Majaliwa ziarani Russia na maamuzi ya Rais Samia kuficha aibu ya kuitikia mwito wa Putin.

Steven Joel Ntamusano

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
2,948
1,988
Afrika ni bara tajiri sana. Hilo halina ubishi, wasomi wetu wengi wanakuja na ushahidi wa kila namna unaoshihirisha namna bara hili lilivyobarikiwa. Kuanzia juu kabisa kule Morocco mpaka Afrika ya Kusini pote huko kumejaa mali nyingi zilizo chini ya ardhi.

Uranium inayopatikana nchini Niger ndio chanzo cha umeme wa Ufaransa, wakati nchi hiyo nzima ya Ulaya ina umeme tena wa miaka na miaka huko Niger wanapotoa chanzo chao cha umeme walio na nishati hiyo hawafiki hata asilimia 60 ya wakazi wa nchi hiyo!.

Madini kama Nickel na mengine mengi yamejaa katika kila kitongoji cha Afrika, kila kukicha zinakuja taarifa za madini mapya yaliyovumbuliwa sehemu fulani ya bara hili. Na wazungu wanajua watukamatie wapi tusikurupuke kabisa. Kila siku ni habari za misaada zisizokwisha.

Kila siku wanaibuka vikaragosi wapya wa wazungu kwenye kila sekta ya nchi za afrika, hawa wanakuwa chanzo cha umaskini wetu wa kudumu. Tunapopigana wao wanajichotea kiulaini tu mali zetu za kila aina. Wanajua tukitulia na kuishi kwa amani hata hatuwahitaji wao katika shughuli za kiuchumi zenye maslahi mapana ya bara zima.

Utajiri wa asili tulionao ni mwingi mno kiasi cha kukosa hata huo muda wa kujenga urafiki na watu wa mabara mengine. Tunao uwezo wa kufanya biashara na kuishi vyema kwa muingiliano wa sisi kwa sisi wa rasilimali bila hata kuvuka ile bahari ya Mediterranean kwenda kuomba chochote kitu kwa wazungu.

Hivi karibuni kulifanyika kikao kikubwa kule Moscow Russia kati ya Rais Putin na baadhi ya marais wa Afrika, na wakawa kama vile wanawashtakia Wamarekani na Magharibi kwa Vladmir Putin anayesumbua nao kila uchao.
Nilielewa ni kwanini Rais Samia hakutaka kuhudhuria kikao hicho cha Russia na badala yake akamtuma Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amuwakilishe.

Uso umeumbwa na aibu, hakutaka aonekane ni sehemu ya wagomvi wapya wa magharibi na Marekani wakati mwezi mmoja kabla alipewa msaada mkubwa na EU na picha za ukumbusho zikapigwa!.

Uso umeumbwa na aibu, Mheshimiwa Samia hakutaka kuwakera wazungu wa magharibi baada ya kufanya maamuzi kadhaa ya kuwaridhisha ikiwepo kumuachia huru Freeman Mbowe na kuruhusu siasa ya vyama vingi ifanyike kwa uhuru na uwazi.

Kuwepo kwa PM Majaliwa kule mkutanoni Russia ni kujaribu kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Kwamba Samia anaonekana machoni mwa dunia ya magharibi kuwa hana ubaya wa moja kwa moja ndio maana akamtuma waziri mkuu wake na pili ni huyo huyo aliyetumwa kufanya kazi ya kutafuta wawekezaji wapya huko Russia.

Ukiangalia ugumu wa maamuzi ya rais ya kumtuma waziri mkuu wake huko Russia unaweza kuelewa kwa mapana ile kazi ya umoja uliokuwa na nguvu sana kipindi cha Mwalimu Julius Nyerere akiwa rais, wakati wa awamu ya kwanza na mpaka alipostaafu.

Umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote ulikuwa na mashiko miaka ile ya vita baridi kati ya Marekani ya Hayati Ronald Reagan na Russia ya Hayati Mikhail Gorbachov. Ni umoja wenye kila sababu ya kufufuliwa upya wakati wa vita mpya ya baridi inayoweza kuwa ya moto wakati wowote ule kuanzia sasa.

Russia ya Putin haina amani na USA ya Biden na hivyo ni muda muafaka wa kuwepo chombo cha kimataifa kinachosimama katikati ya pande hizi mbili zenye kuishi kwa uhasama.

Binafsi nimeelewa kwanini Samia aliamua kumtuma PM Majaliwa kule Russia, ni kujaribu kuwafikisha ujumbe magharibi kwamba yupo pamoja nao. Hakutaka kupigwa picha na kuchukuliwa na kamera za video akiwa sehemu ya picha ya marais inayopigwa kwenye ngazi za jengo la mkutano wakati miezi michache kabla ametoka kupokea pesa nzito kutoka kwa taasisi ya EU.
 
Watu huwa mnajiandikia.
Samia angeendaje kule wakati alikuwa na ugeni hapa nyumbani.

Kitenfo cha waziri mkuu kwenda ni sawa naye kuhudhuria
 
Hii sera haitotulipa......
Wazungu sio wapumbavu wanaona tunachofanya pia, If ni West tuwe west if ni East tuwe full East.
U ndumilakuwili utatuacha Nyuma wakati wenzetu wanakimbia.
Pamoja na kuwa mimi sio mtaalamu wa Siasa, lakini naona kabisa kuna jambo linaendelea Duniani hapa.
Lilianzia Kwenye Arab Springs likaja Syria, likaja Ukraine na Sasa Linasambaa kwa kasi Afrika.
Naamini viongozi wa Kitaifa wanaliona hili pia, na wataelewa Upepo unavuma wapi saiv.
Ila najua kwa kinachoendelea Angekuwepo Magu, tungeenda East.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom