Kassim Majaliwa: Watanzania tufanye maamuzi ya kuingia kwenye kilimo na mifugo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,818
4,569
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuingia na kubobea kwenye kilimo, mifugo na uvuvi, akisema kuwa hilo ndilo eneo litakaoleta uchumi wa mtu mmoja mmoja na wananchi wote kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa jana Agosti 3, 2023 baada ya kukagua mabanda ya maonesho ya nanenane kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, ambapo ameongeza kuwa ilani ya Chama cha Mapindunzi (CCM), imeagiza Serikali kuhakikisha inafanya kila namna ili kila Mtanzania akingie sekta ya uzalishaji kisha aamua kuzalisha ama kwa matumizi yake au kibishara.
 
Tatizo Majaliwa hatuelewi nyie viongozi mnatakia nini hii nchi. Leo unahamasisha tulime kwa gharama kubwa kesho unanipangia bei ya kuuza mazao yangu. Leo napanga kufuga huku nikipigia mahesabu pumba debe moja elfu mbili, namalizia kujenga mabanda tu pumba debe elfu sita. Kweli hapo moyo wa kufuga upo tena. Laiti wakulima na wafugaji wangekuwa wanapiga mahesabu ya gharama za kilimo na ufugaji sidhani kama wangefuga au kulima
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuingia na kubobea kwenye kilimo, mifugo na uvuvi, akisema kuwa hilo ndilo eneo litakaoleta uchumi wa mtu mmoja mmoja na wananchi wote kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa jana Agosti 3, 2023 baada ya kukagua mabanda ya maonesho ya nanenane kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, ambapo ameongeza kuwa ilani ya Chama cha Mapindunzi (CCM), imeagiza Serikali kuhakikisha inafanya kila namna ili kila Mtanzania akingie sekta ya uzalishaji kisha aamua kuzalisha ama kwa matumizi yake au kibishara.
Namuomba waziri mkuu atenge fungu kwa ajili ya uchimbaji wa visima vya maji kwa ajili ya umwagiliaji.pia ikiwezekana hata mabwawa yachimbwe kwa wingi .mbona maeneo mengi hapa Tanzania maji yapo karibu ni jambo la kuamua na kutenda tu.
 
Stori zilezile za
Siasa ni kilimo
Kilimo cha kufa na kupona
Kilimo ni uti wa mgongo
Kilimo kwanza

Tukaja viwanda kwanza
Waziri mkuu anasema turudi kwenye kilimo.

Maneno meengi kwa miaka 60, utekelezaji Sifuri.
CCM ni chama cha Propaganda. Wao kazi yao ni kusema tu...... Mayendo zero. Yeye pamoja na kuiba kote huko bado wameshindwa kuwekeza kwenye kilimo. Nategemea wa kulima wadogo wadogo ndiyo wafanye hivyo.

Kunhekuwa na term limits kwenye Ubunge, labda hawa watu wangepata akili ya kuwekeza. Lakini kwa vile maisha yao wamezoea kuchuma kwenye shamba la bibi kwa mikataba fake wanajisahau.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuingia na kubobea kwenye kilimo, mifugo na uvuvi, akisema kuwa hilo ndilo eneo litakaoleta uchumi wa mtu mmoja mmoja na wananchi wote kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa jana Agosti 3, 2023 baada ya kukagua mabanda ya maonesho ya nanenane kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, ambapo ameongeza kuwa ilani ya Chama cha Mapindunzi (CCM), imeagiza Serikali kuhakikisha inafanya kila namna ili kila Mtanzania akingie sekta ya uzalishaji kisha aamua kuzalisha ama kwa matumizi yake au kibishara.
Ni yale yale kuww kilimao ni uti wa mgongo wa taifa , halafu kwa nyuma watu wanaiba madini ,safari hii ni DP
 
Aje hapa yule jamaa alikuwa anataka serikali ifunge masoko ya nje ili mazao yashuke bei,yeye ale ubwabwa wa bei nafuu.
 
Aachie uwaziri mkuu aingie yeye kwenye mifugo awe mfano

Ova
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuingia na kubobea kwenye kilimo, mifugo na uvuvi, akisema kuwa hilo ndilo eneo litakaoleta uchumi wa mtu mmoja mmoja na wananchi wote kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa jana Agosti 3, 2023 baada ya kukagua mabanda ya maonesho ya nanenane kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, ambapo ameongeza kuwa ilani ya Chama cha Mapindunzi (CCM), imeagiza Serikali kuhakikisha inafanya kila namna ili kila Mtanzania akingie sekta ya uzalishaji kisha aamua kuzalisha ama kwa matumizi yake au kibishara.
Hii kauli inatakiwa iendane na mfumo wa Elimu na Maisha yetu , ambayo yanatakiwa kuanzia kwenye ngazi ya chini yaani kifamilia, shuleni na kwenda juu. Lakini Kwa miaka Mingi toka alivyo ngatuka Nyerere tumekuwa na Sera za uchuuzi, mishenit town , kuajiriwa nk , sasa inabidi kizazi cha sasa waanze kufundishwa toka utotoni haya mambo na viongozi hasa wa siasa waache upigaji na kusema uongo . Ili watoto waone kweli uongo haufai
 
Stori zilezile za
Siasa ni kilimo
Kilimo cha kufa na kupona
Kilimo ni uti wa mgongo
Kilimo kwanza

Tukaja viwanda kwanza
Waziri mkuu anasema turudi kwenye kilimo.

Maneno meengi kwa miaka 60, utekelezaji Sifuri.
Unafuga au unalima nini, ambacho hakijawa na manufaa kwako?
 
Hii kauli inatakiwa iendane na mfumo wa Elimu na Maisha yetu , ambayo yanatakiwa kuanzia kwenye ngazi ya chini yaani kifamilia, shuleni na kwenda juu. Lakini Kwa miaka Mingi toka alivyo ngatuka Nyerere tumekuwa na Sera za uchuuzi, mishenit town , kuajiriwa nk , sasa inabidi kizazi cha sasa waanze kufundishwa toka utotoni haya mambo na viongozi hasa wa siasa waache upigaji na kusema uongo . Ili watoto waone kweli uongo haufai
Hizo ni sera zako binafsi. Kama hazijakusaidia miaka yote anza japo kufuga kuku wa kitoweo.
 
Back
Top Bottom