Kamishna Ernest Mangu ateuliwa kuwa IGP mpya

kiwatengu

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
16,271
2,000
Atakayechukua nafasi ya Saidi Mwema kama IGP Ni Kamishna Ernest Mangu.

Ataapishwa kesho.

8850079_orig.png

Ernest Mangu


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua

nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.

Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la Polisi.

Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.

Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).

Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

============
Wasifu wake:

IGP mteule Ernest Jumbe Mangu alizaliwa mwaka 1959 mkoani Singida na alipata elimu ya Sekondari katika Shule ya Tumaini mwaka 1981.
Alijiunga na Jeshi la Polisi katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP) tarehe 17 mwezi Agosti mwaka 1982 na kuhitimu mwezi Juni mwaka 1983 ambapo alipata mafunzo ya awali ya Polisi.

Mwaka 1987 alipata mafunzo ya sheria kwa ngazi ya cheti katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mwezi Novemba mwaka 1992 alitunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Mwezi Juni mwaka 2010, alitunukiwa shahada ya udhamili katika masuala ya usalama katika Chuo Kikuu Cha Usalama cha Marekani.

Akiwa ndani ya Jeshi la Polisi amepandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Koplo wa Polisi (1988), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1992), Mkaguzi wa Polisi (1995), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (1997), Mrakibu wa Polisi (2002), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2004), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2006), Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (2010), Naibu Kamishna wa Polisi (2013) na Kamishna wa Polisi (2013).

Amewahi kufanya kazi kama Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mwanza, Kamanda wa Polisi katika mikoa ya Pwani na Mwanza na Kamishna wa Intelijensia ya Jinai.​
 

lutayega

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
1,275
2,000
Mwenye cv yake na taarifa kuhusiana na utendaji wake atuwekee tuone kama anatofauti na mwema
 

Miaghay

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
1,473
1,250
Uteuzzi huo umetolewa sasa hivi kuwa IGP Mpya ni Ernest Mangu na anachukua nafasi ya Said Mwema. Kabla ya Uteuzi huu wa leo kuwa IGP, Kamanda Mangu aliteuliwa wiki chache zilizopita kuwa DCI na sasa anakuwa IGP.

Aidha Kamishna wa Polisi Abdulrahmani Kaniki ameteuliwa kuwa Naibu IGP cheo ambacho ni kipya ndani ya Jeshi la Polisi.
weka source.
 

samaki2011

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
1,775
0
Sidhani kama kuna jipya. Natarajia mapya baada ya ccm kutoka madarakani out of that expect nothing. Mtajifariji tu na kujilisha upepo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom