Mzalendo Mkuu
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 735
- 191
Bora amestaafu maana hakuwa na tabia za ukamanda! Alikuwa legelege sana. Atupishe tujenge nchi.
Bora amestaafu maana hakuwa na tabia za ukamanda! Alikuwa legelege sana. Atupishe tujenge nchi.
Tumeshasahau kuhusu udini naona JK ameanza kuuchokonoa tu! Hivi huyo Naibu IGP ni wa nini? Huu ni udini tu unaomsumbua huyu Rais wetu aliyevunja record ya kupanda Ndege nyingi na mara nyingi sana lakini hajui hata Blackbox ni nini.
Atakayechukua nafasi ya Saidi Mwema kama IGP Ni Kamishna Ernest Mangu.
Ataapishwa kesho.
![]()
Ernest Mangu
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua
nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la Polisi.
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic Investigations).
Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
Hongera sana kamanda
Jeshini yupo mnadhimu mkuu wa jeshi, ambae ni cheo cha pili na msaidizi wa CDF. Nafikiri nako polisi wanataka kuadopt mfumo huo!
...mwema kafukuzwa kwa kuharibu,bado mwamunyange,nae aondolewe haraka....
hongera ! Tunategemea kwamba utaondoa vitu vyote vyenye ncha kali pale makao makuu ya polisi , maana vimedhuru wengi sana ! usisahau kumshughulikia KAMUHANDA hatujasahau kifo cha mwangosi .
ni sawa na naheshimu success yake, but that doesnt take away the fact that anafanya packing na shipping... kwikwikwikwikwiii [labda angekua hapa na huu ukada wa chama chake angekua mbali sana, wangempa vyeo lukuki]Aaah Mkuu Timing acha hizo,
Chris Lukosi "is very successful businessman".
teh-teh-teh!
Nani ka kuambia. Mangu ni mtu wa moshi?hio damu ya singida mnyaturu in Nature
Mbona kwa uteuzi huu wa ernest jk haitwi mdini!? Lkn kwa ule wa naibu wake anaitwa mdini!? Katiba inamruhusu amiri jeshi mkuu (rais) kuunda cheo cha kijeshi