Ipi tofauti kati ya Suluhu na Sare?

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Kuna watu huwa wanachanganya sana haya maneno. Kwamba ni ipi tofauti ya maneno Suluhu na Sare?

Kwa mujibu wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Maneno yote haya mawili yanazungumzia matokeo katika mchezo ambayo ni ya bila kuzidiana, matokeo ambayo ni sawa. Yaani, timu moja na nyingine kuwa na nguvu sawa, kama ambavyo tumekuwa tukisema katika mchezo wa mpira wa miguu.

Hata hivyo, kuna tofauti ya msingi kati ya Suluhu na Sare. Suluhu ni matokeo ya sare ambayo hakuna timu iliyopata magoli. Mchezo ambao timu zimetoka Suluhu ni ule ambao matokeo yake ni sifuri kwa sifuri au bila kwa bila (0-0).
Matokeo ya Sare kwa upande wake licha ya kubeba maana ya bila kwa bila lakini ni matokeo ambayo pia yanahusisha kufungana magoli yenye idadi sawa kama vile 2-2, 3-3, 1-1 n.k.

Hivyo, tunaposema timu zimetoka Suluhu tumaanishe matokeo ya mcheo wao ni bila kwa bila (0-0). Aidha, tunaposema timu fulani zimetoka sare tumaanishe kuwa timu hizo ama zimetoka Suluhu au zimefungana idadi fulani ya magoli ambayo ni sawa kwa kila upande.

Mifano ya matumizi inaweza kuwa, ‘Jana timu ya Zimamoto na Majimoto zilitoka Suluhu (0-0) au ‘Jana timu ya Zimamoto na Majimoto zilitoka Sare (0-0, 2-2, 3-3,1-1 n.k).
 
Kamuulize Sare.
 
1)Umesema kwa BAKITA wanachukulia kuwa ni kutokuzidiana

2)Unavyosema kimsingi unamaanisha nini? Ni taasisi nyingine hiyo kimsingi?
 
Suluhu ni kukubaliana kuwa yaishe tunalingana, sare ni kuwa hata kama hatukubaliani bado tuko sawa. Mwisho wa yote ni kuwa yote yana maana ya kuwa sawa
 
Back
Top Bottom