high vampire
JF-Expert Member
- Nov 17, 2012
- 2,939
- 2,181
Hakuna kitu
kumbe anatabia ya kulindana wewe utakuwa mfanyabiashara maana mfanyabiashara wanakimbilia polisi kuficha mapungufu yao
kumbe anatabia ya kulindana wewe utakuwa mfanyabiashara maana mfanyabiashara wanakimbilia polisi kuficha mapungufu yao
Niliwahi kutoa comment hapa siku moja kuhusiana na suala la IGP mpya na nikasema kati ya wale watatu waliokuwa wanatajwa mangu akiwepo nilisema Mangu ndiye anayefaa kushika nafasi hiyo baada ya Said Mwema ambaye kimsingi hakupenda kuendelea na nafasi uake hiyo hata baada ya kuombwa.
Pengine anajua ni kwa nini amekataa,lakini kwangu mimi nasema safi yeye kuacha hiyo nafasi ili wengine waipate na waifanyie kazi inayotakiwa.
Jeshi la Polisi ni Jeshi kubwa ambalo lipo hadi vijijini,tofauti na majeshi mengine ambayo yanaishia mkoani tu ama wilayani tena kwa uchache.
Ni jeshi ambalo linahitaji mtu walau mwenye uelewa na shule hata kama si kubwaa saaaana lakini aongozwe zaidi na Busara!
Kwa mtu yeyote ambaye amewahi kukaa meza moja na Mangu atakubaliana na miji kwa haya ambayo nakwenda kuyasema.
Mangu ji miongoni mwa askari polisi ambao wametuloa sana na wanalijua vizuri sana jeshi hili.
Ni mtu ambaye hakurupuki katika kutoa maamuzi hata kidogo anapenda kujiridhisha kwanza kabla ya kuchukua hatua,na ikibidi anaingia field mwenyewe.
Nimefanikiwa kukutana naye kwenye mambo matatu hivi pale jijini mwanza mazito kweli kweli ambayo yalikuwa yamelikamata taifa lakini moja likiwa ni mkoa huo wa mwanza ni mtu ambaye ametulia sana.
Katika mazungumzo baina yangu na yeye ambyo yalidumu kwa wiki nzima kwa kila tukio hapo mwanza,alionekana mtulivu sana na umakini wa hali ya juu katika majibu.
Na niseme tu jambo moja yeye ndiye pia aliyemuokoa kigogo mmoja wa serikali katika mkoa huo asifukuzwe kazi baada ya kuvurunda katika moja ya matukio hayo matatu.
Ujinga unaondelea ndani ya jeshi la polisi hivi sasa kwa baadhi ya askari kugeuza watu miradi yao naamini muda wao umefika.
Ni mtu asiyeshikiliwa akili kama ambavyo wakati mwingine mtangulizi wake alikuwa anafanya yeye hana labda abadilike!