Ni wazi kampuni ya simu ya VODACOM inapitia kipindi kigumu na hii ni kutokana na tuhuma za kuruhusu mamlaka za nchi kudukua mawasiliano ya wateja wake.... Hili ni jambo baya na itawachukua muda kidogo mpaka kuja kukaa sawa tena.... Si kwamba watatetereka sana la hasha ila watu wengi watahoji umahiri na weledi wao kwenye kuhifadhi taarifa za wateja wao!
Kuna outrage kubwa kutoka kwa watu mbali mbali hasa viongozi wa kisiasa na watu wengine wa kaliba mbali mbali wakihamasisha watu waususie huu mtandao... Baadhi ya watu ni prominent figures ambao wana wafuasi wengi hivyo wanaisulubu VODACOM watakavyo....
Swali la kujiuliza.. Kwanini kadukuliwa Voda na si mitandao mingine....
Jibu ni kwamba si kwamba mitandao mingine ina kikubwa cha ziada na haiwezi kudukuliwa...
Kilichowaponza VODACOM ni uimara wa mtandao wake, huduma bora (mapungufu yapo) na kuweza kuhimili soko muda mrefu bila kuyumba wala kubadilibadili jina la biashara zaidi ya kubadili rangi na logo zake
Uimara wa vodacome na uhakika wa huduma zake.. Umevutia watu wengi prominent wakiwamo viongozi wa kaliba zote, watu maarufu na watu wa kawaida pia
Sinema za udukuzi zinazoendelea wateja wake wengi ni wa vodacome lakini si kwamba mitandao mingine haidukuliwi wala haidukuliki....
Tunaweza kufuata panic ya wanasiasa na kuususia mtandao wa vodacome... Lakini ni vema kumakinika ili usije ukajikuta unaruka mkojo na kukanyaga kinyesi.... Si vema kufuata mkumbo.. Hakuna mtandao ambao haidukuliki Tanzania....! Tusidanganyane kabisa... Maadui wa Voda na wenye chuki binafsi na huu mtandao wasikubebe kwenye mkumbo usiojua.... Ukitaka usidukuliwe tumia satellite mobile phones kama thuraya nk
Nitabaki VODACOM bado sijaona mbadala wake.... Huu ni upepo mchafu tu utapita... Mawasiliano yetu bado yataendelea kulindwa kwa kadiri inavyowezekana... Tunailaumu VODACOM lakini kamwe hatujariribu kujiuliza kama tungekuwa sisi kwenye nafasi yao tungefanyaje...
VODACOM client since 2000




watakuja na hasira Kaka