Nyafwili
JF-Expert Member
- Nov 27, 2023
- 2,773
- 6,885
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini kuwaangalia zaidi vijana, akilitaja kama kundi ambalo liko hatarini zaidi kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI, huku akiwataka kuimarisha huduma za unasihi na malezi yenye mlengo wa kustahimili mabadiliko yanayotokana na utandawazi.
Waziri Majaliwa emetoa wito huo leo Disemba 02, 2023 wakati akizungumza na washiriki pamoja na wadau mbalimbali kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, mara baada ya kushiriki matembezi hayo kwa km. 5, ambayo yameratibiwa na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT).
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo pia kuwaomba viongozi wa dini wawaeleze waumini wao kwamba licha ya mafanikio ambayo Serikali imeyapata kwenye mapambano dhidi ya VVU, wanapaswa watambue kuwa UKIMWI bado upo.
“UKIMWI bado upo, ninawaomba suala hili lipewe kipaumbele wakati wa mahubiri, hotuba na mihadhara. Endeleeni kuwakumbusha waumini kuhusu umuhimu wa kubadili tabia hususan zile zinazochangia maambukizi.” - Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.