Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Atakayechukua nafasi ya Saidi Mwema kama IGP Ni Kamishna Ernest Mangu.

Ataapishwa kesho.

8850079_orig.png

Ernest Mangu

​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua
​

nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la Polisi.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).

Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
​
Hongera kamanda Mangu
 
Kuna tofauti kubwa kati ya intelligence na investigation. Intelligence kwa maneno machache ni utaratibu wa kukusanya taarifa mara nyingi kwa njia ya siri na kuzifanyia analysis ili kupata usahihi wa taarifa hizo. Katika muktadha huo, Directorate ya Criminal Intelligence ina wajibu wa kukusanya na kutafuta taarifa kuhusu uhalifu wa kijinai hata kabla ya kutokea kwa uhalifu huo. Mathalani, kama kuna mtu au kikundi cha watu kinakusudia kufanya aina fulani ya uhalifu ni jukumu la Directorate hii kupata taarifa za mtu au kikundi hicho kabla hakijafanya uhalifu husika na kuchukua hatua stahiki za kuzuia uhalifu huo. Hiki si kitu kipya kwa Jeshi la Polisi bali sasa kitengo cha intelligence kilichokuwa chini ya DCI kimeimarishwa kuwa Idara kamili. Hii ni kama ilivyo kwa Military Intelligence kwa jeshi lolote ikiwemo TPDF. Kwa upande wa investigation, huu ni uchunguzi wa makosa ya jinai ambayo tayari yameshatendeka. Kusudi hapa ni kupata ushahidi wa kuthibitisha uhalifu wa kijinai uliotendeka mahakamani. Kuteuliwa kwa Naibu IJP kunafuatia muundo mpya wa Jeshi la Polisi ambao pamoja na mambo mengine umeongeza Idara na vitengo ambavyo awali havikuwepo katika Jeshi la Polisi. Ongezeko la Idara hizo linahitaji uwepo wa Naibu IJP wa kusaidia usimamizi na uendeshaji wa shughuli za jeshi. Hii ni kama ilivyo kwa TPDF ambapo kuna Chief of Staff ambaye hushughulikia masuala ya kila siku ya utawala ndani ya jeshi.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums

Umeelezea vizuri like one of them ...Alsante.

Taarifa za kiintelejesia ahahaaaaaaaa tumekuwatukisikia sana maneno recently kumbe ni matunda ya hiki kitengo
 
Jk najua haya mabadiliko ndio mwendelezo wa uwajibikaji wa operation tokomeza sema hutaki kusema tu kulindiana heshima.Bado kule "jikoni" yule mwenye mikasi begani nae awajibishwe pamoja na askari waliotekeleza huu unyama na ule wa Mtwara wakamatwe tuwaone hadharani na msituletee "vichaa wa Kenya" tena.Hili liwe funzo.
 
Kila la heri,Ispector Mangu,katika utekelezaji wa majukumu yako mapya.
(a)Tutapima utendaji wako kwa namna Jeshi la Polisi kote nchini litakavyotekeleza dhana ya Haki za Binadamu,Utawala wa Sheria na Demokrasia.
(b) Tungependa kuona usalama wa raia na mali zao unaimarishwa.
Hongera sana.
 
Kwa hatua tuliyofikia hapa nchini, ukipewa cheo cha umma usikubali pongezi maana wengi hudhani ni nafasi ya ulaji bali ni nafasi ya uwajibikaji na utendaji. Kwa kuwa waliokutangulia wameonekana kuwa ni wapigaji hadi wengine kufikia hatua ya kushutumiwa kutumia baadhi ya walio chini yao kujinufaisha, basi tukutakie tu utendaji mwema na utekelezaji wa majukumu yako mapya kama IGP na tukikukumbusha tu kuwa nchi hii ni yetu sote, tusiyumbishwe kuitendea tofauti na akili zetu halisi na maarifa vinavyotuongoza kutenda kwa maslahi ya wapigaji na wezi wa raslimali.
Ombi tu kwako IGP mpya: epuka kuandaa sherehe ya kujipongeza na maua ya kujaza pale viwanja vya IKULU hapo baadae maana vitakupumbaza tu na kukufanya ujione umeula, kumbe umewekwa kwenye nafasi ngumu. Kwangu mimi sitofautishi ugumu wa kazi ulonayo na ile ya uwaziri wa maliasili na utalii (nakumbuka Kagasheki wakati anaapishwa katika mahojiano alisema anfahamu changamoto za wizara ile na kuomba watanzania wamuombee aweze kusimamia raslimali za Taifa kwa manufaa ya watanzania wa leo na wa kesho, lakini kwa kuwa wizara ni kisiki cha mpingo, kama jina la jengo lenyewe MPINGO house, basi aliyoyatabiri kama changamoto yamemkumba: wajanja wajanja na wenye mkono mrefu wamehakikisha anang'oka).
Ikiwezekana mwambie kabisa mkeo na wanafamilia yako waungane kukuombea katika utendaji na siyo kukubebea MIZIGO ya maua na mashada kukupongeza, maana soon wanaweza wasiamini watakachokua wanakisikia mitaani kuhusu IGP Mangu (Mume na Baba na ndugu yao).
Kila la kheri,

Tukutane katika uwajibikaji na utendaji safarini katika OFISI ZA UMMA kote nchini.
 
