Mbeya: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa wito kwa Taasisi za fedha kusaidia wakulima

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
207
453
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa taasisi za fedha nchini kuendelea kubuni huduma zinazolenga kutatua changamoto zinazowagusa wakulima, huku akionesha kuguswa zaidi na hatua ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kuwekeza nguvu zaidi kwenye utoaji wa mikopo ya zana za kilimo kwa wakulima nchini.

‘’Siku zote serikali imekuwa ikisisitiza na kuziomba taasisi mbalimbali za kibenki kuongeza juhudi kwenye ubunifu wa huduma zake ili zije na huduma zinazoonekana kutatua kero za makundi mbalimbali kulingana na mahitaji yao mahususi. Na hii ndio sababu nawapongeza benki ya NBC ambapo kupitia mkakati wa NBC Shambani wanaweza kuwasaidia wakulima wengi kupata mikopo ya zana muhimu za kilimo…hongereni sana

NBC,’’ - amesema Waziri Kassim Majaliwa alipotembebelea banda la NBC lililopo kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya John Mwakangale mjini Mbeya.

Amesema utoaji wa mikopo yenye riba nafuu kwa zana za kilimo utasadia kuchochea mapinduzi ya kilimo kwa kuchochea kasi ya uzalishaji na ongezeko la mapato kwa wakulima.

Awali akifafanua kuhusu mikopo hiyo Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, riba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Raymond Urassa alisema kupitia ushirikiano na kampuni ya kuuza pembejeo za kilimo ya Agricom Africa benki hiyo tayari imefanikiwa kutoa mikopo ya zana za kilimo zenye thamani ya shilingi bilioni 2.3 kwa wakulima mbalimbali nchini.

“NBC itaendelea kuunga mkono kwa vitendo dhamira ya serikali inayolenga kufanikisha ukuaji wa sekta ya kilimo kutoka asilimia 5 hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2030’’ amesema Urassa huku akiwakaribisha wakulima kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo ya zana za kilimo sambamba na kufungua akaunti ya NBC Shambani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Agricom, Alex Duffar ameishukuru NBC, huku akibainisha kuwa katika kipindi kifupi cha ushirikiano na benki hiyo kampuni hiyo imefanikiwa kuchochea mauzo yake mara 10 zaidi ya mwaka jana

Sources via Azam Tv
 
Back
Top Bottom