~ Kanga zina Mambo Mengi ~

Kanga inaniuwa, kifo cha mende jamani
Kanga yanizuzuwa, hata njia siioni
Kanga iliyovaliwa, mimi huku hamkani
Kanga ilobenuliwa, akh! hivi naitwa nani?

Kanga yanipagawisha, yanikosesha amani
Kanga wakijivalisha , napayukwa hadharani
Kanga yanipa mkesha, akivaa wa pembeni
Kanga inavyonikosha, naweza honga milioni

Kanga ya kifuani , pumzi nusu hupotea
Kanga ya kiunoni, huishia kuzimia
Kanga hizi si utani, asifiwe alovumbua
Kanga akiwa chumbani, burudani yatulia.

By Klorokwini a.k.a kibaka mzoefu

Malaria kwishneee:dance:
 
Nakumbuka moja niliwahi kusoma zamani "Umeyataka Mwenyewe"..

Sasa hadi leo sijui ujumbe huo ulikuwa unamhusu nani, kwanini na kwa vipi. Nilitaka hata kuuliza "imekuwaje"? Kwa kweli kanga nyingine huacha maswali bila kujibu wala kujaribu kujibu.

TM umepotea saaaaaaana assante kwa hii ya kuunga mkono ile. Ngoja tusubiri Khangaologists waje kutupa elimu hapa.
 
Mkuu mwanakijiji, fani yako ni kucheza na mameno tena kwa kalamu so jitahid ujikite ktk uandishi rasmi kaka!
 
FashionLinzy7293.jpg

Kanga zina mambo mengi, zina mengi hizo kanga,
Kanga zinaficha vingi, vinavyofichwa na kanga,
Kanga zina siri nyingi, zina siri hizo kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga!

Kanga zinaona mengi, chumbani ziliko kanga,
Kanga zahifadhi vingi, vyasitiriwa na kanga,
Kanga zafunika mengi, visivyoonwa bila kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga!

Kanga zinagusa vingi vinavyoguswa na kanga,
Kanga zapangusa pengi, papanguswapo na kanga,
Kanga zina hisa nyingi, za wadau wenye kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga

Kanga zinaganda vingi, visivyoganduka bila kanga,
Kanga zinashinda nyingi, kweli vitenge si kanga,
Kanga zina rangi nyingi, na misemo kwenye kanga,
Kanga unapoachiwa , ana penzi mwenye kanga.

Kanga hata kama nyingi, atakupa moja kanga,
Kanga itasema mengi, kubwa ni hilo la kanga,
Kanga yatangaza vingi, hakuna kuzidi kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga.

UKIMPENDA ITUNZE.

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
(picha kutoka Mombasa Events)
Mwanakijiji kweli we ni mtata, maana duh! ila ndo wazee mlobakia cku hizi.
 
Mkuu ebu nijuze, bado sijaijua kanga
Kanga naona kitenge, nini ni siri ya kanga?
Kanga nipewe kipande, nguo gani nitashona?
Kanga yafaa kitenge, hata shati utashona

kanga ya nini mkuu, nikipewa niitunze!
kitenge bado kigumu, kanga bora ya kitenge
kanga na wepesi huu, haidumu kama tenge
Kanga yafaa kitenge, bora utashona sare.

Kanga nilipewa pwani, hakika sikuitunza
kanga ina siri gani, Bara hatujui kanga
Mkuu niweke wazi, nini ni siri ya kanga?
Kanga yafaa kitenge, kwa gauni lashoneka.
 
Na nyie mkome na mananiiii yenu yacyo na hekima. Mbna magaguro na vipens vyenu vyenye mabao kibao amviweki hadharan. Hamna lolote mmekosa 2 pa kutuliza hyo michebwengo yenu. Mwatiana hashki 2.
 
Na nyie mkome na mananiiii yenu yacyo na hekima. Mbna magaguro na vipens vyenu vyenye mabao kibao amviweki hadharan. Hamna lolote mmekosa 2 pa kutuliza hyo michebwengo yenu. Mwatiana hashki 2.
He!! Vipi kwani........hupendi kanga inavyopewa sifa??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom