Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

Hicho cheo cha naibu mh!manaibu hadi kwenye majeshi?kweli Tanzania siasa kila mahali,anyway,labda anajaribu kupunguza kelele za "mfumo kristo" manake huyu kamanda Ernest angeteuliwa peke yake kusingekalika!
 
NAIBU IGP...wa nn..?? No need at all....I hope hata hii nafasi kikatiba haipo....so JK hapa kakosea kabisa kabisaa....OMG....!!!
 
Hizi huteuliwa kwa process zinzoendeshwa na kamati ya ulinzi na usalama kinachomshauri raisi kuteua viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kama jwtz, polisi, Tiss na kadhalika. Hivyo c suala la udini wala upendeleo bali ni uweledi na ufanisi wa majukumu ndio inayopelekea kuwateua wasaidizi kwa wakuu wa majeshi na vitengo vya usalama.
 
hapo hakuna cha usawa wote ni wasilamu, mdogo wake na Ernest mangu ni rafiki yangu fika, anaitwa Juma Mangu yuko mwanza na anafanya kazi Idara ya maji.


Basi hata huyu Ernest atakuwa wa idara ya maji mkuu hebu mwambie juma adadavue fresh! !!!!!!
 
Hicho cheo cha naibu mh!manaibu hadi kwenye majeshi?kweli Tanzania siasa kila mahali,anyway,labda anajaribu kupunguza kelele za "mfumo kristo" manake huyu kamanda Ernest angeteuliwa peke yake kusingekalika!


Hata angemchagua mslamu mwingine kama anasifapoa tuu....haya mambo ya zamu hayafai
 
Kuna tofauti kubwa kati ya intelligence na investigation. Intelligence kwa maneno machache ni utaratibu wa kukusanya taarifa mara nyingi kwa njia ya siri na kuzifanyia analysis ili kupata usahihi wa taarifa hizo. Katika muktadha huo, Directorate ya Criminal Intelligence ina wajibu wa kukusanya na kutafuta taarifa kuhusu uhalifu wa kijinai hata kabla ya kutokea kwa uhalifu huo. Mathalani, kama kuna mtu au kikundi cha watu kinakusudia kufanya aina fulani ya uhalifu ni jukumu la Directorate hii kupata taarifa za mtu au kikundi hicho kabla hakijafanya uhalifu husika na kuchukua hatua stahiki za kuzuia uhalifu huo. Hiki si kitu kipya kwa Jeshi la Polisi bali sasa kitengo cha intelligence kilichokuwa chini ya DCI kimeimarishwa kuwa Idara kamili. Hii ni kama ilivyo kwa Military Intelligence kwa jeshi lolote ikiwemo TPDF. Kwa upande wa investigation, huu ni uchunguzi wa makosa ya jinai ambayo tayari yameshatendeka. Kusudi hapa ni kupata ushahidi wa kuthibitisha uhalifu wa kijinai uliotendeka mahakamani. Kuteuliwa kwa Naibu IJP kunafuatia muundo mpya wa Jeshi la Polisi ambao pamoja na mambo mengine umeongeza Idara na vitengo ambavyo awali havikuwepo katika Jeshi la Polisi. Ongezeko la Idara hizo linahitaji uwepo wa Naibu IJP wa kusaidia usimamizi na uendeshaji wa shughuli za jeshi. Hii ni kama ilivyo kwa TPDF ambapo kuna Chief of Staff ambaye hushughulikia masuala ya kila siku ya utawala ndani ya jeshi.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Hongera watanzania tunategemea uongoz uliotukuka na co kuongoza kwa mazoea ya mwema weka kapun njoo na mipango mipya
 
Hongera,lakini tunahitaji kuona akishughulikia haraka wale wote waliohusika na operation tokomeza ujangili akiwemo Said Mwema.
 
Huyu Bwana Mangu ni clean tena msomi naomba Mungu asije akawa KIKWAZO sababu ya siasa!:hand:
 
Back
Top Bottom