matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,596
- 15,391
Maombi ni moja ya njia ya kuondoa wasiwasi na kuongeza imani katikati ya changamoto na sintofahamu za maisha.
Lakini kama hujui kuomba vizuri unaweza kujikuta yanakuongezea stress, wasiwasi, hata kushusha imani yako kwa Mungu. Na hii imepelekea watu kucheza miguu miwili. Mmoja kwa Mungu mwingine kwenye utamaduni kificho.
Kosa liko wapi.
Unapoanza maombi unaanza kwa kutanguliza shida na masumbufu yako badala ya kutanguliza ukuu na uweza wa huyo Mungu kwanza.
Tumia muda mwingi katika utangulizi kumtambua Mungu, uweza wake, ukuu wake sifa zake na utukufu wake. Hii itakufanya akilini mwako uone Ukuu wa Mungu na katatizo kanafifia hata kabla hujakataja. Ukifika wakati wa kueleza unachotaka basi unakuwa na uhakika na huyo unayemuomba maana unajua akilini fika anauwezo gani.
Kutanguliza kuvurumisha matatizo yako kama kipaumbele, unayakuza kuliko uwezo wa Mungu akilini mwako. Hivyo unamkuza shetani na uwezo wake kwako Kuliko Mungu. Unampa nafasi kubwa kuliko Mungu. Hivyo maombi ya kumbrand shetani na uwezo wake huwa yanaarika majini badala ya malaika. Yanajaza hofu, mashaka na wasiwasi.
Mfano wa hili fundisho ni story ya Mfalme Yehoshafat 2Nyakati 20. Namna walivyoanza maombi ni kwa kumtambua Mungu na uweza wake kisha wakamsakizia matatizo yao. MUNGU ALIINGILIA KATI KWA KASI YA AJABU.
HII NDIO MAANA YESU ALIFUNDISHA TUANZA KUOMBA KWA KUSEMA " BABA YETU ULIYE MBINGUNI, JINA LAKO LITUKUZWE, UFALME WAKO UJE".
Hii ni kama frame work wewe hapo unatakiwa kujaza maneno mengi kwenye hii sentensi ya Yesu.
Ni hayo tu.
Kama umepata kitu, sema amina.