Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Kimemuuma sansa kumteua mkristo kiasi kwamba amehakikisha katengeneza nafasi mpya isiyo na tija ili kuwaridhisha wafadhili wake wa Islamization of our mother country, amelaniwa anayetegemea mwanadamu
 
Lakini tukirudi Nyuma...Mwinyi (Rais wa awamu ya pili) alimteuaA. Mrema( Mb) kuwa Naibu waziri mkuu...!Na inasemekana Mrema analipwa masurufu ya nafasi hiyo ya Unaibu waziri mkuu. Swali, Je.Mwinyi Alikiuka Katiba?

Hayo ndo matokeo ya Udhaifu wa katiba na matumizi mabaya ya madaraka,,,! tucyatetee Watu timamu wanapotaka KATIBA MPYA lengo ni kuondoa upuuzi km huo mtu anajiamualia2 kujianzishia Vyeo kwaajili ya washkaji,,,?
 
Namchukia sana mtu ambaye kabla ya kumteua mtu kushika nafasi anaanza kujiuliza, huyu ni wa dini gani, nitafanyaje kubalance dini, n.k. Mteue mtu kwa kuangalia uwezo wake bila ya kujali kama mi muislam, mkristo au mpagani.

Kikwete anafanya kosa kubwa kwa kufikiria kuwa akiwateua watendaji wake kwa kubalance dini ndiyo ataonekana ni kiongozi mzuri. Kikwete ataingia kwenye kumbukumbu kwa kuwa Rais mdini. Kuwa mdini hakumaanishi kuwapendelea watu wa dini yako bali ni kufanya mambo kwa mtazamo wa dini ya mtu. Hata pale Rais anapoamua kuwa nafasi hii sasa nimpe mtu wa dini fulani kwa vile aliyetangulia alikuwa wa dini fulani, nao ni udini.

Jk ametengeneza cheo cha Naibu Mkuu wa Polisi, ambacho hakipo kwenye muundo wa jeshi la polisi kwa nia ya kuwafurahisha maswahiba wake hata bila ya kuwepo sababu za msingi za kutengeneza nafasi hiyo. Hapo ndipo udhaifu wa uongozi wa Kikwete unapoonekana wazi.

Well spoken brother!

Huyu fastjet cjui cjui anaipeleka wapi Nchi. Alianzisha kwenye campaign 2010 watanzania kumbukumbu tumeitunza ipo Cku ataulizwa tu, Muda ukifika Hakuna wa kuzuia.
 
Said mwema kastaafu au naye kapigwa chini kwa nguvu kama boss wake Nchimbi?
Kila la kheir kwa aliyetoka na aliyeingia.

Afande Said Ali Mwema amestaafu rasmi tangu tarehe 26/12/2013, kila heri kwake..
Afande Mangu ni mtu mwenye upeo mkubwa, msomi na anasimamia sana taratibu za kijeshi.
Hivyo tutegemee kuendelea kuboreshwa kwa nidhamu ya askari, hongera kwake.
Afande Abrahaman Kaniki ni msomi pia, anapenda sana kufundisha na kujifunza hivyo ni sahihi kwake kuwa mshauri wa IGP, nampa hongera pia.
 
Tusio na dini tunahujumiwa na Jk.

Teh teh teh, msio na Dini mlikuwa mnawakilishwa na Mzee Kingunge na sasa hivi amestaafishwa kwa Manufaa ya Umma,so subiri tena miaka 50 ijayo atokee tena Mtu kama yeye.
 
Someni vizuri huo ujumbe kuna muundo mpya wa jeshi la polisi ndiyo unafuata. tujadili uwezo wao

Kuwa na muundo Mpya ni lazima kurundika watu kwenye CHEO 1? mi nadhani km lengo nikuboresha utendaji wa Polis wangewaongezea vifaa sio kujaza watu!
 
Ni vyema na hongera kinachopasa kwao ni kuendelea kuboresha jeshi la Polisi ktk kupambana na uhalifu askari kufuata sheria na kuboresha maslai hayo ili kupunguza rushwa.
 
Tutajie tofauti kubwa hiyo.
How you perform investigation without involving intelligence ?
Kama kuna anayejua role Director of Criminal Investigation na Director of Criminal Intelligence atusaidie tafadhali
Of course mara nyingi tulikuwa tunamsikia Director of Criminal Investigation kidogo tunajua role yake sasa huyo mwingine.....?

