Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Mimi nachukia kweli mtu kuchezea katiba, sina namna, huyo sijui tulimtolea wapi?? ametoa sababu gani za kuongeza matumizi??? Je mangu hana uwezo vizuri hadi awekewe mtu karibu kabisa nyuma yake??? amemteua magu wa nini kama hana uwezo sawia???
 
Tumeshasahau kuhusu udini naona JK ameanza kuuchokonoa tu! Hivi huyo Naibu IGP ni wa nini? Huu ni udini tu unaomsumbua huyu Rais wetu aliyevunja record ya kupanda Ndege nyingi na mara nyingi sana lakini hajui hata Blackbox ni nini.

mzee wa kubalance

Sijaelewa naibu igp ni wa kazi gani hapo,hata kama angekua mkristo!

Someni vizuri huo ujumbe kuna muundo mpya wa jeshi la polisi ndiyo unafuata. tujadili uwezo wao
 
Kwani kulikuwa na ulazima wa kumua kamanda Barlow?...Bora waliokuwa wanamhofia wote hawakupa ...
 
Nadhani tukielewa majukumu ya Naibu IGP itamaliza hofu iliyotanda.
 
Namchukia sana mtu ambaye kabla ya kumteua mtu kushika nafasi anaanza kujiuliza, huyu ni wa dini gani, nitafanyaje kubalance dini, n.k. Mteue mtu kwa kuangalia uwezo wake bila ya kujali kama mi muislam, mkristo au mpagani.

Kikwete anafanya kosa kubwa kwa kufikiria kuwa akiwateua watendaji wake kwa kubalance dini ndiyo ataonekana ni kiongozi mzuri. Kikwete ataingia kwenye kumbukumbu kwa kuwa Rais mdini. Kuwa mdini hakumaanishi kuwapendelea watu wa dini yako bali ni kufanya mambo kwa mtazamo wa dini ya mtu. Hata pale Rais anapoamua kuwa nafasi hii sasa nimpe mtu wa dini fulani kwa vile aliyetangulia alikuwa wa dini fulani, nao ni udini.

Jk ametengeneza cheo cha Naibu Mkuu wa Polisi, ambacho hakipo kwenye muundo wa jeshi la polisi kwa nia ya kuwafurahisha maswahiba wake hata bila ya kuwepo sababu za msingi za kutengeneza nafasi hiyo. Hapo ndipo udhaifu wa uongozi wa Kikwete unapoonekana wazi.

Tumeshasahau kuhusu udini naona JK ameanza kuuchokonoa tu! Hivi huyo Naibu IGP ni wa nini? Huu ni udini tu unaomsumbua huyu Rais wetu aliyevunja record ya kupanda Ndege nyingi na mara nyingi sana lakini hajui hata Blackbox ni nini.
 
we need postive changes to police officers and community,
not propaganda,We wish you good responsibilitiez,comitement & transparence.
 
Ukifuatilia siasa za TZ IGP akiwa kutoka upande mfano wa Christian waislamu wenye msimamo mkali kila jambo likiwatokea wanasema waneonewa. It is good kuwaonyesha kwamba ni taifa tu!

Jadilini hoja acheni udini.kwani umeambiwa IGP ni kiongozi wa kanisa au msikiti?
 
Director of Criminal Investigation=Mungulu
Director of Criminal Intelligence =alikua Mangu!
Ni vitu viwili tofauti


Tutajie tofauti kubwa hiyo.
How you perform investigation without involving intelligence ?
Kama kuna anayejua role Director of Criminal Investigation na Director of Criminal Intelligence atusaidie tafadhali
Of course mara nyingi tulikuwa tunamsikia Director of Criminal Investigation kidogo tunajua role yake sasa huyo mwingine.....?
 
Jadilini hoja acheni udini.kwani umeambiwa IGP ni kiongozi wa kanisa au msikiti?

Hongera kamanda mpya, ila ktk utendaji wako wa kila siku kumbuka KUCHANGANYA na za kwako
 
Rais angefanya Staili ya Uganda,Kenya , na Rwanda ya kuwateua Majenerali toka Jeshini Kuwa wakuu wa Polisi kwani uzoefu umeonyesha Kuwa wakiwa ni wanajeshi nidhamu ndani ya jeshi inaimarika zaidi kuliko wakitawaliwa na IGP anayetoka humo humo polisi .
 
Duh naanza kuamini savimbi yu karibu na mkulu,Mangu!anatoka usingidani huyu.Hautapita muda tutajua rangi zake halisi.
 
Rais angefanya Staili ya Uganda,Kenya , na Rwanda ya kuwateua Majenerali toka Jeshini Kuwa wakuu wa Polisi kwani uzoefu umeonyesha Kuwa wakiwa ni wanajeshi nidhamu ndani ya jeshi inaimarika zaidi kuliko wakitawaliwa na IGP anayetoka humo humo polisi .

unaongelea Kenya ipi ? wenzio wapo kidemokrasia,Igp anafanyiwa Vetting..siyo mambo ya "ikimpendeza" rais..! nafasi nyeti zote wahusika wafaniwe vetting.
 
Back
Top Bottom