Kampeni ya kuikataa Vodacom

Kampeni ya kuikataa Vodacom

Ni wazi kampuni ya simu ya VODACOM inapitia kipindi kigumu na hii ni kutokana na tuhuma za kuruhusu mamlaka za nchi kudukua mawasiliano ya wateja wake.... Hili ni jambo baya na itawachukua muda kidogo mpaka kuja kukaa sawa tena.... Si kwamba watatetereka sana la hasha ila watu wengi watahoji umahiri na weledi wao kwenye kuhifadhi taarifa za wateja wao!

Kuna outrage kubwa kutoka kwa watu mbali mbali hasa viongozi wa kisiasa na watu wengine wa kaliba mbali mbali wakihamasisha watu waususie huu mtandao... Baadhi ya watu ni prominent figures ambao wana wafuasi wengi hivyo wanaisulubu VODACOM watakavyo....

Swali la kujiuliza.. Kwanini kadukuliwa Voda na si mitandao mingine....
Jibu ni kwamba si kwamba mitandao mingine ina kikubwa cha ziada na haiwezi kudukuliwa...
Kilichowaponza VODACOM ni uimara wa mtandao wake, huduma bora (mapungufu yapo) na kuweza kuhimili soko muda mrefu bila kuyumba wala kubadilibadili jina la biashara zaidi ya kubadili rangi na logo zake
Uimara wa vodacome na uhakika wa huduma zake.. Umevutia watu wengi prominent wakiwamo viongozi wa kaliba zote, watu maarufu na watu wa kawaida pia
Sinema za udukuzi zinazoendelea wateja wake wengi ni wa vodacome lakini si kwamba mitandao mingine haidukuliwi wala haidukuliki....
Tunaweza kufuata panic ya wanasiasa na kuususia mtandao wa vodacome... Lakini ni vema kumakinika ili usije ukajikuta unaruka mkojo na kukanyaga kinyesi.... Si vema kufuata mkumbo.. Hakuna mtandao ambao haidukuliki Tanzania....! Tusidanganyane kabisa... Maadui wa Voda na wenye chuki binafsi na huu mtandao wasikubebe kwenye mkumbo usiojua.... Ukitaka usidukuliwe tumia satellite mobile phones kama thuraya nk

Nitabaki VODACOM bado sijaona mbadala wake.... Huu ni upepo mchafu tu utapita... Mawasiliano yetu bado yataendelea kulindwa kwa kadiri inavyowezekana... Tunailaumu VODACOM lakini kamwe hatujariribu kujiuliza kama tungekuwa sisi kwenye nafasi yao tungefanyaje...

VODACOM client since 2000
Nchi hii mambo mengine inaendeshwa kihuni, walianza kwa kumjegea hofu CEO wao, wakamfungulia mashitaka ya kihuni , ili baadae wakamilishe nia yao ovu.
 
Vodacom nawapendea kwenye kasi ya internet wako vizuri, lakini hawa jamaa wana vifurushi ghali sana watu "wanapitiamo" humohumo.
.
Huu ni muda muafaka kwa Tigo kuchanga karata zake vizuri wawe na strong network kila sehemu na upatikanaji internet kila mahala watawapiku Vodacom kwa sabab hiki ndicho kinawafanya Voda kuwa na watumiaji wengi.
.
Khaly
 
Napokea kwa unyenyekevu... Natambua nimekuudhi lakini ni vema kubalance story... Kila kitu kina pande mbili...
kaka mshana.nakuheshimu sana. naweza kukutajia watu ambao naweshimu wwe ni mmoja wapo. nakuheshimu kwa mchango na knowlege yako. nimesoma vya kutosha lakini ......
itoshe tu kusema NAKUHESHIMU KAKA MSHANA
 
kaka mshana.nakuheshimu sana. naweza kukutajia watu ambao naweshimu wwe ni mmoja wapo. nakuheshimu kwa mchango na knowlege yako. nimesoma vya kutosha lakini ......
itoshe tu kusema NAKUHESHIMU KAKA MSHANA
 
Aise mimi nina line nne lakini ikitokea kuna line natakiwa niache kuzitumia na nizitupe basi katika line ambayo siwezi kuiacha wala kuitupa ni ya Vodacom kwa sababu kwanza kabisa mimi naipenda na naitumia sana M Pesa katika miamala yangu pili ndo line niliyosajilia Sim Banking na sitarajii kusajilia line nyingine

Yaani Vodacom huwa nawakubali tu kwenye huduma ila vifurushi vyao ni ghali sana na MB au GB huwa zinaisha haraka sana hivyo huwa siitumii sana kwa ajili ya mawasiliano wala mtandao lakini kamwe siwezi kuacha kuwa mteja wa Vodacom kwa namna yoyote ile yaani kuwa tu mteja wa mtandao mkubwa kama Vodacom kwangu ni fahari na heshima kubwa
 
Back
Top Bottom