Kariakoo na Dar es Salaam: Wanahistoria tendeeni haki Historia za majina hayo

Dar es salaam hujulikana kama "Heaven of Peace" hiyo inajulikana sana na imeandikwa sehemu nyingi mno.

Bandar means port, port city or city by the sea kwa kiarabu; Hata mji ulio pembeni ya bahari huitwa Bandar lexchangeably kwa sababu miji mingi iliyo pembeni mwa bahari hutokana na bandari. Kwa hiyo siyo kosa kuita huu mji bandari ya salama.

"Carrier Corps" ni kikosi maalum cha wabeba mizigo wa KAR na hata Nairobi kuna kariakor, Dar es salaam pia kutokana na makaazi au kambi za vikosi hivyo. Babu yangu mzaa upande wa baba yangu alikuwa KAR na alipewa space mtaa wa Muheza waliporudi kutoka Sri Lanka (mwenyewe alipaita Ceylon) na alikuwa karibu na kea wenzake wengi.
Kikosi hiki kilikuwepo hata kenya. Kariakoo jina limetokana na waingereza.
Hebu twende kwenye historia. Kabla ya Waingereza kuja Tanganyika, Kariakoo ilikuwa inaitwaje? Au hapakuwa na jina?
 
1646223828269.png

Hii ramani ilitayarishwa na Wajerumani 1891. Hakuna kariakoo, kuna kitongoji cha Gerezani na Jangwani. hayo yote ni majina ya kiswahili na yanaeleweka.
 
View attachment 2136302
Hii ramani ilitayarishwa na Wajerumani 1891. Hakuna kariakoo, kuna kitongoji cha Gerezani na Jangwani. hayo yote ni majina ya kiswahili na yanaeleweka.
Kobello,
Mimi nimewasikia wazee wakisema kuwa mji ulikuwa Kisutu ukiangalia hiyo ramani imeandikwa, ''Kissuto.''

Ikiwa hivi ndivyo ina maana Kariakoo kwa jina hili ilikuwa haipo ingawa inawezekana walikuwa wanaishi watu.

Si kila sehemu ina jina.
Majina huja baada ya watu kufanya makazi.

Sasa ukifuata historia ya Kisutu wazee wanasema kuwa msikiti wa kwanza Dar es Salaam ni Msikiti wa Sheikh Mwinyikheri Akida ambao upo Titi Street hadi leo.

Msikiti huu una umri zaidi ya miaka 100 na uko chini ya uangalizi wa kwa sasa wajukuu wa ukoo wa akina Tambaza na waliujenga upya katika miaka ya 1980.

Mimi nimeishi katika utoto wangu Libya Street Jumba la Posta na ule msikiti wa asili ulikuwa jirani yetu na nikiufahamu vizuri halikadhalika nilikuwa nikiingia ''Kisutu Mji.''

Kwa kweli Kisutu palikuwa na mvuto wa peke yake kwa ya zile nyumba zake za kizamani zikivutia kuzitazama.

Nyumba za udongo na makuti sehemu mbili huku na huku kati kuna barabara ya udongo ambayo ndiyo mitaa.

It was like walking back into history.

Sasa hapa nataka nieleze historia ya nyumba ambazo mimi nimekuta wazee wangu kwa nasaba wanazo Kariakoo pamoja na wengine wa rika lao na hizi ni nyumba walijenga kutokana na viwanja walivyonunua.

Babu yangu Salum Abdallah alikuwa na nyumba Mtaa wa Mbaruku na Congo jirani na nyumba ya Aziz Ali.

Hii ni Gerezani.
Hii ni nyumba ya udongo miti na fito na nyingi zilijengwa hivyo.

Bibi yangu Asha bint Farijala alikuwa na nyumba Mtaa wa Msimbazi mimi nazaliwa hii nyumba iko nimeikuta.

Mdogo wake Sophia bint Farijala alikuwana nyumba Mtaa wa Likoma mwisho kuelekea Jangwani.

Hii ni Kariakoo.

Baba yangu mdogo Abdallah Mohamed alikuwa na nyumba Mtaa wa Gogo ambayo yeye alirithi kutoka kwa baba yake.

