Mbunge Edward Lekaita asisitiza Serikali kuwekeza kwenye Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambako kuna Watanzania wengi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
"Tunataka Utekelezaji wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2024-2025 uelekezwe Vijijini, watanzania walio wengi wako Vijijini, Mpango uende kwenye Maendeleo ya Vijijini (Rural Developments)" - Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto​

"Taarifa ya Serikali inaonyesha mikopo Trilioni 22 ni ya Biashara lakini asilimia 7 tu ndiyo imeelekezwa kwenye Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Hii haiwezekani, ni lazima tuwekeze sana huko kwasababu ndiyo watanzania wengi wapo huko, tuwe na Mipango inayoenda na watu wengi" - Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Ilani ya CCM 2020-2025 ni kuhakikisha tunatenga Maeneo ya ufugaji yapimwe mpaka kufikia Hekari Milioni 6. Mpango wa wakulima ni kuendeleza juhudi za kujitosheleza kwa mahitaji ya Chakula nchini na kuendelea kuongeza matumizi ya Mbolea, Mbegu bora, Kilimo na Umwagiliaji" - Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Jimbo la Bunda Mjini Kata ya Kunzugu familia 16 Ng'ombe 500 zimeshikiliwa na TANAPA na wana mpango wa kuzitaifisha lakini Mahakama imetoa amri walipe faini, wananchi wanataka kulipa faini ili waokoe Ng'ombe wao lakini TANAPA wanakataa" - Mhe. Esther Bulaya, Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA akimpa taarifa Mhe. Edward Ole Lekaita

"Mpango wa Maendeleo wa Taifa, Waziri wa Mipango na Uwekezaji muanzishe mjadala wa Kitaifa tuzungumze Habari ya Mpango wa Kitaifa. Injini ya Mipango ya Serikali ni Watumishi wa Umma" - Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Tofauti ya nchi yetu na nchi zingine kama Marekani wanaangalia Who You're rather than the Test ulizopata kwenye Distinction zako. They appreciate those who take bold decisions, who do things differently, who overcomes problems, who are strictly smart, who see the word for what they can do and not what they cannot do" - Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Tukiwa na Sheria zinazoleta ukaguzi (Bias) badala ya kusaidia (Support) Ubunifu (Innovation) na watu wa Umma. Nguzo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa ni nidhamu. Ni lazima tutekeleze Ripoti ya CAG" - Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto.

 
Back
Top Bottom