Kwa ufupi: investigation ni uchunguzi wa taarifa nyeti baada ya uhalifu (wa kijinai) kuwa umeshafanyika (post);
Intelligence: uchunguzi wa taarifa nyeti kabla ya uhalifu (wa kijinai) haujafanyika (pro)
 
Ernest Mangue
Produce at Whole Foods Market Napa
Went to Andrew Hill High School '93

Lives in Napa, California

In a relationship with Brianna Bristow

qOj82g6S0tS.png

Listens to Sublime and the DEVEROS





Ana uhusiano na huyu?!!
 
Rais angefanya Staili ya Uganda,Kenya , na Rwanda ya kuwateua Majenerali toka Jeshini Kuwa wakuu wa Polisi kwani uzoefu umeonyesha Kuwa wakiwa ni wanajeshi nidhamu ndani ya jeshi inaimarika zaidi kuliko wakitawaliwa na IGP anayetoka humo humo polisi .

Alafu yakitokea ya tokomeza atalaumiwa nani? Msipende kudharau haya majeshi yana miongozo yake. Ukimweka mwanajeshi alafu watu wasifike mahakamani na wakaning' inizwa kwenye mti siku tatu msilaumu.
 
Karibu Mzee wangu Mangu,namuomba Mungu Mkuu akujalie Siha Njema,Busara,Hekima,Ustahimilivu na Utulivu katika Uongozi wako hasa katika kufanya maamuzi kwa manufaa ya Taifa.
 
Kamanda huyu wa Mwanza anaheshimika sana ndani ya Jeshi la Polisi. Tangu achukue mikoba iliyoachwa wazi na hayati Liberatus Barlow aliyekuwa akishikilia wadhifa huo na kuuawa kikatili, Mangu amefanya vema.
Anatajwa kuwa msomi wa shahada ya kwanza katika Sayansi ya Polisi (Police Science) aliyoipata ughaibuni. Anaelezwa kuwa msimamizi mzuri wa misingi ya upolisi kama ilivyoainishwa katika Police General Order (PGO).
Siku hizi, askari hawafuati misingi ya upolisi kama ilivyo kwenye PGO. Misingi inasema, kwa mfano, askari hatakiwi kuacha lindo hadi mwenzake afike lakini siku hizi askari anaacha silaha lindoni kabla mwenzake hajafika.
�Ni jambo la kawaida siku hizi kuona askari akiingia kazini huku amelewa. Lakini kwenye PGO unaambiwa kabla askari hajaingia lindoni ni lazima akaguliwe lakini hilo halifanyiki siku hizi. Mangu anaweza kusimamia PGO,� kilisema chanzo hicho.
- See more at: Raia Mwema - Watatu wapitishwa

Kweli kamanda Kitundu.
 
Si tulisikia kuwa IGP - Msataafu Said Mwema kaongezewa miaka 2?? Ilikuwa zuga??

hahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa!!! hiyo miaka 2 ilikuwa ni taarifa toka kwa intelejinsia ya wanaojiita makamanda. ni umbuko safi kabisa. sasa waanze tu kumpondea, maana ndivyo wanavyofunzwa huko kambini!
 
Hongera sana mkuu,
Naamini utazidi kuimarisha jeshi letu la polisi.

Hongera pia JK walau umekonga nyoyo za wale wa mfumo Kristo.
 
Uteuzi ni mzuri sana. Makamanda wote wana uwezo sawa. Ila kuanzisha nafasi kwa ajili ya kubalance masuala ya dini kwenye vyombo vya dola ni jambo la hatari sana. Ni vizuri tunapoanzisha nafasi kubwa kwenye majeshi tuwe tunafanya tathmini ya kina.
 
IKO CHEO CHA UNAIBU NAZANI KIMEWEKWA ILI KUBALANCE UDINI
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).
 
Nashangaa sana wanaompongeza na kushukuru badala ya kumhurumia na hoja ya kuwa eti ni usomi hii haina hoja hoja ni utendaji kazi kwamba kazi hiyo ataiweza pili ataweza kuboresha masirahi ndani ya jeshi na kutoa matabaka ndani yake na kuleta usawa wa vyeo kuacha vya kupeana kama chai
 
Back
Top Bottom