tutamkumbukamagu
JF-Expert Member
- Jul 3, 2021
- 317
- 270
Kwa mujibu wa Katiba yetu hii mbovu ktk ibara ya 52 (2).
(..)Rais atamteua mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi, kuwa waziri Mkuu (..)
N.B. Kila kwenye (..) kuna maneno nimeyaruka.
Sasa huyu mhe Majaliwa alichaguliwa na wananchi ktk Jimbo lake? Jibu ni HAPANA hakuchaguliwa na wananchi. Bali alipita bila kupingwa (maneno batili kabisa ktk demokrasia)
Hata kama alikuwa mgombea pekee ilipaswa wananchi wapige kura kumkubali ama la! Lkn haikufanyika hivo. Kwahiyo wananchi hawakushiriki kabisa katika kumchagua mtu huyu ambaye ndiyo waziri mkuu wa JMT. Pathetic!
Sasa kwann mhe Majaliwa amekuwa Waziri Mkuu ikiwa hakutimiza vigezo vya kikatiba? Jibu ni rahisi tu. Katiba yetu ina mianya mingi ya kupenyeza maovu yanayotokana na uvunjifu wa katiba.
Ndiyo maana tunaitaka katiba mpya itakayo ondoa ujinga huu katika demokrasia.
sasa wewe na baba yako, babu yako kwa nn msiwe waziri wakuu?
kuwa na akili ndogo tu.....
Katiba ni interpretation pia