Rais Samia: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yupo kwenye "Mchezo wa kutunzwa" maendeleo, tutamtunza

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,225
103,846
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ‘Mcheza kwao hutunzwa’ hivyo ni lazima Serikali ipeleke maendeleo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi ili kumtunza kwa maendeleo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo kwakuwa kazi yake ya kuwatumikia Watanzania ni kubwa hivyo Serikali ni lazima ihakikishe nyumbani kwake kunakaa sawasawa.

Akiongea na Wananchi wa Ruangwa leo Sept 18,2023 kwenye mkutano wa hadhara Ruangwa Mjini, Rais Samia amesema “Waswahili wanasema ‘Mcheza kwao hutunzwa’ kwanini tusimtunze Waziri Mkuu kwa maendeleo!?, lazima Serikali tumtunze Waziri Mkuu kwa maendeleo, Wadhifa wake ni Mkubwa kazi yake ni kubwa ya kushughulikia Tanzania nzima ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi ni kubwa mno lazima tuangalie nyumbani kunakaa sawasawa lazima tulete maendeleo Ruangwa”

“Ruangwa ina fursa nyingi za kiuchumi yamesemwa hapa kilimo, madini, uvuvi, utalii, gesi na misitu mikubwa ya Lindi, kwa mambo yote haya ni lazima maendeleo yapatikane, Mungu ameumba Ruangwa na Mkoa wa Lindi na rasilimali zote hizi kama hazikuleta maendeleo sisi Viongozi tunapata dhambi, zimeumbwa ili zilete maendeleo na tutazitumia kuleta maendeleo ya Mkoa na Wilaya ya Ruangwa”

“Mwaka huu bei ya ufuta na mbaazi ni nzuri lakini Waziri wangu huyu halali anahangaika kuipandisha bei ya korosho”

My Take
Labda tuna laana ya kukosa viongozi wenye vision.
 
Viongozi ni binadamu....

Tulimtunza UWANJA WA NDEGE WA CHATO hayati JPM ....

Kwanini tusipeleke maendeleo RUANGWA nao ni wananchi....wana haki kama wengine na pia ni nyumbani kwa PM anayekesha kulijenga taifa hili ?!!!

Tuache unafiki
 
Back
Top Bottom