Hii nyumba ilikuwa jirani kabisa ya soko la Kariakoo.

Bibi yangu mkuu Bi. Deborah yeye nimekuta ana nyumba Mtaa wa Swahili karibu sana na soko la Kariakoo na watoto wake wote wamezaliwa nyumba hiyo katika miaka ya 1920.

Bi. Deborah kazaliwa mwaka wa 1890 na kafariki 1995.

Katika nyumba hizi mimi nimezikuta za mawe ya kutomea udongo na fito na kuchapiwa chokaa.

Nyumba ya bibi yangu Asha bint Farijala huyu alikuwa na nyumba ya kisasa kwa hali ya nyakati zile.

Nyumba hii ilikuwa Mtaa wa Mafia na Msimbazi na ilivunjwa miaka ya 1970 kupisha upanuzi wa barabara ya Msimbazi.

Nyumba nyingine ni ya Sheikh Abdallah Simba huyu alikuwa rafiki ya babu yangu na nyumba yake ilikuwa Mtaa wa Kipata na New Street.

Hii ni Gerezani.

Hizi nyumba zote kama kujengwa zitakuwa zimejengwa mwanzoni mwa miaka ya 1900 na nyumba za kwanza katika hivyo viwanja.

Tunaweza kusema ni nyumba za kwanza kujengwa Kariakoo.

Nyumba hizi zote zilikuwa zinafanana kwa mjengo na nyingine kuezekwa kwa makuti au madebe.

Nyumba ya vyumba sita na uani kuna kuwa na mabanda, jiko na vyoo.

Kwangu mimi nachukulia kuwa Karikaoo kama makazi wazee wetu walianza kujenga na kuishi hapo miaka hiyo ya mwanzoni 1900.

Bila shaka wenyeji walikuwapo na vibanda vyao na mashamba yao na viunga vyao vya minazi.

Labda hii inaweza kutoa picha ya mtu kuweza kuielewa Kariakoo.
Picha hiyo hapo chini ni mmoja wa mitaa ya Gerezani ilivyokuwa ikionekana.

Mimi nimezaliwa mwaka wa 1952 nimekuta huu ndiyo muonekano wa mitaa yote ya Gerezani na Kariakoo pia.

Angalia nyumba za makuti na kuezekwa na madebe na angalia watu walivyokuwa wakivaa.

1646235732635.png

1646239757403.png
 
Hii ni Gerezani

Picha hiyo hapo chini ni mmoja wa mitaa ya Gerezani ilivyokuw aikionekana.

Mimi nimezaliwa mwaka wa 1952 nimekuta huu ndiyo muonekano wa mitaa yote ya Gerezani na Kariakoo pia.

Angalia nyumba za makuti na kuezekwa na madebe na angalia watu walivyokuwa wakivaa.

View attachment 2136444

View attachment 2136482
Samahani sijalielewa swali lako. Au sijaipata mantiki.
Tanzania siyo jina tulilojipa wenyewe. Ilikuwepo na watu waliishi katika miji mbalimbali ikijulikana kwa majina mbalimbali.
Tatizo siyo kutokuwepo nyumba na wakati, Bali jina la sehemu, na mara nyingi majina huja baadae . Pia majina mara nyingi hupewa na wageni au wasfiri wa kutoka sehemu nyingine.
Evidences nyingi zinaegemea Kariakoo kuwa jina lililotokana na wazungu.
Hii haiondoi uwepo wa waafrkia wanaofuata dini ya kiislam katika maeneo hayo.
Wala haimaanishi kuwa Dar es salaam ni mji wa wakristo, la hasha.
Waarabu, wahindi, wapersia na wazungu wote kwa nyakati tofauti au Moja wamehusika na kujenga na kubomoa mji wa Dar es salaam na Vitongoji vyake.
Andikeni historia wanenu wazisome, lakini msimamie ukweli.
 