Mangu sina ufahamu wake ila huyu kamishna Kaniki ni msomi na mwalimu mzuri tu wa sheria na anaifahamu sheria hasa,

Nakumbuka wakti ule miaka kati ya 1980 na 1990 Kaniki alivuma sana kwenye vipindi vya elimu kwa umma vya jeshi la polisi.

Ameandika makala kadhaa za kisheria zikiwemo ile ya "Treatment of Older People" na ile ya "Dissolution of Muslim Marriages".

Ni juzi juzi tu naibu IGP Kaniki alikuwa nasi pale Ankara kuhudhuria kozi ya mwezi mmoja ya ku-iprove performance kwenye utendaji wa jeshi la polisi.

Pale tulijifunza uchunguzi maalum, namna ya kuendesha magari katika mazingira yenye utata na kikubwa zaidi ni teknolojia mpya ya kufanya uchunguzi wa maabara ambayo kamishna Kaniki hilo ni eneo lake.

Ni mtaalam mzuri tu ila tatizo watu wakipewa madaraka wanalewa na kuwa chakari kiasi cha kuacha raia wasio na hatia wakiuawa pasina sababu yoyote ile.

Kila la kheri maIGP wetu wapya.

CC: Chris Lukosi.
 
na uishie hapohapo maana nyie mareject mliacha kazi za umma na kwenda kuishia kufanya packing ya maboksi na spea za used

Aaah Mkuu Timing acha hizo,

Chris Lukosi "is very successful businessman".

teh-teh-teh!
 
Ablrahaman ndo kaula. Tangu uhuru hamna hiyo kitu. Labda ni kuweka usawa wa kidini. Inabidi huyo naibu afanye kazi kubwa ya kummonitor boss..hahahaaaa....!!!!
for shizzle man, bila kusahau wananchi wanakamuliwa fedha kuwalipa mishahara wote .
 
Naamini utatenda haki na mabwepande itafungwa, watu watakuwa na amani na kucha na meno yao haitang'olewa tena. Kazi njema E. Magu.
 
Kamanda huyu wa Mwanza anaheshimika sana ndani ya Jeshi la Polisi. Tangu achukue mikoba iliyoachwa wazi na hayati Liberatus Barlow aliyekuwa akishikilia wadhifa huo na kuuawa kikatili, Mangu amefanya vema.
Anatajwa kuwa msomi wa shahada ya kwanza katika Sayansi ya Polisi (Police Science) aliyoipata ughaibuni. Anaelezwa kuwa msimamizi mzuri wa misingi ya upolisi kama ilivyoainishwa katika Police General Order (PGO).
Siku hizi, askari hawafuati misingi ya upolisi kama ilivyo kwenye PGO. Misingi inasema, kwa mfano, askari hatakiwi kuacha lindo hadi mwenzake afike lakini siku hizi askari anaacha silaha lindoni kabla mwenzake hajafika.
“Ni jambo la kawaida siku hizi kuona askari akiingia kazini huku amelewa. Lakini kwenye PGO unaambiwa kabla askari hajaingia lindoni ni lazima akaguliwe lakini hilo halifanyiki siku hizi. Mangu anaweza kusimamia PGO,” kilisema chanzo hicho.
- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/watatu-wapitishwa#sthash.UqElBqUp.dpuf
 
Mimi nachukia kweli mtu kuchezea katiba, sina namna, huyo sijui tulimtolea wapi?? ametoa sababu gani za kuongeza matumizi??? Je mangu hana uwezo vizuri hadi awekewe mtu karibu kabisa nyuma yake??? amemteua magu wa nini kama hana uwezo sawia???

Jamani soma taarifa ya kutoka Ikulu, tusipende kuwa negative na kila kitu
 
Heko JF maana....mlichambua possible candidates wa hiyo nafasi na wala hamkuwa mbali na matokeo.......ilikuwa ni Mangu, Andengenye na Kaniki.....naona wawili wamepita....heko JF!.........
 
Back
Top Bottom