~ Kanga zina Mambo Mengi ~

Kanga zina mambo mengi, zina mengi hizo kanga,

Kanga zinaficha vingi, vinavyofichwa na kanga,

Kanga zina siri nyingi, zina siri hizo kanga,

Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga!

Kanga zinaona mengi, chumbani ziliko kanga,

Kanga zahifadhi vingi, vyasitiriwa na kanga,

Kanga zafunika mengi, visivyoonwa bila kanga,

Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga!

Kanga zinagusa vingi vinavyoguswa na kanga,

Kanga zapangusa pengi, papanguswapo na kanga,

Kanga zina hisa nyingi, za wadau wenye kanga,

Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga

Kanga zinaganda vingi, visivyoganduka bila kanga,

Kanga zinashinda nyingi, kweli vitenge si kanga,

Kanga zina rangi nyingi, na misemo kwenye kanga,

Kanga unapoachiwa , ana penzi mwenye kanga.

Kanga hata kama nyingi, atakupa moja kanga,

Kanga itasema mengi, kubwa ni hilo la kanga,

Kanga yatangaza vingi, hakuna kuzidi kanga,

Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga.

UKIMPENDA ITUNZE.

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

(picha kutoka Mombasa Events)

<br /
M.M.mwanakijiji,naona unatunza vya nyumbani,ni kwel kabsa,kanga inaladha yake,mama wangu watoto anapoivaa moja hua najua ucku kutakua na international match btn ManU na Barca.

Khanga moko ndembendembe. Mambo yote iko kila Jumatano pale hotel Continental bana.

Wenyewe wanakwambia laki si pesa! Teh teh teh

Mzee mwanakijiji, naomba ufafanuzi
majibu nayahitaji, niyafanye maamuzi
ninaomba nikuhoji, nisijefanya ajizi
Kanga unayoisema, ni ndege au ni nguo?

Mimi nawafuga kanga, ni kitoweo kizuri
ukila wa kukaanga, watamu kama asali
watalaamu wa kuunga, hili watalikubali
kanga unayemsema, ni ndege au ni nguo?

Mzee mwanakijiji, naomba ufafanuzi
majibu nayahitaji, niyafanye maamuzi
ninaomba nikuhoji, nisijefanya ajizi
Kanga unayoisema, ni ndege au ni nguo?

Mimi nawafuga kanga, ni kitoweo kizuri
ukila wa kukaanga, watamu kama asali
watalaamu wa kuunga, hili watalikubali
kanga unayemsema, ni ndege au ni nguo?

Kanga afugwae baba hawezi ishi chumbani..
Hata kwa yake manyoya hawezi kausha maji..
Kanga aisifiayo ni ile ionayo mwili...
Hata ukiwa bafuni ruksa kukuchingulia!

Kanga ina raha zake hata kwake mvaaji..
Acha we huko pembeni ulobaki mwangaliaji..
Unaetamani kuona kila saa ikiwa maji..
Hakika kanga jamani...mi naipenda sana!

Yampendeza mnene hata nae mwembamba..
Utashangaa wanaume jinsi inavyowabamba..
Mimacho itawatoka hauwaishi ushamba..
Hakika kanga jamani...mi naipenda sana!

Naifunga kibwebwe shereheni nikienda..
Ikikamata kiuno hakika utaipenda..
Nikiifunga kifuani kesi nimeshaishinda..
Hakika kanga jamani mi naipenda sana!

d! Kumbe kanga inavutia kiasi hiki,mbona sasa wengine wanavaa jeans chumban?

Mzee Mwanakijiji hujapitapita kinondoni-mkwajuni...huwa hawavai hivyo.
besides when they are closing the road is very fun movie watching.

also i wonder why so called fashionalist are blind in this style.

Kanga inaniuwa, kifo cha mende jamani
Kanga yanizuzuwa, hata njia siioni
Kanga iliyovaliwa, mimi huku hamkani
Kanga ilobenuliwa, akh! hivi naitwa nani?

Kanga yanipagawisha, yanikosesha amani
Kanga wakijivalisha , napayukwa hadharani
Kanga yanipa mkesha, akivaa wa pembeni
Kanga inavyonikosha, naweza honga milioni

Kanga ya kifuani , pumzi nusu hupotea
Kanga ya kiunoni, huishia kuzimia
Kanga hizi si utani, asifiwe alovumbua
Kanga akiwa chumbani, burudani yatulia.

By Klorokwini a.k.a kibaka mzoefu

Kanga inaniuwa, kifo cha mende jamani
Kanga yanizuzuwa, hata njia siioni
Kanga iliyovaliwa, mimi huku hamkani
Kanga ilobenuliwa, akh! hivi naitwa nani?

Kanga yanipagawisha, yanikosesha amani
Kanga wakijivalisha , napayukwa hadharani
Kanga yanipa mkesha, akivaa wa pembeni
Kanga inavyonikosha, naweza honga milioni

Kanga ya kifuani , pumzi nusu hupotea
Kanga ya kiunoni, huishia kuzimia
Kanga hizi si utani, asifiwe alovumbua
Kanga akiwa chumbani, burudani yatulia.

By Klorokwini a.k.a kibaka mzoefu

weweweeeee! kumbe Kidonge hiki chaweza kuwa kitamuuuuu

Kwa watu wa pwani, khanga ni culatral expressions and it deliver important messages....

Utawakuta wanawake wamekaa kisimani/bombani na wamevaliana kanga zenye maneno kama;

1) huniwezi wewe
2) mama Mkwe hasidi
3) mambo iko huku
4) mlaji kala leo mla jana kala nini

na mengine mengi tu. Kwa watu wa pwani, khanga ni instrument muhimu kwa mipasho!

Kanga ina raha zake hata kwake mvaaji..
Acha we huko pembeni ulobaki mwangaliaji..
Unaetamani kuona kila saa ikiwa maji..
Hakika kanga jamani...mi naipenda sana!

Yampendeza mnene hata nae mwembamba..
Utashangaa wanaume jinsi inavyowabamba..
Mimacho itawatoka hauwaishi ushamba..
Hakika kanga jamani...mi naipenda sana!

Naifunga kibwebwe shereheni nikienda..
Ikikamata kiuno hakika utaipenda..
Nikiifunga kifuani kesi nimeshaishinda..
Hakika kanga jamani mi naipenda sana!

Umenifurahisha sana wafa kuwa mama mkwe

Similar Discussions

Back
Top Bottom