Samahani sijalielewa swali lako. Au sijaipata mantiki.
Tanzania siyo jina tulilojipa wenyewe. Ilikuwepo na watu waliishi katika miji mbalimbali ikijulikana kwa majina mbalimbali.
Tatizo siyo kutokuwepo nyumba na wakati, Bali jina la sehemu, na mara nyingi majina huja baadae . Pia majina mara nyingi hupewa na wageni au wasfiri wa kutoka sehemu nyingine.
Evidence nyingi zinaegemea Kariakoo kuwa jina lililotokana na wazungu.
Hii haiondoi uwepo wa waafrkia wanaofiata dini ya kiislam katika maeneo hayo.
Wala haimaanishi kuwa Dar es salaam ni mji wa wakristo, la hasha.
Waarabu, wahindi, wapersia na wazungu wote kwa nyakati tofauti au Moja wamehusika na kujenga na kubimoa mji wa Dar es salaam na Vitongoji vyake.

Kuna swali limeulizwa?

Nimejitahidi kueleza niyajuyo.
 
Kobello,
Kuna swali limeulizwa?

Nimejitahidi kueleza niyajuyo.
Mohamed Said,
Nilikuwa bado sijaipata mantiki kutoka kwenye maandishi yako.

Lakini uliyoyasema ni sawa na picha ulizoweka mimi hasa hiyo ya pili mara yangu ya kwanza kuiona ni mwaka 1980 katika kitabu kimoja ambacho marehemu baba yangu alikuwa nacho na mpaka sasa hivi kipo nyumbani kwetu. Kilikuwa kitabu ninachokipendda sana kwa sababu katikati kulikuwa na kurasa zenye picha na hiyo ilikuwa ni mojawapo.

My point is, mimi natambua lengo la post yako na ujumbe ambao kwa msomaji mzuri wa vitabu na nakala ataupata ni pale uliposema hivi.
Angalia nyumba za makuti na kuezekwa na madebe na angalia watu walivyokuwa wakivaa.
Ukijaribu kuangalia kiundani zaidi utaona kuwa hayo si "madebe" kama ulivyotanabahisha, bali ni corrugated sheets ambazo ni used. Siyo flat sheets.
Nasema hivyo kwa sababu, building materials zinaelezea technology na technology ni kielelezo kizuri cha time-frame. Corrugated sheets zimefika Africa throgh military. Kambi za jeshi na nyumba za polisi post first world war. Hizo picha nazipa post Germany colonization. Kihistoria, na kwa uchakavu wa mabati hayo, naipa time ya pre- second to even post second world war kwa nyumba binafzsi kuezeka corrugated sheets (pia age ya hizo sheets zimezeeka sana).
Naweza kabisa kusema kuwa wakati wa picha hizo, makea walishaanza kukaa kariakoo na kuhusu kanzu ulizotaka kutujulisha, ni kweli waislamu walikuwa wengi katika maeneo hayo but that's besides the point kuwa Kariakoo ni jina lililotokana na wazungu. To dispute that, you will be running a very high risk of "lampooning the cliche".
 
Mimi nimezaliwa Mtaa wa Kipata Gerezani.
Hizi nyumba nazijua kwa kuwa nimeishi ndani yake na nimeziona kwa macho yangu.

Kuhusu asili ya jina ''Kariakoo,'' sikusema lolote.
 
Kobello,
Nitashukuru kama utanifahamisha kosa langu ili nijisahihishe.
Kosa lako kubwa ulilolifanya ni kunyamaza kimya kuhusu mada iliyopo mezani. Kwa ufahamu wako jina "Kariakoo" limetokana na nini?

Badala yake, ukaanza kuelezea jinsi mji wa Kisutu na Gerezani ulivyokua na mandhari yake. Hapo umekwepa jukumu ulilokuwa nalo kama mkaazi wa maeneo hayo kwa vizazi angalau viwili pia (most importantly) wewe kama mwandishi ambaye maisha yamekupa fursa ya kupitia historia kimaandishi na kiimla juu ya maeneo hayo.

Maelezo yako yangesaidia kutoa elimu kwa vijana, lakini umehepa hilo. Wakati mwingine historia haikupendezi na haikusifii kama unavyotaka, lakini ni historia na kuinyamzia elimu uliyokuwa nayo si uchoyo tu bali ni kukosa uwajibikaji.
 
