~ Kanga zina Mambo Mengi ~

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
FashionLinzy7293.jpg

Kanga zina mambo mengi, zina mengi hizo kanga,
Kanga zinaficha vingi, vinavyofichwa na kanga,
Kanga zina siri nyingi, zina siri hizo kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga!

Kanga zinaona mengi, chumbani ziliko kanga,
Kanga zahifadhi vingi, vyasitiriwa na kanga,
Kanga zafunika mengi, visivyoonwa bila kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga!

Kanga zinagusa vingi vinavyoguswa na kanga,
Kanga zapangusa pengi, papanguswapo na kanga,
Kanga zina hisa nyingi, za wadau wenye kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga

Kanga zinaganda vingi, visivyoganduka bila kanga,
Kanga zinashinda nyingi, kweli vitenge si kanga,
Kanga zina rangi nyingi, na misemo kwenye kanga,
Kanga unapoachiwa , ana penzi mwenye kanga.

Kanga hata kama nyingi, atakupa moja kanga,
Kanga itasema mengi, kubwa ni hilo la kanga,
Kanga yatangaza vingi, hakuna kuzidi kanga,
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga.

UKIMPENDA ITUNZE.

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
(picha kutoka Mombasa Events)
 
Mzee Umeshaa chiwa khanga?
 
Mzee Mwanakijiji,
Ujumbe wako katika jukwaa la MMU,
Ni kama ladha ya supu iliyotiwa ndimu,
Ubarikiwe sana!!!!!!!!!
 
nimependa shairi,kanga na mvaaji mwenyewe
sikujua zinamaana kiiiiiiivyo,
kumbe kuna haja yakuacha japo kipande kila unakopitia
 
usiombe ikiwa imevaliwa akitoka bafuni.
wenye mihemko ya express tangu kifuani
kuhangaika kwa mapigo kutoka moyoni
Kanga unapoachiwa, ana penzi mwenye kanga.
 
Jamaa kashtuka chumbani kuna kanga akampigia simu haraka mpenzi wake:

"Dear umeacha kanga yako hapa"
"Iache tu" akajibiwa.

Jioni anakuja mpenzi wake mwingine anakuta kanga ndani imesambaa juu ya kitanda kama mkeka. Anaulizwa

"Kanga ya nani hii".
"Ya dadangu" anamjibu...

liasheshe....
 
Nyumba nzima itakuwa kama kiganya cha mkono.... Hahahaha..
 
Kanga ina raha zake hata kwake mvaaji..
Acha we huko pembeni ulobaki mwangaliaji..
Unaetamani kuona kila saa ikiwa maji..
Hakika kanga jamani...mi naipenda sana!

Yampendeza mnene hata nae mwembamba..
Utashangaa wanaume jinsi inavyowabamba..
Mimacho itawatoka hauwaishi ushamba..
Hakika kanga jamani...mi naipenda sana!

Naifunga kibwebwe shereheni nikienda..
Ikikamata kiuno hakika utaipenda..
Nikiifunga kifuani kesi nimeshaishinda..
Hakika kanga jamani mi naipenda sana!
 
Lizzy....
Hongera
:A S 41::clap2::A S 41:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom