashukuru sana mkuu, ila nimeamua kuchukua AZAM kwa sababu zifuatazo:
1. Ina channel nyingi ambazo huenda zitampendeza mlengwa. Nafikiri hata UPENDO TV inaptikana kwenye kisimbusi cha AZAM.

2. Wajukuu zake wasipate shida pindi wanapomtembelea, hasa ukizingatia kuwa wengi wao wanapendelea mpira.
 
Nikuambie tu ukweli Mkuu,

Wewe ni Mkristo bila shaka. Chukua StarTimes.

Azam imejaza Channel nyingi zenye maudhui ya Kiislamu. Hata movie nyingi zina lengo haswa la kueneza Uislamu.

Ambacho Azam wanakimudu vizuri ni mambo ya Soka la Bongo tu.

Startimes wana Channel za kila aina.
Wana Upendo TV, muda mwingi ni Injili na nyimbo za kuabudu na sifa. Channel za Kikristo zipo nyingi mno.

Kama mpira si sehemu ya wanachopenda wazee, opt for Startimes. Bei chee, mzigo mwingi.
Hata azam kuna Channel za kikristo pia Acha chuki za kidini had unaandika pointless kama mtu ambae hujawahi kumiliki akili hata moja
 
Peleka star times yenye local channel za maana nyingi bure wazee waka enjoy taarifa za habari bure mwaka mzima. Hao wengine local channel ya bure ya maana ni moja tu zingine zote ni za kulipia hakuna kifurushi cha bure
 
Wakuu, nashukuruni, mmenirahisishia. Nitamchukulia AZAM.

Nashukuruni sana , tena sana
Tena kama anampenda Mwampoza kuna mahubiri live... Niliwahi pata mgeni siku moja home kwangu kumbe ni muumini mzuri wa Mwamposa, aisee ilibidi tumuachie TV peke yake maana muda wote ni channel ya mwamposa, ambayo hata sisi wenyeji tulikuwa hatuijui
 
Back
Top Bottom