Kimantiki mimi nakubaliana 100% na Aunt FaizaFoxy kwamba Kariakoo ni derivative ya maneno mawili; Qarya na kuu (Qaryah kwa kiarabu قرية) ni kijiji au mji, kwa maana hiyo Kariakoo ni sawa useme; kijiji/mji mkuu, katika mazingira hayo ilikuwa ni rahisi sana eneo hilo kupewa jina Qarya kuu (na baadaye kutamkwa Kariakoo) kutokana na maneno hayo kuliko kutokana na maneno Carrier corps (keria kops) kwani maneno hayo (carrier corps) hayana nguvu ya kimantiki ukilinganisha na Maneno; Qarya kuu. Labda tuseme imekuwa coincidence kwamba maneno "Qarya kuu" na "Carrier corps" yanafanana kiasi fulani kimatamshi na Carrier corps walihusika mahali hapo kwa namna fulani na ndio maana mkanganyiko ukatokea wa lipi ni lipi??.
 
Kosa lako kubwa ulilolifanya ni kunyamaza kimya kuhusu mada iliyopo mezani. Kwa ufahamu wako jina "Kariakoo" limetokana na nini?

Badala yake, ukaanza kuelezea jinsi mji wa Kisutu na Gerezani ulivyokua na mandhari yake. Hapo umekwepa jukumu ulilokuwa nalo kama mkaazi wa maeneo hayo kwa vizazi angalau viwili pia (most importantly) wewe kama mwandishi ambaye maisha yamekupa fursa ya kupitia historia kimaandishi na kiimla juu ya maeneo hayo.

Maelezo yako yangesaidia kutoa elimu kwa vijana, lakini umehepa hilo. Wakati mwingine historia haikupendezi na haikusifii kama unavyotaka, lakini ni historia na kuinyamzia elimu uliyokuwa nayo si uchoyo tu bali ni kukosa uwajibikaji.
Kobello,
Sijui kwa nini umekuwa mkali.
Mimi nimeangalia ramani ambayo Kariakoo haipo.

Nikasema kweli jina kuwa sehemu hii ni Kariakoo haipo.

Nikaeleza kuwa jina hakuna lakini labda ni kwa kuwa hapakuwa na wakazi.

Ndipo nikaeleza nyumba za ukoo wangu zilizokuwa karibu ya Kariakoo na miaka ambayo huenda zilijengwa kama njia ya kuweza kujua ni lini watu walianza kujenga nyumba hapo.

Hili kwangu ndilo nililoona muhimu.
Wewe ulipenda nizungumze asili ya jina Kariakoo.

Hili mimi sikulipa umuhimu kwa kuwa ni elimu mashuhuri kila mtu anafahamu na Maalim Faiza kachangia mapya katika jina hili.

Mimi nikaona nieleze kile ambacho si wengi wanakifahamu.

Sisi wenyeji wa mji huu tumepokea kutoka kwa wazee wetu kuwa Dar es Salaam ikiitwa Mzizima lakini hiyo ramani haionyeshi jina hilo sehemu yoyote.

Hapo Kariakoo kuna Mtaa unaitwa Mzizima na si mbali na soko na hapo kuna nyumba ya asili ya Bi. Sikitiko mmoja wa akina mama maarufu sana Dar es Salaam katika wakati wake.

Nyumba hizi zote ninazokutajia za watu hawa ni kuwa koo zao bila shaka zilikuwapo hapo kabla ya hilo jina la Kariakoo na baadhi ya koo hizi bado zipo hapa Dar es Salaam hadi hii leo.
 
Jina Dar es salaam limeanza kutumika 1866.
Hiyo ramani ya 1890.
Yaishe.
 
Kwa nini ndugu yangu unaghadhibika?
Hatugombani tunajadili.

Mimi sikujua kuwa jina la Dar es Salaam lilianza 1866.

Nakushukuru umeniongezea elimu.
Ramani hii ni 1891.

Haipendezi tuhitimishe mjadala wetu kwa kisirani.
 
Sijagadhibika ila umepta elimu, ishikilie.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom